Nimekwenda DAWASCO Kimara, majibu nimepewa hadi nimemkumbuka mwenda zake

Nimekwenda DAWASCO Kimara, majibu nimepewa hadi nimemkumbuka mwenda zake

Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee, huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.

Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee, may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
Acheni kukaririshwa maneno ya KIJINGA ambayo Mwendazake aliwapandikiza. Huduma kwenye maofisi ya Serikali hazijawahi kubadikika. Ninaandika kwa UHAKIKA kabisa kuwa hata ungekinganisha kipindi cha Mkapa- Kikwette - Magufuli, HAKUNA jipya kwenye Huduma.

Huwezi kuwa na Serikali bila Urasimu. Ni sekta binafsi tu ndiyo Ina Huduma bora, tuwe wakweli

Tofauti ni kwamba Mwendazake alikuwa anapenda masifa ya uwongo
 
Unakumbuka Magufuli !!!

Hakukuuwia nduguyo?
Hakumteka nduguyo?
Hakubomoa nyumba yako ama ya nduguyo?
Hakumfukuza kazi nduguyo kwa husuda?
Hakumpora nduguyo fedha zake?
Hakumweka ndani nduguyo kwa uonevu?
Hakumtukana nduguyo hadharani?

Huyu mtu siyo wa kumkumbuka hata kidogo.
Watu wangapi waliuliwa ndugu zao na Magufuli? Una hakika huyo ndugu aliyeuawa aliuawa kwa mkono wa Magufuli?

Utekaji hapa nchini ulianza lini? Ulimboka, alipofanywa alifanywa na Magufuli?




Hapa napo alifanya Magufuli??


Aliyemteka, kumtoboa jicho na kumg'oa kucha ni Magufuli?

Hawa waliwekwa ndani na Magufuli? Je waliwekwa kwa uonevu? Kutolewa kwao ni kwa kuwa hawana hatia?



Nani aliyefukuzwa kazi ma Magufuli pasipo sababu?
Mtu anayependa upumbavu wa kuwa na wafanyakazi hewa kwenye payroll, unaweza kusema ana akili gani mtu jinsi hiyo?

Nyumba ipi iliyobomolewa na Magufuli kinyume cha sheria?

Wewe umetukana watu wangapi hadharani?

NI upumbavu wa kishetani dio huongoza watu kusahau mema yote na hukumbuka mabaya tu, kujihesabia haki hata anapotendewa haki, kuwalaumu wengine kwa makosa yao, ama ni mtu mjinga asiyeona thamani ya mazuir watu wanayfanya. Ustitupotezee muda .
 
Ungetufahamisha ulikwenda kutaka huduma gani, na ulijibiwa nini ingekuwa vizuri zaidi.

Nitag akijibu! Limekatiwa Maji Halikulipa eti linataka likishalipa libebe mafundi na toyo likaunganishiwe Maji!
 
Hili la nyodo kwenye ofisi za umma awamu hii linakwenda kuwa baya hata kuliko wakati wa Kikwete. Huyu mama by nature hana haiba wala tabia ya ukali.
Anayejua mama anakotupeleka anyooshe mkono tafadhali.
 
Mimi hawajapita kusoma mita na tarehe 26/6 nikaona mwezi unaisha hawajaja nikapigia simu waje wasome mita ili nilipe namehangaika kila siku unawaomba ndio leo wamekuja 30/6
Soma mita mwenyewe wajulishe wakutolee bili na wakupe control number ya kulipia.

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee, huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.

Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua [emoji23][emoji23] yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee, may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
ofisi za umma karibia zote zilikuwa na huduma mbovu.
suala la customer care mbovu limekuwepo tokea enzi za mkapa.
 
Tunawajua Bwashee ndio maana nyinyi ndio mnaongoza kwa chuki na umimi na kubebana bebana na ufisadi na ukabila,endelea kuimba mwamba wenu mzee wa konyagi aliyeshughulikiwa na Sabaya hadi akahama nchi awavushe huku nyinyi mkimpa michango tuu huku ruzuku akiitafuna yeye na ukoo wake,Magufuli yuko ndani ya damu na mioyo ya watanzania milele na milele nyinyi pigeni kelele tu ila musahau kwa nchi mliyoijenga kwa watanzania na ukabila wenu basi uraisi mtausikia kwa wengine tuu.
Kajenge sanamu kwenye kaburi lake!
 
Ungetufahamisha ulikwenda kutaka huduma gani, na ulijibiwa nini ingekuwa vizuri zaidi.
Business as usual haisaidii hata nikisema nilifata huduma gani ila mshukuru hii nchi haturuhusiwi risasi lakini pale nikikuta wanaliwa Simba nasaidia Simba iwale iwamalize
 
Unakumbuka Magufuli !!!

Hakukuuwia nduguyo?
Hakumteka nduguyo?
Hakubomoa nyumba yako ama ya nduguyo?
Hakumfukuza kazi nduguyo kwa husuda?
Hakumpora nduguyo fedha zake?
Hakumweka ndani nduguyo kwa uonevu?
Hakumtukana nduguyo hadharani?

Huyu mtu siyo wa kumkumbuka hata kidogo.
haya mabaya kila mtu anayo yake yamezidiana tu we mwenyewe unayo na UNAYAJUA basi tu acha mazuri yake tuseme narudia "NIMEMKUMBUKA SANA"
 
Sasa wewe umeenda Dawasa ili wakukopeshe pesa ukalipe ada ya wanao jumatatu, afu ulitegemea wakupe majibu yapo?
Kina Edo shida ni majina yenu , hivi mikopo wanatoa Dawasa ? kule tunafata huduma za maji mzee hii bangi unavuta tafuta iliyokauka
 
Niliwahi kumuweka kwenye wakati mgumu mdada mmoja kwenye halmashauri moja baada ya kunipamba kichwani, mpaka mkuu wake alikuja kuomba msamaha huku mdada machozi yakimtoka.
Tupe mbinu uliyotumia mkuu maana na mimi kuna dada mmoja NHIF mbeya hakunitendea haki nilipotaka huduma
 
Haha na hata kama una mwili mdogo unatakiwa uwe na roho kubwa. Unamtamkia maneno mazito hadi anakupa huduma kwa heshima.

Mimi ofisi ya majunior officer kama hiyo naingia casual tu ila ili nipate concentration yake na nimfundishe uoga nikifika hapo huwa naanza kwa kujitambulisha kwa majina yote mawili, alafu namuuliza mtoa huduma jila lake akinitajia naliandika kwenye note book akiwa anaona alafu ndiyo naendelea kumwelezea shida iliyonileta kwenye ofisi yao.

Sasa hapo akili kichwani kwake, afanye kazi au afanye blanda.
kwa biti hilo la kuandika jina lazma awe mpole kidogo,itabidi nikuige ndugu
 
Ofisi za Umma zimeanza kurudi enzi za Kikwete aisee, huduma mbovu majibu mabovu na wanajua huna pa kuwapeleka.

Dawasa Kimara kumbukeni mnafanya huduma jamani mtatuua 😂😂 yaani imefanya nimkumbuke marehemu Magufuli aisee, may he continue rest in heaven sasa namwelewa japo too late.
Mtanyooka tu
 
Unakumbuka Magufuli !!!

Hakukuuwia nduguyo?
Hakumteka nduguyo?
Hakubomoa nyumba yako ama ya nduguyo?
Hakumfukuza kazi nduguyo kwa husuda?
Hakumpora nduguyo fedha zake?
Hakumweka ndani nduguyo kwa uonevu?
Hakumtukana nduguyo hadharani?

Huyu mtu siyo wa kumkumbuka hata kidogo.

Usiwatengenezee watu chuki kwa lazima!! Mi hajafanya hata moja apo
 
Nchi iendeshwe kimfumo siyo mtu mmoja binadamu tunapita mfumo utabaki mpaka mwisho wa dunia, endelea kumkumbuka ila alianzisha utaratibu mbaya wa yeye kuwa kila kitu, mf mawaziri na watendaji kumsifia kutoa hela za miradi wakati ni za watanzania wote

Ni za watanzania sawa!! Mbona hazipiti kwako?
Kazichukue bas


Ye ndo mwenye dhamana
 
Back
Top Bottom