Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Yeah uko sahihi mkuu. Huenda jamaa anatamani amuoe ila anashindwa kutokana na tabia zake.

Tabia zipi? Sina tabia za ajabu japo pia sipo perfect kama binadamu wengine tu. Na ndio mara ya kwanza nimeanzisha mahusiano nje ya haya tulokuwa nayo. Na naona kabisa siwezi kumudu kuwa na wanaume wawili kwa wakati mmoja. Soon nitakamatwa tu, kwahiyo kabla hayajanikuta ya kunikuta ndio nataka nimuache mmoja.
 
Hawa viumbe ni wabinafsi sana ni wa kuishi nao kwa akili sana. Kuna mdau kasema hapo chukua mkopo then jifanye huwezi kuulipa ili akuone duwanzi akuache. Nami naungana nae maana naona kama ukilianzisha wewe utapigwa na kitu kizito.
Hapana sisi sio wabinafsi ila tunapenda kutawala tunavyovimiliki na hapo ndipo penye wivu na maumivu kadha wa kadha. Ni kama Mungu tu,pale ambapo anaona kiumbe wake anaabudu miungu wengine kwake huwa inakuwa nongwa tena sio ndogo. Tuna hali ya asili ya kutetea 'mamlaka' tuliyopewa ingawa kuna wanaume wenzetu kwa kujua au kwa kutokujua wanaitumia hovyo mamlaka hiyo.
 
Mfalme Sulemani alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Mfalme Daudi alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Haya, Ibrahimu ambaye wewe mwenyewe unamuita baba wa Imani alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Au wewe Mungu wako ni bora zaidi ya Mungu wa Ibrahimu, Yacobo na Isaka?

Lakini kwa hayo waliyofanya yalionekana ni machukizo mbele za Mungu maana tumeagizwa kuwa mume wa mke mmoja tu hadi kifo kiwatenganishe. Mtumishi wa Mungu akitenda dhambi haihalalishi hiyo dhambi bali linapaswa kuwa funzo kwetu kuwa unapozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo shetani anavyokuandama zaidi. Hivyo tunapaswa kuendelea kuzitetea imani zetu na tukianguka tutubu na kusimama tena.
 
Haya dada, uamuzi ni wako, ila nachojua mimi uhawala huwa haufi hasa kama mlipendana vizuri! naposema kurasmisha simaanishi mkafunge ndoa kanisani, bali muyaweke wazi mahusiano yenu na kutafta namna ya kuwezesha jamii au familia zenu kuyapokea na kuyatambua! Huyo sio Mkristo wa kwanza kuoa wake wawili!
 
Kwa hiyo wewe unamzidi Imani Ibrahimu?
 
Hapana sisi sio wabinafsi ila tunapenda kutawala tunavyovimiliki na hapo ndipo penye wivu na maumivu kadha wa kadha. Ni kama Mungu tu,pale ambapo anaona kiumbe wake anaabudu miungu wengine kwake huwa inakuwa nongwa tena sio ndogo. Tuna hali ya asili ya kutetea 'mamlaka' tuliyopewa ingawa kuna wanaume wenzetu kwa kujua au kwa kutokujua wanaoitumia hovyo mamlaka hiyo.
Mamlaka kama mamlaka sio? Basi sawa.
 
Natambua hilo ndio maana naogopa sana kufanya maamuzi. Alishawahi kuniambia nisifikirie hata kumsaliti yaani isitokee hata kwa bahati mbaya.
 
Haya dada, uamuzi ni wako, ila nachojua mimi uhawala huwa haufi hasa kama mlipendana vizuri! naposema kurasmisha simaanishi mkafunge ndoa kanisani, bali muyaweke wazi mahusiano yenu na kutafta namna ya kuwezesha jamii au familia zenu kuyapokea na kuyatambua! Huyo sio Mkristo wa kwanza kuoa wake wawili!

Nimekuelewa, ila hilo ni gumu sana.
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Kabla ya yote jipe muda wa kutosha sana,tafakari ni nini unahitaji kwenye maisha yako. Kisha orodhesha.

Kujua upande basi gani ni muhimu kwanza ujue unakotaka kwenda. Kwa maoni yangu hii ni changamoto ambayo ni mtoto wa tatizo la wewe kutokujua vipaumbele vya maisha yako. Usipokata mzizi matawi yataota tena na tena.
 
Shukrani sana mkuu.
 
Back
Top Bottom