Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Rudisha mali zake ili uwe na maisha ya amani.. vitu hutafutwa ila uhai once ukiondoka haurudi tena...

Hama alipokupangishia ikiwezekana tafuta kazi sehem nyingine maana bila hivyo ataendelea kukutafuta.. piga block kila sehem.. hayo ni madhara ya kudate mume wa mtu .. pole sana kwa hali hiyo ya kujitakia.. unahitaji nawe uwe na familia lakini uliendekeza kudanga kwako kwa kumtegemea kila kitu..

Hivi dada unajiskiaje kudate na mtu ambae akitoka kwako anaenda kulala na mwanamke mwingine? Mnawezaje jaman.. I don't judge you by the way

'Mwanaume ukimfanya danga lako nae atakufanya malaya wake..'

Cc: DeepPond

Ahsante kwa kuniita mkuu,
Iyo Aya ya mwisho ndo umemaliza kila kitu[emoji4]

Mwanaume ukimfanya danga lako nae atakufanya malaya wake..' [emoji3578]
 
Mtu anipe kahawa kwenye hiki kijiwe wazee tumshauri huyu aende milembe udsm au central pol
 
kwahiyo unamshauri dada wa watu kufa sio. Akifanya hivo ajue wazi kabisa anakufa muda wowote afanye na maandalizi tuu. Na sasaivi watu wanavouana ni hatare.
Anampotosha mwenzie,
Iyo ndoa labda akaifungie kaburini apotee kabisa Kwny uso wa dunia[emoji4]
 
Sikuzote wamawake hua mtu kukufanyia hivo vyote simjinga wala upumbavu kiasi icho Kama uliona humpendi ungekataa vitu vyake na kazi yake kwa ujumla na ukimuacha ujue umeacha vyte hata kazi pia Kuna hatihati akakufanyia fitna usepeshwe na hata Huyo Mchumba mpya uliempata asikulevye inawezkana Kisa kakuona unakazi nzuri na Gari akaamua kujiweka Hapo Sasa ukose vyte utajua Kama anakupenda ama la
Na Hawa vijana wakujiremba wanapenda wanawake finished product.

Hawajui wakiona mwanamke anapendeza, Kuna jasho la mwanaume limevuja

Dawa ya hao barobaro nae unawatia adabu[emoji4]
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Daah unakwama wapi limwage fanya namna wambea wamwambie mkewe kisanuke, Ila pia huo usaliti wa ubwete uvuke daraja kisha utukane mamba ujipange, mimi ni kama huyo nakufyatua kweli na risasi, jipange yote yatakuhusu, dadadadeki... huyo ukimponyoka atakuwa fala sana. Mchuma janga hula na wa kwao.! Karma is real and equally a butch.
 
Wapendwa badala mnipe ushauri mnaniongezea magazijuto kweli? Najua i messed up big time and an not proud. Nisaidieni najikwamuaje hapa.
Nataka nikusaidie ila kura ya mwanaume siwezi kuisaliti ninayo njia tena ya hakika wote mnaendelea na maisha yenu, ila sio kwa dhambi hio unastahili adhabu kali kuliko kusaidiwa, nyie ndiomnatakiwa kuliwa kabsa nyama zenu hadi mifupa ya kongolo.
 
Mbona unayakimbia maisha uliyoyachagua mamkubwa [emoji849].

There is a price to pay to make the changes you want in life.
There is also a price you're already paying for staying the way you are

You have to weight these two prices and decide what to do based on that comparison and no one can do that for you. [emoji847]
We call it trade-off in economics
 
Hata siumizwagi na upuuzi Kama huu wa mtoa mada,

Binafsi Mimi nazijua fitna, afu nna visasi Sana. Afu kuniacha hawezi hata kwa dawa.
Afu akileta upumbavu na uyo anayemletea mahaba ya nyuki nae nadili nae ipasavyo mpaka achakae.

Vinginevyo akiniletea huo upuuzi ajiandae kujinguliza ahera mapema Sana yeye mwenyewe Maana baada ya hapo ataishi Hii dunia kwa mateso Sana.

Hatofanya kitu kikafanikiwa, nitamuandama bampa to bampa mpk anaenda futi 6 kaburini.

Sitakagi upuuzi kabisa Mimi[emoji3525]
Ila buda huu ukali wa ujumbe haufanani na tone ya simulizi, you were too lenient to let it go kwenye simulizi zaidi tu kuwe umelewa mbunyende mbunyende ya huyo manzi ambae hakupenda anapenda kivuko cha matunzo yako.
 
Tatizo umaskini,acha kazi, mrudishie nyumba yake, gari na nyumba aliyokupangishia halafu katafute mume wako ambaye pia atakuwa na michepuko yake….
Ukijifanya mjuaji utasomwa kweny taarifa za habari
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
kitu unachokitamani sasa badae utakuja ukijutie vivo hivyo.......kama umtaki sugar daddy mwambie njoo ijia mali zako uniache salama.....Alf uendelee na huyo kijana ulomsema....Ila kaa ukijua kuna wanaume pia ma gold digger kama ulivokua ww..... kua makini sana na uamuzi wowote utakaochukua

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom