Nimeleft group la WhatsApp la Familia ya mke wangu

Nimeleft group la WhatsApp la Familia ya mke wangu

Mi ndio maana nimezuia kwenye settings kuwekwa kwenye magrupu bila ridhaa yangu, hizo settings zipo for a reason, use it.
Kuna kundi niliwah unganishwa na mteja ambae nilimpa namba baada ya kufanya nae biashara sekunde ya mwanzo tu ziliingia sms km mia na ktk hizo jumbe na picha za utupu nazo zimo ilibid nitoke tu
 
Naaomba kuuliza wadau katika kutafakari sababu za familia ya mke wangu kuniunganisha katika group la familia yao sikuona mantiki na hivi leo nimeaamua kuondoka.

Je, nitakuwa nimekosea?
Ni sahihi, hata usijilaumu kuleft hilo group.

Group la familia ni Baba,mama na watoto.

Shemeji,mjomba, shangazi, bibi,babu na n.k hawana sifa ya kuwa members, wao wanafamilia zao pia.
 
Naaomba kuuliza wadau katika kutafakari sababu za familia ya mke wangu kuniunganisha katika group la familia yao sikuona mantiki na hivi leo nimeaamua kuondoka.

Je, nitakuwa nimekosea?
Ujinga kama huu kawaulize hao ndugu zako, usituletee hapa! Hapa tunajadili issues na siyo huu utumbo wako!
 
Mimi hata group la familia yetu tu huwa sikai maana usnitch huwa sitaki. Mimi group langu ni moja tu la Liverpool FC mambo ya soka tu.

Wakiniweka group sijui la shule najitoa sijui la familia najitoa sitakagi uduanzi mimi. Sasa sembuse la ukweni.
Yaelekea huna mahusiano mazuri na jamii
 
Yaelekea huna mahusiano mazuri na jamii
Mahusiano sio mazoea. Sina shida na mtu isipokuwa sipendi mtu anifuatilie wala sipendi kufuatilia mambo ya mtu. Hata kwenye ngazi ya familia. Napenda kufanya mambo yangu kivyangu vyangu.

Undugu ni lawama.
 
Umeoa ila una utoto mwingi bado nyie ni familia moja learn kufanya socialization na watu and be humble it won't cost you anything
 
Hayo magroup sogozi yana kazi ya michango tu kila wakati kutaja kuwafikia watu kwa karibu na kutishia watu wasochanga kuwa hawatachangiwa iwapo haja ikijitokeza!

Huwa nawauliza hivi;

Kwani kabla ya kuwepo kwa whassap groups mambo yalikuwa hayaendi?
 
Umeoa ila una utoto mwingi bado nyie ni familia moja learn kufanya socialization na watu and be humble it won't cost you anything
Won't cost you wapi? Ukishazoeana na familia ya mkeo ikitokea shida yoyote we ndio wa kwanza kupgwa kizinga.
 
Kuwa na whassap groups nyingi ni mojawapo ya chanzo cha kuleta “ mind attachments” ambayo zikizidi zinaelemea moyo.

We need to live like children with free minds without any attachment.

Hiyo huimarisha afya ya akili na moyo na mifumo mingine ya mwili.

Turejee kuishi kwa asili kwa kupunguza hizo mambo.

Ndiyo wengine wanakosa kuwa na regular sleeping [emoji932]
 
Back
Top Bottom