Nimeleft group la WhatsApp la Familia ya mke wangu

Naaomba kuuliza wadau katika kutafakari sababu za familia ya mke wangu kuniunganisha katika group la familia yao sikuona mantiki na hivi leo nimeaamua kuondoka.

Je, nitakuwa nimekosea?
Nibora umeleft maana kifuatacho wataanza kukusema mara una kibamia mara humridhishi mtoto wao [emoji23]
 
Uko sahihi,kuna jamaa yangu mimi hakauki ukweni,kisa kuna vimisosi vidogo vidogo vya hapa na pale,siku moja nikasikia wanasema huyu nae kwa kula,nikajua hapa hakuna kupendwa,sana sana wanakuzoea mwishowe hukawii kusikia baba tunaomba utusaidie katununulie pumba za nguruwe zimeisha...
 
Mimi hata group la familia yetu tu huwa sikai maana usnitch huwa sitaki. Mimi group langu ni moja tu la Liverpool FC mambo ya soka tu.

Wakiniweka group sijui la shule najitoa sijui la familia najitoa sitakagi uduanzi mimi. Sasa sembuse la ukweni.
Njoo kwenye group la Chelsea wewe ..achana na iyo livakuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…