Mnafiki Wa Kujitegemea
JF-Expert Member
- Dec 30, 2022
- 3,751
- 6,337
Mimi Mnafiki ni jina la babu yangu lkn pia ni jina langu. Huyo babu yangu km ilivyokuwa kwa wazee wengi wa Kiafrika hapo zamani baada ya shughuli zao walikuwa wanakutana kwenye vijiwe vyao na kupata kinywaji kama vile pombe,ndio ilikuwa starehe yao wakiwa chini ya mti mkubwa huku wakijadili mbinu za kumfukuza ngozi nyeupe.
Ndugu zake babu kwa mama mwingine ilipofika miaka mwishoni mwa 197+ hivi wakampa pombe yenye sumu akafariki na alifia shambani akiwa analima.
Sasa kizazi cha hawa babu zangu wengine walioshiriki kuhujumu uhai wa ndugu yao kikawa kinatuita sisi wajukuu wa Mnafiki tuliorithi jina la Mnafiki jina la utani linaloashiria mnywaji wa pombe.
Nilipinga sana kuitwa hilo jina la utani hata kabla sijajua kama babu yangu alihujumiwa uhai,yaani nikiwa mdogo kabisa.
Tuliorithi jina la Mnafiki yaani wajukuu zake ni wanne. Kati yao watatu hatuvuti sigara wala hatunywi aina yoyote ya pombe na tuna maisha ijapo siyo ya kifahari lkn ni ya kiwango kizuri.
Mmoja yeye yuko kijijini anabwia pombe uatadhani kalazimishwa,tena kwakujitapa kuwa babu yangu alikuwa anakunywa mpaka pombe zikamuua.
Alipokuja kujua kuwa babu yetu aliuawa kwa sababu ya kumiliki mashamba mengi tayari alishakuwa teja wa pombe.
Tabia ninayoambiwa kuwa ina fanana na ya babu yangu ni ya utafutaji mali,misimamo juu ya kile ninacho kiamini lkn pia na muonekano.
Katu sijawahi kuonja pombe wala sigara ya aina yoyote na hata mtu mwenye mienendo ya namna hiyo huwa ninapunguza mazoea naye kabisa.
Ni UPUUZI WA KUPINDUKIA KUAMINI KUWA TABIA NA JINA VINAHUSIANA.