Nimeletewa Kesi: Mke wangu anatoka kimapenzi na Mume wa Mtu

Unapata wapi muda wa kuja kuomba ushauri humu jukwaani kabla ya kumtafuta kwanza huyo mtoa taarifa, ili upate ukweli wa hizo shutuma zake?
 
Na Wewe ukamuacha?!.. dahh
 
Pole sana mkuu kwa maumivu unayopitia kipindi hiki kigumu. Hongera na endelea kutuliza akili. Usipaniki,acha akili itawale maumivu na hisia ulizokuwa nazo kwa wakati huu. Inawezekana kabisa mkeo sio muaminifu na wewe Kwa sababu upo bize au unakuwa kazini anapata muda kufanya huo uasherati. Na kama hauna tabia ya kujichanganya na watu inakuwa ngumu kupata taarifa za uzinzi wa mkeo. Mtafute kwa siri huyo dada ukae nae sehemu umdadisi kiundani akupe mkanda mzima. Na pengine kama Kuna ushahidi basi akupe Ili ukusaidie kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Though if the case is true.. breaking up is necessary ,vise versa is also is a decision. Considering the options and reasons available. Ni ngumu kuishi na mwanamke mzinzi.

Pole sana mkuu
 
Huenda huyo dada mumewe ni mkorofi ndio maana kakimbilia huko atakuwa ameshindwa kupata ushahid ikiwa watakana atafute ushahid kwanza
kama ni hivyo jamaa awasiliane na dada pasipo wazinzi kustuka, liandaliwe fumanizi
 
Kwakweli ni shida
Kunarafikiyngu Jana wameachana na mkewe mke kasomba vitu vyote vya ndani ndoa Ina miak 2 na ni ya kanisani nimemuonea huruma sana
Kataa Ndoa Wana hoja wakat mwingine
Kwa hiyo wasikilizwee... Haya mwakilishi wa Wakataa Ndoa Una la kuongezeaaa, mpeni maiki jamani 😂
 
Matatizo mengi ya ndoa ni matokeo ya msingi au mwanzo mbovu. Hapo usipokuwa makini hata huyo dada aliyekuletea kesi, ukimuweka karibu utatoka naye.

Atakuwa anasema ukweli. Wanawake anasense kali sana. Ongea na mke wako. Mwambie aache hiyo tabia bila kujali anabisha au la. Ila baada ya kujiridhisha.
Mwambie ukweli akiendelea baada ya katazo hilo, akaolewe na huyo jamaa.

Usizunguke sana.
 
Alikuwa na shida na zamani za ndani bila shaka lengo lake limetimia 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…