Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo linaanzia hapa!!Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoish
Nahisi unanishawishi[emoji4] akili yangu kuwa wewe ni mwanamke bora sana1: uko tiyari kuachia nyumba?
2: uko tiyari kuachia gari?
3: uko tiyari kuikosa hiyo kazi?
4;hako ka serengeti boy kana chochote au kamekupendea mali za jamaa?
Kama yote hayo uko tiyari muweke wazi ondoka bila chochote.
Ila nakuhakikishia hako ka serengeti baada ya miezi 2 tu katakuacha maana hutokuwa na chochote.
Kuanzia hapo utakuwa nagundu hata mme wa kukuoa hutompata.
Utaishia kulala na vitoto ambavyo unavizidi umri, na vitakuzalisha vikutekeleze.
Mimi nimekuelewa ila ujinga uloufanya ni kumruhusu akawekeza kwako wakati humpendi.
Dada kuna siku utapauka utakumbuka hii comment. Unakwenda kukosa kila kitu kisa hicho kivulana ulichokipata na wenda hakina kitu labda smartphone na laptop.
Dada duniani huwezi pata vyote, bora ukose upendo lakini unahudumiwa.
Nani kakudanganya hako kavulana katakupa raha kuliko huyo baba?
Ondoka ila jiandae kupauka, nimeona walofanya kama wewe wanatamani kurudisha siku nyuma.
Ukipenda jibu maswali hapo juu.
Hivi wanawake kwanini mnakosa bahati kama ya kunipata musuguaji mimi? luckyline mlete huyo dada ata enjoy life [emoji4]Wanawake nao sometimes wanapitia magumu, kuna rafiki yangu alikuwa na mme wa mtu wameachana juzi kwa mwenyekiti maana police ilishindikana.
Pia kabla ya police nilikuwa nasuluhisha kila siku.
Mme wa mtu alikuwa anamuhudumia hadi sisi tunaona wivu, sema huyu dada alitumia akili hakutaka kukubali kujengewa, sijui gari vyote alikwepa na kizuri mwanaume ndo alikuwa akija kwa dada, tuko fensi moja so hayo yote niliyaona kwa macho yangu.
Mimi nikamuita dada nikamuuliza mbona huyu mwanaume anakudekeza huduma zote anakupa hadi sisi majirani tunaona wivu nini shida, kwa nini unachepuka?
Huyo dada alilia akafunguka,
" mimi nimechoka ndani ya miaka 4 niko kifungoni na huyu baba nateseka mimi, hajawahi nifanyia chochote, hata shuka halijawahi lowa hata kidogo.
Usimuone huo urefu, kalea kitambi kadudu kamebaki kadogo sana, na mimi nilivyomnene kanaishia mapajani, nilikuwa namvumilia kwa sababu ananihudumia ila kwa sasa nimechoka.
Kuna biashara tuliwekeza wote namrudishia mtaji wake ila mimi siwezi tena, ana wivu, ananifata kazini, nikitoka out ananisaka mji mzima tukifika ndani hana anachonifanyia, nimechoka mimi, staki tena mgongo unaniuma , bado kunionea wivu kunipiga na mkanda, staki mimi akapiga ukunga."
Dada alivyoenda police wakasema hawataki kesi za wapenzi, akaenda kwa mwenyekiti wakaita wajumbe, mwanaume akasema hawezi kumwacha kirahisi eti kawekeza
kwake, dada kasema hela yote ya mtaji nitampa ila tuachane nipumue.mwanaume akagoma.
Kwenye huo mgogoro mwanaume alitoa vitisho vya kumuua dada kwa sms akaituma kwa mama dada,so siku hiyo kwa mwenyekiti dada kaonesha hiyo sms. Dada kamwambia mwenyekiti kuwa huyo mwanaume atamuua wagawame walichowekeza mbele ya mwenyekiti.mwanaume kagoma.
hiyo ishu ya kushindwa kufanya kazi kitandani hakuisema kwa mwenyekiti.
Sasa mwenyekiti akaamua kuwa mwanaume aondoke pale maana dada alikuwaga akipanga hapo before.aondoke hapo arudi kwake mpaka baada ya wiki. Wakirudi kila mtu aje na anachodai wakabidhiane kwa mwenyekiti.
Dada kaomba asindikizwe mwanaume atowe vitu vyake, maana na ufunguo mwanaume alizigomea dada akawa analala hotelini. Walipofika ndani akatoa vitu kiduchu nguo zote zikabaki, dada kasema avumilie mpaka huo muda waachane kwa amani.
Dada kamwambia mlinzi asiruhusu kuingia getini, lakini pia mwenyekiti aliandika barua ya kumtaka mwanaume asikanyage hapa mpaka siku walopewa kupata suluhu.
Mwanaume akaondoka, wakaanza jibizana kwenye simu mdada kamwambia alivyonchoka gegedo halifanyi kazi, mwanaume akasala kuwa kapata mabwana wengine, ni kweli dada alikuwa kapata mtu.
Baada ya wiki mwanaume hakurudi kwa mwenyekiti, dada akaandaa mtaji alopewa akapeleka kwa mwenyekiti, wakamsubiri mwanaume hakuja hadi leo.
Dada katoa nguo za mwanaume kaziweka kwenye salufeti ziko hapo coridoni. Ni mwezi sasa mwanaume hajarudi. Tunasikia alienda kwa mganga amroge asiachike.
Nb huyu mwanaume ana familia yake mkewe waliachana anaishi na wanae tu. Mwanaume alitaka amuoe huyu dada akagoma akawa akimpotezea coz alijua hawez ingia nae ndoa.
Za chini chini zinasema mke wa huyu mwanaume aliondoka sababu ya mapungufu ya kitandani ya mwanaume, kwamba siku moja alizidiwa akachepuka alipigwa akaondoka ndani yupo uchi hadi leo hajawahi rudi.
Mwanaume kosa vingine ila sio nguvu za kiume
So mleta mada kuwa makini rudisha kila kitu ishi maisha yako.
Hujitambui Sijui Unaandika NiniUnadhani aliponunua gari, kujengea nyumba kulipa kodi kwamba he did it just for granted? Kwa maelezo yako nakuonea huruma sana hasa kwa hayo maamuzi unayotaka kuchukua kwani kaburi limekaribia kukumeza, unamkumbuka yule mwanamke mwenzio aliyeuawa huko dsm kisa kala vya watu afu mzigo anawapa wengine? UKITAKA KULA LAZIMA ULIWE nakuomba sana hata kama sikujui usilete ujanjajanja kwenye uwekezaji ulofanywa na mtu tena akiwa na akili timamu.
Yaani unaumia alipokwambia umzalie na akati una gari, una kazi, nyumba n.k. kwa taarifa yako huyo jamaa siyo lofa wala siyo buzi nakuomba umvumilie kama alivyojikamua na kukufanyia hayo uliyoyasema mwenyewe vinginevyo hizo mali utaziacha na huyo kiben10 wako hatakuoa ataishia kuhudhuria mazishi.
Kama hujui ukiona mtu una date naye anakujengea nyumba n.k huo ni msumari unajipigilia kwani hatokubali hiyo nyumba aingie mwanaume mwingine.
Mkuu@DeepPond hapo unamuonea dada wa watu kurudisha sawa lakini sio na gharama zingine. Kwani yeye alivyo kua anapanda pale juu gharama yake vipi?Uwezo wa kuvirudisha na kusimama mwnyw unao?
Maana ake Apo itabid urudishe kuanzia Ito kazi, Kodi alizokulipia, posho zote alizokupa, Gari,nyumba na gharama zote alizotoa kwako.
Kwa HARAKA HARAKA Happ sio chini ya mil.100
Vipi uwezo upo?
Au Ongea na uyo barobaro wako uwezo anao?
Ili mchangie hizo cost uondokane na icho kifungo dada [emoji4]
Mkuu @DeepPond hapo unamuonea dada wa watu kurudisha sawa lakini sio na gharama zingine. Kwani yeye alivyo kua anapanda pale juu gharama yake vipi?
Anamnyanyasa sababu anajua hana backup yoyote...Huyo bwana harusi akikutwa ndani ya gari alonunua yule bwana itakuwaje mbona unamtakia mtu kifo?
Mkuu zile zilikuwa zamani za ujinga [emoji4]Mfalme Sulemani alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Mfalme Daudi alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Haya, Ibrahimu ambaye wewe mwenyewe unamuita baba wa Imani alikuwa na wake wangapi? Yeye hakuwa na dini? Au wewe Mungu wako ni bora zaidi ya Mungu wa Ibrahimu, Yacobo na Isaka?
HakikaLakini kwa hayo waliyofanya yalionekana ni machukizo mbele za Mungu maana tumeagizwa kuwa mume wa mke mmoja tu hadi kifo kiwatenganishe. Mtumishi wa Mungu akitenda dhambi haihalalishi hiyo dhambi bali linapaswa kuwa funzo kwetu kuwa unapozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo shetani anavyokuandama zaidi. Hivyo tunapaswa kuendelea kuzitetea imani zetu na tukianguka tutubu na kusimama tena.
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.
Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.
Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.
Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?
Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.
Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.
Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.
Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Sijui kana shida gani na ban siku hizi!!!Ban hua zina mhusu [emoji4][emoji4][emoji23]
Atakua na visa na modsSijui kana shida gani na ban siku hizi!!!
Kwahio alikuwa anastarehe bure [emoji23]Kwani alikua anamuuzia?