Nimeifungua mahsusi ili niombe ushauri.
Kuna kitu kipo ndani yetu wanaume ambacho hamnacho nyie wanawake nacho ni kupenda.
Tunauwezo wa kupenda Mwanamke zaidi ya mmoja na kuheshimu wote kwa nafasi zao.
Kwenu wanawake ni changamoto kidogo kuwa na upendo kwa wanaume wawili.
Sisi tunaweza kutamani ukajua tumependa kumbe la!
Tunaweza kupenda ukajua tumetamani.
Kipimo cha mwanaume anayependa ni ile kujali na kuhudumia, fikiri mtu ama make na pengine ana familia lakini bado amejitoa kukujali na kukuhudumia na kukulinda.
Hapo hajakutamani bali amekupenda.
Na kama unavyojua maswala ya kupenda huenda mpaka ndani ya moyo na nafsi na akili na matokeo huonekana kwenye mwili.
Sasa mtu kama huyo kumtoka sio rahisi sana maana mchakato wake ni kuanzia ndani ya nafsi mpaka aje akubali atakua amesumbuka sana na pengine kupoteza vingi wakati akichakata kuondoka kwake moyoni mwake.
Kwa sisi wengine tunaweza kuvumilia kipindi kigumu kama hiko kwa tumaini ya kwamba yatapita tu lakini tutabakiwa na majereha makubwa sana moyoni.
Wengine kwa kweli hawana uwezo wa kuvumilia hali hiyo, wanafanya maamuzi magumu yenye gharama kubwa mpaka ya uhai, na vile umesema ana bunduki, jiadhari sana.
Unaweza ukafanya jambo hilo bila athari kubwa iwapo unatumia busara na akili kubwa na hoja za nguvu.
Kuna dawati la jinsia,kuna viongozi wa dini, kuna wanasheria,kuna watu wa heshima kwako na kwake, na pia nyie wawili mkikaa mkiambina ukweli naamini kabisa mtafika mwafaka ulio bora.
Binafsi nakuombea na kukutakia yote mema,naamini kidogo unapitia pagumu lakini wakati mmoja utafika na utakuwa na heri na furaha na amani.