Nimelikataa jina walilonipa wazazi wangu

Nimelikataa jina walilonipa wazazi wangu

Mimi Mnafiki ni jina la babu yangu lkn pia ni jina langu. Huyo babu yangu km ilivyokuwa kwa wazee wengi wa Kiafrika hapo zamani baada ya shughuli zao walikuwa wanakutana kwenye vijiwe vyao na kupata kinywaji kama vile pombe,ndio ilikuwa starehe yao wakiwa chini ya mti mkubwa huku wakijadili mbinu za kumfukuza ngozi nyeupe.

Ndugu zake babu kwa mama mwingine ilipofika miaka mwishoni mwa 197+ hivi wakampa pombe yenye sumu akafariki na alifia shambani akiwa analima.

Sasa kizazi cha hawa babu zangu wengine walioshiriki kuhujumu uhai wa ndugu yao kikawa kinatuita sisi wajukuu wa Mnafiki tuliorithi jina la Mnafiki jina la utani linaloashiria mnywaji wa pombe.

Nilipinga sana kuitwa hilo jina la utani hata kabla sijajua kama babu yangu alihujumiwa uhai,yaani nikiwa mdogo kabisa.

Tuliorithi jina la Mnafiki yaani wajukuu zake ni wanne. Kati yao watatu hatuvuti sigara wala hatunywi aina yoyote ya pombe na tuna maisha ijapo siyo ya kifahari lkn ni ya kiwango kizuri.

Mmoja yeye yuko kijijini anabwia pombe uatadhani kalazimishwa,tena kwakujitapa kuwa babu yangu alikuwa anakunywa mpaka pombe zikamuua.
Alipokuja kujua kuwa babu yetu aliuawa kwa sababu ya kumiliki mashamba mengi tayari alishakuwa teja wa pombe.

Tabia ninayoambiwa kuwa ina fanana na ya babu yangu ni ya utafutaji mali,misimamo juu ya kile ninacho kiamini lkn pia na muonekano.

Katu sijawahi kuonja pombe wala sigara ya aina yoyote na hata mtu mwenye mienendo ya namna hiyo huwa ninapunguza mazoea naye kabisa.

Ni UPUUZI WA KUPINDUKIA KUAMINI KUWA TABIA NA JINA VINAHUSIANA.
 
Mwaka 2009 wakati nikiwa form 3 nilienda kanisani na kumwambia baba mchungaji nataka kubadilisha jina hili walilonipa wazazi wangu silitaki.

Eti wamenipa jina la babu yangu mzaa baba, babu mlevi kiwembe balaa kwa madem, alikuwa na utajiri wa ng’ombe 500 mbuzi kibao wote kahonga madem, mifugo wengine alikuwa anawapa wanaume kama fidia pale wanapomfuma na wake zao. Nikasema babu gani ndezi namna hii yaani mimi ndio nirithi jina lake?

Baba mchungaji akaniambia sawa nikachagua jina nilitakalo nikabatizwa. Japo mavyeti yanasoma hilo jina bado napambana kubadilisha japo kuna kimbembe.

Wazazi wapeni watoto wenu majina mazuri.
Huna nidhamu mjukuu wangu.
 
Hata hilo ulilochagua ni la babu wa mtu flan mahali flani tena mwenye mambo mengi kuliko hata huyu babu yako.
 
Wanangu wameyakataa ya kizungu na wanashangaa kumbe baba tuna majina ya nyumbani na wanafurahia kweli kuitwa majina yao ya nyumbani. Walienda kwa babu yao wakaambiwa majina yao.
Mwaka 2009 wakati nikiwa form 3 nilienda kanisani na kumwambia baba mchungaji nataka kubadilisha jina hili walilonipa wazazi wangu silitaki.

Eti wamenipa jina la babu yangu mzaa baba, babu mlevi kiwembe balaa kwa madem, alikuwa na utajiri wa ng’ombe 500 mbuzi kibao wote kahonga madem, mifugo wengine alikuwa anawapa wanaume kama fidia pale wanapomfuma na wake zao. Nikasema babu gani ndezi namna hii yaani mimi ndio nirithi jina lake?

Baba mchungaji akaniambia sawa nikachagua jina nilitakalo nikabatizwa. Japo mavyeti yanasoma hilo jina bado napambana kubadilisha japo kuna kimbembe.

Wazazi wapeni watoto wenu majina mazuri.
 
Inafikirisha Sana .

Mimi nimepewa majina ya babu yangu yote matatu.

Babu yangu alikuwa prominent person na MTU ambaye yupo well financial successful. Na kazi ya mwisho amemalizia Bungeni.

Tuje katika hoja
Babu yangu alikuwa anakunywa bia Ila Mimi sinywi pombe yoyote.

Babu yangu alikuwa Ana wake wawili Ila Mimi sio MTU wa wanawake na naaamini katika falsafa ya mke mmoja na watoto wachache.

Babu yangu alikuwa anapenda anaamini kumiliki PESA Sana na sio nyumba

Mimi naamini kuwa na nyumba nyingi na kumiliki hela inayotembea cash flow.

Babu yangu aliacha hela nyingi Sana bank ili zisaidie watoto wake kusoma

Mimi pia napenda kuweka hela bank ila ikiwa ntakufa zitumike kusaidia watoto wote wanaopitia magumu.

Kuhitimisha jina halina uhusiano na tabia za MTU wala destiny .

Kikubwa kuwa na "The sense of who you are"

Tambua udhaifu wako uhufanyie kazi ili usikulemee.
 
Mzigowapumbu Misulupwete , hili jina alipewa mtu mmoja hivi alitrend sana 2015
 
Mwaka 2009 wakati nikiwa form 3 nilienda kanisani na kumwambia baba mchungaji nataka kubadilisha jina hili walilonipa wazazi wangu silitaki.

Eti wamenipa jina la babu yangu mzaa baba, babu mlevi kiwembe balaa kwa madem, alikuwa na utajiri wa ng’ombe 500 mbuzi kibao wote kahonga madem, mifugo wengine alikuwa anawapa wanaume kama fidia pale wanapomfuma na wake zao. Nikasema babu gani ndezi namna hii yaani mimi ndio nirithi jina lake?

Baba mchungaji akaniambia sawa nikachagua jina nilitakalo nikabatizwa. Japo mavyeti yanasoma hilo jina bado napambana kubadilisha japo kuna kimbembe.

Wazazi wapeni watoto wenu majina mazuri.
Kweli Kabisa
 
Hapa ndiyo Ngozi nyeupe walituweza!

Kwamba ukiitwa Mussa au Muhamad ndiyo mambo yako yatanyooka?!

Bora hata huyo babu yako aliweza kupata hata hao Ng'ombe 500 wewe baada ya kubadili jina sasa hivi una mali kiasi gani?!

Hakuna ujinga kama kuthamini majina ya Wazungu na Warabu!
Majina ya kiafrika hayatoshelezi watu wote thus wengine ukopi nje
 
Mimi jina la kizungu nililopewa na wazazi linanikera sana, i feel comfortable and powerful watu wakiniita kwa jina la ubini wangu.
 
Back
Top Bottom