Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Nimekuwa na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 3 nahitaji kuachana naye, nimuachaje bila yeye kuweka kinyongo

Hivi wanaume wanajifunza nini kupitia huu uzi ?

Ndio mjue Umalaya ni ubatili mtupu [emoji108][emoji108]

Mnaibiwa bure tu [emoji57][emoji57]
Sasa tunaibiwa nini tena wakati tunagegeda mwa starehe yetu na wanawake walishasema mbususu haiuzwi wala sio bure
 
Lakini kwa hayo waliyofanya yalionekana ni machukizo mbele za Mungu maana tumeagizwa kuwa mume wa mke mmoja tu hadi kifo kiwatenganishe. Mtumishi wa Mungu akitenda dhambi haihalalishi hiyo dhambi bali linapaswa kuwa funzo kwetu kuwa unapozidi kuwa karibu na Mungu ndivyo shetani anavyokuandama zaidi. Hivyo tunapaswa kuendelea kuzitetea imani zetu na tukianguka tutubu na kusimama tena.
Aisee...hindsight is 20/20
 
Big boy hawezi kubali kirahisi rahisi hivyo kwa solution ya kumrudishia vitu vyake, maana jamaa kashawekeza kwa dada hapo kwahiyo kashatune mind ni wake..

Hata wakiachana atamfanyia visasi tu, kinachowatesa watu ni attachment
Big boy😀😀
 
Mungu akatupe hekima
IMG-20220222-WA0025.jpg


Sent from my Moto C using JamiiForums mobile app
 
Kuja haina tatizo ila basi atoe taarifa. Kuna wakati unastukia tu saa sita ya usiku katoka safari badala aende kwa mkewe anakuja kwangu!
Kwako au kwake? Si Analipa kodi yeye ni kwake hapo!
 
Aliyeleta uzi mbona yuko kimya au kashapigwa risasi ya ubongo😃
 
Habari wanajamii forum, ni matumaini yangu kuwa mko salama. Ama la, basi Mungu awafanyie wepesi.

Ndugu zangu nahitaji msaada wa mawazo yenu sana. Ninapitia sijui niseme ni wakati mgumu au ni ujinga wa kujitakia. Niko kwenye mahusiano na mume wa mtu sasa yapata miaka mitatu. Imefikia hatua nimechoka na nahitaji kujing’atua ila nakosa njia nzuri ya kuachana nae. Am not even proud with what i did so if you judge me i’ll understand.

Huyu mtu tangu nafahamiana nae ameyabadilisha sana maisha yangu maana ana mchango mkubwa sana. Alinisaidia kupata kazi nzuri na kuachana na kakazi kangu nilikokuwa nafanya, alinihamisha na kunipangishia sehemu nzuri zaidi. Baadae alininunulia gari nami nikawa natembea nimekaa, pia amenijengea nyumba iliyo kwa jina langu ila kwakuwa ipo nje ya mji nimeipangisha nakula kodi ila bado analipia kodi hapa ninapoishi.

Mahusiano yalipoanza sikufikiria hata yangechukua miezi 6, ila sasa ni miaka mitatu+. Ni mwanaume anayejali sana ila ana wivu balaa. Ni mara kadhaa amekuwa akinitishia kuwa akigundua ninamsaliti atanikata shingo. Sasa huwa najiuliza huyu ni mume wa mtu, anatarajia kweli niwe na yeye tu ili iweje?

Sasa nimechoka jamani, natamani niwe na mpenzi wangu na sio mume wa mtu. Kuna huyu kijana nimeanza nae mahusiano sasa ni miezi 5, kusema kweli nampenda na ninaona kabisa nae ananipenda. Haya ndio aina ya mahusiano niyatakayo. Nimekuwa nikitafuta visingizio kuwa asije kwangu maana sio maadili ila ukweli ni kuwa naogopa mlipa kodi akijua atanitoa roho.

Huyu mume wa mtu nishamtafutia visingizio ili tuachane ila inashindikana. Natamani yeye ndio aanze ili asije kuwa na kinyongo. Ila kuna wakati najipa moyo kuwa nimwambie tu tuachane lakini nikikumbuka aliwahi kunikunja nusura anipige alipokuta msg asizozielewa kwenye simu nahisi kutetemeka. Aliwahi kunionyesha silaha anayomiliki, nilipomuuliza ni ya nini akasema hata mimi nikimletea ujinga ananifyatua. Japo ulikuwa utani ila niliogopa kusema kweli.

Balaa zaidi recently ameanza kung’ang’ania nimzalie. Nimekuwa nikijifanya mimba hazishiki ila kusema kweli natumia dawa zisishike maana siko tayari kuzaa nae. Kwanza nahisi kama suffocation maana ananibana sana. Kwangu anakuja tu muda wowote akijisikia, na ole wangu asinikute nyumbani ni tatizo kubwa. Kila ninachofanya anahitaji apate taarifa kwanza, yaani kama mkewe vile jamani.

Nimejaribu kuelezea haya ili angalau muelewe ni kwanini nahitaji msaada wa mawazo yenu ili nijikwamue kwenye hili shimo nililojichimbia. Nipeni ushauri naachanaje na huyu mwanaume bila kuleta madhara kwangu.
Rudisha mali zake ndio uendelee na huyo unaempenda
 
Aya sasa wacha tukushauri.
Ushauri wangu hapa ni kwamba uhai ni muhimu. Ili uokoe uhai wako rudisha gari rudisha nyumba sema hivyo vyote sivitaki.
Kama unaona unataka chill with the big boys wee endelea tuu kumpa jamaa mbususu basi ule life ila sasa usije ukasaba isha kifo cha huyo kijana mwengine. So achana nae kabisaa na umwambie why. Wewe uishie kuwa na huyo mume wa mtu basi cha muhimu sii anakupa huduma bwana...security that money provides.

Out of topic. Inaelekea mrembo una tako na mbususu tamu mpaka jamaa anajenga nyumba[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
"Tako na Mbususu [emoji1787]" ntakutafuta unifungulie haya mabano maana isijekuwa nimetumia kanuni tofauti
 
Mi ntakupa ushauri ambao ni very risky lakini Una chances kubwa za kukusaidia kuondokana na hili.

Mwambie Una mazungumzo naye ya muhimu so mpange date, kakaeni kwenye sehemu ambayo ina watu wengine msiongelee chumbani.

Mwambie unapata shinikizo la familia pamoja na nafsi yako Kwa ajili ya kuanzisha familia yako kama ilivyo kwake yeye na mkewe. Kwahiyo imekuchukua Muda mrefu Sana kuwaza namna gani ya kutimiza lengo lako Hilo (Sisitiza Hilo ni tamanio lako)

Then mwambie kuwa unampenda Sana lakini Kwa status yake hawezi kukutimizia Hilo tamanio lako, na ili kutimiza tamanio lako huwezi kuendelea na style ya maisha mnayoishi sasa. Sasa kwakuwa amekufanyia mambo mengi Kwa kipindi mlichokuwa pamoja mwambie uko tayari kumrudishia gari aliyokununulia, nyumba na viwanja ili aone hukuwa na Nia ovu Ila situation inakufanya ufanye maamuzi haya (Hapa unamfanya yeye ndio ajione tatizo/kikwazo) then ndio umwambie unataka kuanza maisha mapya na Mungu akikujalia upate mtu ambaye atatimiza ndoto yako ya kuwa na familia.

Sasa hapa ndio kwenye gamble na risk yenyewe. Kwakuwa anakupenda hatakubaliana na wewe atatoa option ya Kwanza kuwa atafanya mpango WA kuachana na mke wake (uongo na hata kama ni kweli never accept it) atatoa options nyingi lakini usikubali zote simama kwenye malengo yako ya kuanzisha familia yako ambayo yeye hawezi kuitimiza.

Kama ni Gentleman hatakubali urudishe hivyo vitu, Ila atasema basi either tuendelee kuwa marafiki Kwa maana kwamba atajua ataweza kuwa anapata mbususu mara moja moja au atasema miendelee mpaka utakapopata mtu (This is tricky atakufuatilia kuliko mwanzo maana atataka kuua mahusiano yako kabla hayajaanza ili aendelee kuwa mwenyewe) na katika mazungumzo never tell him tayari uko kwenye mahusiano itaharibu maana atajua huyo ndio anakupa kiburi.

Accept friendship, accept kuendelea mpaka utakapopata mtu mwingine lakini on your terms. Wewe ndio utaamua lini aje kwako au lini mionane yeye aombe then we uangalie availability yako (Put this clear) then taratibu Anza kumpunguzia umiliki wake kwako ambao ndio unampa kiburi, upunguza utegemezi wako kwake, Anza kupunguza mawasiliano yako na yeye and with time atakubaliana na matokeo.

It's risky but it could pay
 
Mi ntakupa ushauri ambao ni very risky lakini Una chances kubwa za kukusaidia kuondokana na hili.

Mwambie Una mazungumzo naye ya muhimu so mpange date, kakaeni kwenye sehemu ambayo ina watu wengine msiongelee chumbani.

Exactly what i was thinking to do too. Thank you.
 
Hahahaaa! Not yet nafikiria cha kufanya but its like jamaa nae ashashtuka kuwa am not okay.
Nikuulize tu je humpendi huyo jamaa, hisia zimekata kabisa?

Twende kwa haki kabisa sababu zako kutotaka kuendelea nae.

1. Mume wa mtu, nikweli lakini imeathiri vipi mahusiano yenu wawili, alishindwa kuwajibika kwa lipi?, na kama unamwonea huruma mkewe kwanini yeye humuonei huruma kwa uwekezaji wa hali, mali na hisia kwako? Kwa kipindi chote hicho.

2. Anakuja kwako muda anaotaka, 🤔🤔
Jameni kuna mwanamke asiependa kuspend muda mwingi na mwanaume wake, ndio nasikia leo, kitendo cha kuja kwako mara kwa mara na muda wowote ilipaswa iwe advantage kubwa kwenye kuimarisha penzi lenu, lakini kwako ni mateso🤔🤔.

SABABU ZA KUTAKA KUACHANA NA MWENZIO.

Fahamu ya kuwa penzi kwa mwanamke haligawanyiki hata siku moja mwanamke hawezi hudumu na mabwana wawili hajaumbwa na uwezo huo, na hii ndio changamoto kubwa inayokusumbua kwasasa.

Kitendo cha kuanzisha mahusiano mapya automatically unahamisha kilakitu kwa mwanaume mpya, utatengeneza sababu nyingi za kusingizia ooh ni mme wa mtu oohh anakuja kwangu ooh hiki na kile, ila sababu kubwa nakwambia tena ni huyo mwanaume mpya ndio unataka umkabidhi yale unayoyapokonya kwa bwana wako wa awali.

NINI CHA KUFANYA
Nakushauri na kukusihi kaa chini fikiria kwa kina tumia akili hisia ziweke kando, angalia mazuri yote na mabaya yote ya huyo mwanume wako unaetaka kumwacha na ujipime kwelikweli bila kujipendelea je anastahili hicho unachotaka kufanya, na katika hilo fanya tathmini ya kutosha, kuhusu impact ya maamuzi yako.
Ukituliza kichwa unaweza kuta ni mihemko tu ya penzi jipya ila kiuhalisia kuna mengi ya manufaa kwako kabla ya hilo jipya.

Mwisho nikukumbushe kitu.
Kurudisha nyumba, gari na pesa havitasaidia kitu vinginevyo kama umepanga kufanya maamuzi yako kwa kujiaminisha ukirudisha hivyonvitu utakua salama ni kujidanganya.

Hizo nyumba magari na fedha alikua hakuhongi alifanya hivyo kwa mapenzi ya dhati kabisa, ni kama vile unavyomnunulia kitu mama yako, au baba yako zawadi au chochote dhumuni la ununuzi linatangulizwa na upendo kwanza.

Ili urudishe hizo mali sasa inabidi umfanye asikupende kabisa ndio atazipokea vinginevyo fanya maamuzi yako ukijua lolote baya au zuri linaweza kukukumba.

Mwisho.
 
Thread Tele Humu Watu Wanakufa Kisa Mapenzi Nawe Umeanza
Rudisha
Gari Alilokununulia
Nyumba Aliyokujengea
Kodi Anayolipa

Halafu Huyo Unayempenda Mkaanze Upya
Hapo Umenasa Mwenyewe, Huna Namna
Point.Huwezi kuchukua vitu vyote hivyo alafu mtu akuache tu lazima akuue tu
 
Point.Huwezi kuchukua vitu vyote hivyo alafu mtu akuache tu lazima akuue tu
Mimi Nilimwambia Toka mwanzo...!! Atafanyiwa kitu ambacho Hakitaacha alama wapi yupo na wapi alienda... Wadada wanadhani kila mtu wakumchezea na kumuona boyaaa.

Achague Uhai wake na Amani kwa kuacha Mali au Atangaze vita kwa kumgeuka mwana.
 
Nikuulize tu je humpendi huyo jamaa, hisia zimekata kabisa?

Twende kwa haki kabisa sababu zako kutotaka kuendelea nae.
Hakuna Upendo wa kumnunulia gari na nyumba mwanamke alafu kesho akikuacha Ukubali tu ulifanya kwa upendo...!! Na hakuna watu wenye visasi vibaya kama wale ambao upendo ulitangulia kwanza yani Vita yake huwa ni kubwa sana. Usimdanganye mwenzio
 
Back
Top Bottom