Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Hakuna Upendo wa kumnunulia gari na nyumba mwanamke alafu kesho akikuacha Ukubali tu ulifanya kwa upendo...!! Na hakuna watu wenye visasi vibaya kama wale ambao upendo ulitangulia kwanza yani Vita yake huwa ni kubwa sana. Usimdanganye mwenzio
Soma tena unachokisema ndicho nilichoandika
 
Kuna mawili mzalie au mrudishie vyote alivyokupa. Umejiingiza kwenye mtego wa shetani, Hakunaga cha bure tangia ulimwengu umeubwa
 
Ndugu yangu, ushauri wako ndio unaotakiwa kwa huyu dada,

Mimi mpaka leo kesi ipo mahakamani niachane na mtu kama huyu dada na story zake, hawa watu mnapoanza mahusiano huwa wanajua kila kitu kuhusu wewe na familia yako

Na wewe kwa upendo, huruma, na uungwana, unaamua kumjengea maisha mazuri,

Baada ya muda anaona alipotea, lakini kinachomwijia kuchwani muda huo ni dhambi kwamba kwa nini yeye ni nyumba ndogo,

Sasa mali anaitaka, na kuwa nyumba ndogo hataki, jibu hapo ni kurudisha mali za mtu na yeye asepe.

Mimi imenitokea nini?,

Wangu kafanya kila njia ili mimi nisepe, kaniweka, ndani, kaondoka kwangu miezi sita mala ya kwanza, akarudi kwa nguvu ili nimjeruhi anifunge,

Mala ya pili tena baada ya miaka miwili kupita kaaondoka tena karudi baada ya miezi nane, nimeamua kutokwenda kwake ( kwangu) na kufungua kesi ya kuachana,

Kesi sasa hivi ina miezi minne tunapigwa kalenda tu,

Jana kamleta mtoto makusudi nyumbani kwangu kwa mke wangu, ili kutest zari kwa mke wangu, bahati nzuri mke wangu anajua nini kinachoendelea, kamfukuzia mbali yule mtoto.

Mpomshauri kuwaamwambie mke wa jamaa wakati mwingine haisaidii sana.

Hawa viunmbe wakiishaanzisha mahusiano mengine ni rahisi sana kuchukua maamuzi ambayo wanaweza kuja kujutia
 
Kwakweli hana akili[emoji119]
Ndo wanaopigwa risasi hawa
 
Mbona simple tu. Mrudishie gari. Mrudishie nyumba. Anza upya tu na huyo bwege wako ndio utakapokuja kujua kwamba kumbe ulikuwa unamuacha ksbb tayari amekupa ujanja mjini. Ukajua utaendelea kuwa navyo hata usipokuwa nae
 
Indeed,hata km mi mwanaume nakuua
Bora useme wewe mwanamke labda wataelewa....tatizo ya warembo wanatamaa ya mali lakini wanashindwa tambua kuwa kila kitu kina oppportunity cost....alafu hapo hapo mwanamke anakwambia nikiwezeshwa na weza sasa kwa nini usitumie elimu uliyopata kupata hizo mali ambazo sponsor anakupa
 
Kabisa
 
Wanawake mko na roho mbaya sana, asilimia kubwa ya comments mpaka sasa zinatoka kwa wakina dada, lakini vile wanvyomkandia mleta mada badala ya kumsaidia wana msuta.
Kwa jinsi hawa wanaume wenye pesa wanavyoua wanawake waliowekeza kwao wakawaacha uanfikiri watamshauri nn?

Ye anataka ndoa ss,unafikiri itakuaje? Na alishamwambia atamfyatua akimzingua unategemea ashauriwe nn
 
Rudisha vitu vyake alivyokupa, afu muachane uone atafanya nn? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji848][emoji849]aisee mambo ni motooo ila umetisha aisee[emoji119]
 
[emoji87][emoji849][emoji848]wanawake wenzangu si mnayaona haya?!
Mhh kweli hakuna cha bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…