Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Loh watu wamekazana rudisha rudisha...kwani vinahusiana nini wajameni[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Mrudishie gari na nyumba kwanza halafu mengine yafuate, ili huyo mpya nae ajitolee
 
Kwanza nikwambie Hapo huwezi kutoka kwenye kifungo icho ulichokuwepo labda aamue mwenyew kukupotezea au Mungu amchukue, Si rahisi yeye kukuelewa kwa chchte kwa sababu ashawekeza vitu vingi kwako Ila all in all ulisema alikuonesha bastola kimasihara hio ilikua masihara Ila alifanya vile very serious so Kua makini Kama unataka umuache anza na kurejesha vitu vyake
 
Mwambie wazazi wako wamekutafutia mchumba na unataka uolewe wamekushinikiza...

Ikiwa vipi hizo mali mlizowekeza mnaweza mkagawana nae ili aende salama na wewe uende kivyako..., usipoangalia utakosa vyote...

Fanya haya jana na sio kesho..
 
Aya sasa wacha tukushauri.
Ushauri wangu hapa ni kwamba uhai ni muhimu. Ili uokoe uhai wako rudisha gari rudisha nyumba sema hivyo vyote sivitaki.
Kama unaona unataka chill with the big boys wee endelea tuu kumpa jamaa mbususu basi ule life ila sasa usije ukasaba isha kifo cha huyo kijana mwengine. So achana nae kabisaa na umwambie why. Wewe uishie kuwa na huyo mume wa mtu basi cha muhimu sii anakupa huduma bwana...security that money provides.

Out of topic. Inaelekea mrembo una tako na mbususu tamu mpaka jamaa anajenga nyumba[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Au auze nyumba kimya kimya. Aache ajira yake aingie zake mkoani. Namba atafute mpya, akaanze life upya.
 
Kinachonisikitisha zaidi,
Hii I'd ni ngeni Sana humu [emoji848]

Kuna kitu hakiko sawa mahali,
Hebu Ngoja nikanywe maji kwanza[emoji34]

Screenshot_20220217-224131.jpg
 
Back
Top Bottom