Hahahaaa! Not yet nafikiria cha kufanya but its like jamaa nae ashashtuka kuwa am not okay.
Nikuulize tu je humpendi huyo jamaa, hisia zimekata kabisa?
Twende kwa haki kabisa sababu zako kutotaka kuendelea nae.
1. Mume wa mtu, nikweli lakini imeathiri vipi mahusiano yenu wawili, alishindwa kuwajibika kwa lipi?, na kama unamwonea huruma mkewe kwanini yeye humuonei huruma kwa uwekezaji wa hali, mali na hisia kwako? Kwa kipindi chote hicho.
2. Anakuja kwako muda anaotaka, 🤔🤔
Jameni kuna mwanamke asiependa kuspend muda mwingi na mwanaume wake, ndio nasikia leo, kitendo cha kuja kwako mara kwa mara na muda wowote ilipaswa iwe advantage kubwa kwenye kuimarisha penzi lenu, lakini kwako ni mateso🤔🤔.
SABABU ZA KUTAKA KUACHANA NA MWENZIO.
Fahamu ya kuwa penzi kwa mwanamke haligawanyiki hata siku moja mwanamke hawezi hudumu na mabwana wawili hajaumbwa na uwezo huo, na hii ndio changamoto kubwa inayokusumbua kwasasa.
Kitendo cha kuanzisha mahusiano mapya automatically unahamisha kilakitu kwa mwanaume mpya, utatengeneza sababu nyingi za kusingizia ooh ni mme wa mtu oohh anakuja kwangu ooh hiki na kile, ila sababu kubwa nakwambia tena ni huyo mwanaume mpya ndio unataka umkabidhi yale unayoyapokonya kwa bwana wako wa awali.
NINI CHA KUFANYA
Nakushauri na kukusihi kaa chini fikiria kwa kina tumia akili hisia ziweke kando, angalia mazuri yote na mabaya yote ya huyo mwanume wako unaetaka kumwacha na ujipime kwelikweli bila kujipendelea je anastahili hicho unachotaka kufanya, na katika hilo fanya tathmini ya kutosha, kuhusu impact ya maamuzi yako.
Ukituliza kichwa unaweza kuta ni mihemko tu ya penzi jipya ila kiuhalisia kuna mengi ya manufaa kwako kabla ya hilo jipya.
Mwisho nikukumbushe kitu.
Kurudisha nyumba, gari na pesa havitasaidia kitu vinginevyo kama umepanga kufanya maamuzi yako kwa kujiaminisha ukirudisha hivyonvitu utakua salama ni kujidanganya.
Hizo nyumba magari na fedha alikua hakuhongi alifanya hivyo kwa mapenzi ya dhati kabisa, ni kama vile unavyomnunulia kitu mama yako, au baba yako zawadi au chochote dhumuni la ununuzi linatangulizwa na upendo kwanza.
Ili urudishe hizo mali sasa inabidi umfanye asikupende kabisa ndio atazipokea vinginevyo fanya maamuzi yako ukijua lolote baya au zuri linaweza kukukumba.
Mwisho.