Nimekuwa mtu mwema nimeishia kudharaulika naombeni mbinu za kuwa na roho mbaya nisiye na hisia

Nimekuwa mtu mwema nimeishia kudharaulika naombeni mbinu za kuwa na roho mbaya nisiye na hisia

lee jack

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Posts
1,062
Reaction score
1,871
Habari zenu jamii forum kama kichwa cha Uzi kinavyosema naombeni mnisaidie mbinu za kuwa mtu mwenye roho mbaya nisiwe na hisia za huruma wala upendo.

Nimekuwa mtu mwema kwa watu nimeishia kuumizwa na kudharaulika pamoja na kutumika tuu huku wenye roho ngumu na mbaya wakifanikiwa na kupeta na maisha.

Sihitaji ushauri wa dini wala mahubiri nataka ushauri wa kiintelijensiaa.

Nawasilisha.
 
Kama si wa roho mbaya toka awali, ukiiga utapitia wakati mgumu sana kuliko ulopitia nyuma.

Kila life style ina changamoto zake hivo usidhani wenye roho mbaya wanateleza tu.
Kila kitu kina mwanzo wake nitajifunza ukatili mpaka nibobeee
 
Habari zenu jamii forum kama kichwa Cha Uzi kinavyosema naombeni mnisaidie mbinu za kua mtu mwenye roho mbaya nisiwe na hisia za huruma Wala upendo

Nimekua mtu mwema kwa watu nimeishia kuumizwa na kudharaulika pamoja na kutumika tuu huku wenye roho ngumu na mbaya wakifanikiwa na kupeta na maisha

Sihitaji ushauri wa dini Wala mahubiri nataka ushauri wa kiintelijensiaa

Nawasilisha
Wafuatao wana skills hizo watakusaidia mkuu🤣
Lucas Mwashambwa
Tlaatlaah
chiembe
johnthebaptist

Cheki nao inbox, watafanikisha ndoto yako😃
 
Inabidi uchunguzwe, maana magaidi walianza hivi hivi....mwishowe wakawa viongozi wa vikundi vikubwa vya kigaidi duniani
 
Ingratitude is a human nature and it's like natural weeds expect nothing from anyone they said jesus healed many people from leprosy but only one turned back to thanks him so relax mkuu binadamu ndio walivyo.
 
Wafuatao wana skills hizo watakusaidia mkuu🤣
Lucas Mwashambwa
Tlaatlaah
chiembe
johnthebaptist

Cheki nao inbox, watafanikisha ndoto yako😃
Macho na maskio ya waTanzania wote yapo Songea uwanja wa maji maji nyie mnafanya nini hapa, gentlemen?

ni vizuri mkazingatia kinachoendelea uwanja wa maji maji songea, umefurika watu aise, na ni muhimu zaidi kuskiza hotuba ya Rais, ni jambo la maana zaidi 🐒
 
Kuwa na roho mbaya ni kutojali yale watu wanayosema,maana unapojali unaruhusu nishati chanya au hasi kufanya kazi kwa maisha yako,hivyo ili uwe na roho nzuri kwako lakini mbaya kwa wanaokuzunguka,ni kuhakikisha hujiingizi au humfanyii mtu yeyote jambo ambalo wewe hakufanyii,kwa kufanya hivyo utaweza kuilinda nishati yako bila kupoteza, ulishawai kuona mtu anaeongea na watu zaidi ya watatu kwa wakati mmoja,na anataka waelewane vizuri? Hilo haliwezekani kwa sababu umeme mwingi unapotea wakati unapotaka kila mtu umridhishe na matokeo yake hutaweza kujuwa nguvu zako ziliko.
 
Macho na maskio ya waTanzania wote yapo Songea uwanja wa maji maji nyie mnafanya nini hapa, gentlemen?

ni vizuri mkazingatia kinachoendelea uwanja wa maji maji songea, umefurika watu aise, na ni muhimu zaidi kuskiza hotuba ya Rais, ni jambo la maana zaidi 🐒
Tunajua anachokifanya muuaji huyo ni kusaka huruma ya chama ionekane wote wanahusika.

Wauaji wanateteana.
 
Back
Top Bottom