Alipokufa Hayati Rais Dkt. Magufuli na Kuhifadhiwa hapo kwa Siku kama Mbili au Tatu hivi barabara ambayo si tu hutumiwa na Wanajeshi lakini hata Raia ( akina GENTAMYCINE ) ilifungwa huku 'Makomandoo' wakirandaranda japo baadhi yao mida ya Usiku tulikuwa tukipishana nao mno tu katika 'Korido' za Gesti ( Loji ) za Kawe Uswahilini.
Na hivi karibuni tu baada ya kutokea kwa Kifo cha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kwandikwa utaratibu ule ule wa Kufunga njia ( barabara ) hiyo kwa Watu ( Raia ) na hata Wanajeshi ( Wanamedani ) kutokupita kumerejea japo safari hii sijawaona 'Makomandoo' ila ninewaona MP's wengi na kuna Wawili najua kuanzia Saa 1 Usiku nitakutana nao Baa Moja hivi maafufu tukigombea 'Kwichi Kwichi' zilizotapakaa hapo.
Naomba kujua Uhusiano wa Maiti za Viongozi wa Kitaifa ( Kiserikali ) Kuhifadhiwa hapo VIP Mortuary ya Lugalo Hospital ( ndani ya kilipo Chuo chao cha Tiba MCMS ) na Kulindwa sana na mpaka Barabara ambayo hupita Raia na Wanajeshi hulazimika Kufungwa kwa muda.
Wajuvi wa 'Masuala' tupeni tusiyoyajua.