Nimelima nyanya heka 1 nimepata faida ya Tsh. Milioni 9 ndani ya miezi minne

Kuna watu nao nilikutana nao,waliniambia nyanya zinalipa sana,mpaka nimehamasika nina mpango mbele ya safar nilime

Ukisikia maoni ya watu huenda ukapata hamasa ya kulima au kukata tamaa,kikubwa ni uhondo wa ngoma uingie ucheze
 
Kilimo kinahitaj rotation for high quality and quantity products sio kukomaa na zao Moja tu otherwise uwe unabadili eneo la kilimo
 
Nakumbuka kule moshi kuna jamaa alikopa akawekeza kwenye kilimo cha maharagi. Mwanzo mvua ilinyesha vizuri mwisho ikakata jumla. Jamaa kuona maharagi yalivyoungua akala kitanzi. Mke wake akabaki na deni la benki.
Ukifa na deni linakufa, acha kuokoteza story vijiweni, unadhani ile bima ya mkopo ya kazi gani?
 
Hujalima kitu Mkuu, acha longolongo za kukaa na ouanza kutunga maneno. Mkulima akiandika katika sentensi zake unajua huyu ni mkulima na kalima kweli
Kwa hiyo atakudanganya ili apate faida gani?
 
Hongera
Kuna motivesheni spika alitujuza kwamba ana mabwawa ya samaki yanampa mamilioni.....tukaamua kufuatilia tukakuta kuna tope na vyura.
 
Mkwe wangu alilima maharage ya njano kapata gunia moja hivi Karibuni amekuwa mkali hataki hata muulizie kilimo alichofanya, hongera mkuu return nzuri
Me nlilima heka 20 nlipata roba nane napenda kulima ila sijarudi tena na shamba nimemkodisha mtu
 
Me nlilima heka 20 nlipata roba nane napenda kulima ila sijarudi tena na shamba nimemkodisha mtu
Pole mkuu, huyu wa kwetu hataki kukiri bado anasema atalima tena
 
Pole mkuu, huyu wa kwetu hataki kukiri bado anasema atalima tena
Rafiki kilimo kikiamua kukutoa kinakutoa uhakika!!
Fikiria gunia la kitunguu watu walizia 640k roba la kg100. Saivi wanauzia 45-50k!! Ona Sasa tofauti iliyopo

Nyanya kunakipindi tunauzia 6k ndoo Lita20 munda mwingine 35k ndio hiyohiyo!! Kama una heka umetunza vzr hapa kupata m20 ni kawaida sana
 
Hongera mkuu na sisi wengine ndo tumeanza mishe mishe hizo japo bado mtaji ni mdogo ila tutafika na amini Hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…