Nimekuwa nikikumbwa na usingizi mzito wakati wa vikao na wakati nikiwa katika nyumba za ibada. Shida yangu nini?

Kitambi huwa kinaleta mabadiliko unakua Kama mama mjamzito kasoro kutapika na kichefchef, uzembe uzembe unakua mwingi
Punguza kitambi
 
Habari wadau wa JF.

Kwa miaka takriban minne Sasa, napitia nyakati ngumu. Nikiwa kwenye vikao mbalimbali vya kijamii, kikazi au hata Imani napatwa na usingizi wa ghafula.

Pia niwpo ktk nyumba ya ibada, mawaidha na mahubiri yakiendelea najikuta nimesinzia tena usingizi mzito. Ninapata muda mwingi wa kulala na kazi zangu sio nzito.

Kuna kikao fulani mwaka juzi nilisinzia hadi mwisho nashutuka, kikao kinafungwa.

Je tatizo langu ni nini?

Pole sana, shetani amedhamiria kukulaza kwelikweli

Wanadamu Mungu alitupenda sana, akagawa giza na nuru sababu mchana lazima mwili uwe kazini either kijamii au kiibada lakini usiku miili yetu inapopumzika roho zetu huwa macho zikifanya mawasliano na roho wa Mungu na kama Mungu hatunae basi roho za shetani

Kwa maana hiyo wewe wakati wa kujenga maisha, kufanya maamuzi ya kikazi/kiofisi, na wakati wa kuwasiliana na Mungu wako unakua haupo, unakua umetwaliwa kupitia mwili kulala!

Usiku huwa unafanya nini? Kama unayaona ya usiku kupitia ndoto yatakusaidia kujua kinachokulaza
 
Mzee basi hiyo itakuwa ni Sihr (uchawi)...either umeambatana na shetani au umelishwa . Jaribu sana kumuomba Mungu akuondoshee matatizo hayo lakini pia kama una nafasi tembelea katika maduka ya dawa za asili ulizia dawa inaitwa habbat sawdah ( black seeds) nunua pakiti ya mbegu zake zilizosagwa kisha changanya na asali unywe atleast vijiko vitatu daily, pia nunua na mafuta yake ...uwe unajipaka eneo la paji la uso na pembeni ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu.

Pia unaweza kutafuta vitunguu swaum...vipondeponde kisha kabla ya kulala jipake usoni na kwenye mishipa ya fahamu kichwani. Mungu atakufanyia upesi uweze kuondokana na tatizo hilo.
Mkuu umetoa msaada Kwa wengi. Ninayo unga wa habbat soda nikiletewa toka Zanzibar March 2020 Ila upo tu sikutumia. Je huwa umaharibika? Naweza kuutumia? Ila uko chengachenga hivi. Mafuta yake ninayo ninakunywa asubuhi na jioni mara nyingi Sana. Nimejua sasa nipake usoni kidogo. Shukrani Kwa Elimu.
 
Mzee basi hiyo itakuwa ni Sihr (uchawi)...either umeambatana na shetani au umelishwa . Jaribu sana kumuomba Mungu akuondoshee matatizo hayo lakini pia kama una nafasi tembelea katika maduka ya dawa za asili ulizia dawa inaitwa habbat sawdah ( black seeds) nunua pakiti ya mbegu zake zilizosagwa kisha changanya na asali unywe atleast vijiko vitatu daily, pia nunua na mafuta yake ...uwe unajipaka eneo la paji la uso na pembeni ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu.

Pia unaweza kutafuta vitunguu swaum...vipondeponde kisha kabla ya kulala jipake usoni na kwenye mishipa ya fahamu kichwani. Mungu atakufanyia upesi uweze kuondokana na tatizo hilo.
Amina, Inshallah
 
Pole sana, shetani amedhamiria kukulaza kwelikweli

Wanadamu Mungu alitupenda sana, akagawa giza na nuru sababu mchana lazima mwili uwe kazini either kijamii au kiibada lakini usiku miili yetu inapopumzika roho zetu huwa macho zikifanya mawasliano na roho wa Mungu na kama Mungu hatunae basi roho za shetani

Kwa maana hiyo wewe wakati wa kujenga maisha, kufanya maamuzi ya kikazi/kiofisi, na wakati wa kuwasiliana na Mungu wako unakua haupo, unakua umetwaliwa kupitia mwili kulala!

Usiku huwa unafanya nini? Kama unayaona ya usiku kupitia ndoto yatakusaidia kujua kinachokulaza
Duuuhh, nimeshutuka
 
Jaribu kutumia tiba ya vitunguu swaum na Ndimu kama una sheytwan basi ataondoka kwa uwezo wa Mungu ktika mwili wako.

Nunua kitunguj swaum kimenye punje zake kisha kisage vizuri halafu chukua ndimu kama tatu hivi kamulia then mixture yake utaitumia kujipaka mwili mzima usiku kabla ya kulala. Kama unaweza unaweza kupaka na asubuhi siku ambazo huendi kazini. Kama una matatizo ya kuvamiwa na majini wachafu basi yataondoka kwa uwezo wa Mungu
Nitajitahidi kufanyia kazi ushauri huu, kumbe dawa zipo za kawaida tu.
 
Jaribu Bar kwenye viti virefu pale counter huku totoz zikikatisha karibu, ukilala hapo umerogwa!!
 
Pole sana, huyo shetani yupo kazini usiku atakuwa anakufanyisha kazi bila wewe kujijua kwahiyo mchana ndiyo unakuwa na nafasi yakupumzika, ikatae hiyo hali fanya maombi kabla yakulala fuatilia ndoto unazoota
 
MKUU NYIE NDO HUWA MNAANGUSHA MAGARI MTARONI KWA USINGIZI USIOISHA
 
Jaribu kutumia tiba ya vitunguu swaum na Ndimu kama una sheytwan basi ataondoka kwa uwezo wa Mungu ktika mwili wako.

Nunua kitunguj swaum kimenye punje zake kisha kisage vizuri halafu chukua ndimu kama tatu hivi kamulia then mixture yake utaitumia kujipaka mwili mzima usiku kabla ya kulala. Kama unaweza unaweza kupaka na asubuhi siku ambazo huendi kazini. Kama una matatizo ya kuvamiwa na majini wachafu basi yataondoka kwa uwezo wa Mungu
Hivi SHEYTWAN NA SHYTOWN NI NDUGU???
 
Back
Top Bottom