Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Yeah uko sahihi mkuu. Huenda jamaa anatamani amuoe ila anashindwa kutokana na tabia zake.

Tabia zipi? Sina tabia za ajabu japo pia sipo perfect kama binadamu wengine tu. Na ndio mara ya kwanza nimeanzisha mahusiano nje ya haya tulokuwa nayo. Na naona kabisa siwezi kumudu kuwa na wanaume wawili kwa wakati mmoja. Soon nitakamatwa tu, kwahiyo kabla hayajanikuta ya kunikuta ndio nataka nimuache mmoja.
 
Hawa viumbe ni wabinafsi sana ni wa kuishi nao kwa akili sana. Kuna mdau kasema hapo chukua mkopo then jifanye huwezi kuulipa ili akuone duwanzi akuache. Nami naungana nae maana naona kama ukilianzisha wewe utapigwa na kitu kizito.
Hapana sisi sio wabinafsi ila tunapenda kutawala tunavyovimiliki na hapo ndipo penye wivu na maumivu kadha wa kadha. Ni kama Mungu tu,pale ambapo anaona kiumbe wake anaabudu miungu wengine kwake huwa inakuwa nongwa tena sio ndogo. Tuna hali ya asili ya kutetea 'mamlaka' tuliyopewa ingawa kuna wanaume wenzetu kwa kujua au kwa kutokujua wanaitumia hovyo mamlaka hiyo.
 

Lakini kwa hayo waliyofanya yalionekana ni machukizo mbele za Mungu maana tumeagizwa kuwa mume wa mke mmoja tu hadi kifo kiwatenganishe. Mtumishi wa Mungu akitenda dhambi haihalalishi hiyo dhambi bali linapaswa kuwa funzo kwetu kuwa unapozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo shetani anavyokuandama zaidi. Hivyo tunapaswa kuendelea kuzitetea imani zetu na tukianguka tutubu na kusimama tena.
 
Haya dada, uamuzi ni wako, ila nachojua mimi uhawala huwa haufi hasa kama mlipendana vizuri! naposema kurasmisha simaanishi mkafunge ndoa kanisani, bali muyaweke wazi mahusiano yenu na kutafta namna ya kuwezesha jamii au familia zenu kuyapokea na kuyatambua! Huyo sio Mkristo wa kwanza kuoa wake wawili!
 
Kwa hiyo wewe unamzidi Imani Ibrahimu?
 
Mamlaka kama mamlaka sio? Basi sawa.
 

Natambua hilo ndio maana naogopa sana kufanya maamuzi. Alishawahi kuniambia nisifikirie hata kumsaliti yaani isitokee hata kwa bahati mbaya.
 

Nimekuelewa, ila hilo ni gumu sana.
 
Kabla ya yote jipe muda wa kutosha sana,tafakari ni nini unahitaji kwenye maisha yako. Kisha orodhesha.

Kujua upande basi gani ni muhimu kwanza ujue unakotaka kwenda. Kwa maoni yangu hii ni changamoto ambayo ni mtoto wa tatizo la wewe kutokujua vipaumbele vya maisha yako. Usipokata mzizi matawi yataota tena na tena.
 

Shukrani sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…