Nimelizwa, nimeumizwa na kufadhaishwa mno na kifo cha kijana huyu

Daah poleni sana. Sijui mwisho wa hiyo vita lini
80% ya binadam wa miaka hii wana roho mbaya na ngumu zaidi ya shetan mwenyewe. Fikiria kumchoma mtu aliekuwa ndan kalala, hajamshikia mtu kisu wala bunduki. Hii inaonesha ni jinsi gan binadam wengi wasivyokuwa na huruma kwa wengine.
 
Daah poleni sana. Sijui mwisho wa hiyo vita lini
Kinachoiponza kongo ni rasilimali zake. Pale kila taifa kubwa linachaka lake la kuchimba madini na rasilimali mbalimbali.
Mfano Marekani wanachaka la dhahiri kupitia mikataba ya serikali na la siri kupitia vikundi kama hivi vya M23, Halikadhalika Wingereza, Ufaransa, Belgium na wengineo.

Solution ni serikali kuwatafutia raia wote wanaoishi maeneo yenye rasilimali na madini maeneo mengine ya mijini kama vile Kinshasa, Lubumbashi nk. Afu hayo maeneo waachie hao wanaochimba wachimbe na kuipatia serikali kiasi chochote watachoona hao wakubwa kinawafaa. Bila hivyo wataendelea kufa miaka kwa miaka.
 
😭😭😭😭 RIP asee!
Siku nikiwakamata hawa rebels nawepelekea moto
Hawa ilitakiwa wakikamatwa linachimbwa shimo kubwa, watu wanajaza kuni, zinawashwa afu wanadumbukizwa humo shimoni wapuuzi hawa.
 
M23 wanasababu za msingi kufanya mashambulizi, wamenyanyasika miaka yote kutoka serikali ya Congo na hata wananchi pia, kiasili M23 inaundwa na watutsi wenye asili ya rwanda ila walijikuta Congo baada ya wazungu kuigawa Afrika, kwahiyo serikali ya Congo haiwakubali Kama Ni wakongo halisi na wanatengwa kuanzia huduma za kijamii Hadi kwenye ajira, Kabila snr aliwatumia kipindi anaingia madarakani kwa ahadi kuwa atawajumuisha kwenye jeshi la serikali ila alipoingia madarakani akawageuka, ndio maana hao waasi wamekua wakibadili majina ila malengo yao Ni yaleyale.
 
Mfano Marekani wanachaka la dhahiri kupitia mikataba ya serikali na la siri kupitia vikundi kama hivi vya M23,
Halafu kuna watu bado wanaisifu Marekani eti imeendelea....wakati imejengwa kwa kumwaga damu za wasio na hatia kama Jems.

Putin pambana na hawa wauaji...usiposhinda wewe atashinda mrithi wako.
Haki ni lazima itasimama, hata kwa kuchelewa.
R.I.P James.
 
Dah pole sana mkuu. Naungana na wewe katika maombolezo haya. MUNGU ampe pumziko la milele yeye familia yake pamoja na msamaria mwema Rama.
 
Mkuu mbona hii historia inaonekana kupishana na zingine zinazodai kwamba watutsi walikimbilia huko miaka ya 60 hadi 70 kukwepa mauaji yaliokuwa yanasababishwa na serikali ya Rwanda iliyokuwa inaongozwa na wahutu.
Kama historia ingekuwa ni hiyo ya mipaka ya wakoloni basi tusingeona watutsi peke yake, bali tungeona na wahutu pia waliokuwa wakiishi maeneo hayo.
Sasa basi inasemekana baada ya kufika huko kama wakimbizi, walipewa haki zote za kikimbizi, baada ya kuzaliana na kufuata taratibu za kiichi ikabidi baadae na wenyewe wawe muongoni mwa makabila ya Congo.
Sasa wakati wa vita vya kumng'oa Mobutu, Kabila baba aliwatumia wanyarwanda original (jeshi la Rwanda) lililokuwa na watutsi wengi enzi hizo na waganda.
Baada ya vita vile ikabidi itokee kutokuelewana kati ya Kabila na viongozi wa hizo nchi nilizotaja kuhusu makubaliano yao. Sasa ndo hapo serikali ya Rwanda ikaamua kuwatumia hao vijana kama ngao ya kile wanachokitaka kutoka Congo, waganda nao wakawa upande wa hao waasi wengine ambao leo wanajifanya wako nchini Congo kupambana nao. Lkn yote hii inaonekana kuna mkono wa mataifa kabwa yapo nyuma yao ambayo yamekuwa yakiwapa hao waasi silaha kupitia hizo nchi nilizosema hapo juu kwa ajili ya masilahi yao.

Hata hivyo waasi hao walitakiwa wapambane na wanajeshi wa serikali ambao wanasilaha, na wale raia ambao wana uhakika kwa namna moja au nyingine kuwa wanatumika na serikali. Ila sio kuvamia sehem na kuuwa kila mnaemkuta hapo hata kama mtu mwenyew hana silaha yoyote au hana kosa lolote.
 
Dah pole sana mkuu. Naungana na wewe katika maombolezo haya. MUNGU ampe pumziko la milele yeye familia yake pamoja na msamaria mwema Rama.
Amiin mkuu, shukran sana kwa dua yako
 
Fikiria mtu unamchoma moto binadam mwenzako ambae hajakufanya chochote na hana silaha yoyote ya kukudhuru.
Tatizo la hizi terrorist groups hazina malengo yanayoonekana, unakuta wapo Mia tatu tu na AK-47 zao wakivuta drugs wanajiona wako milioni kumi, then wanataka waichukue Nchi nzima ya DRC?
 
Tatizo la hizi terrorist groups hazina malengo yanayoonekana, unakuta wapo Mia tatu tu na AK-47 zao wakivuta drugs wanajiona wako milioni kumi, then wanataka waichukue Nchi nzima ya DRC?
Hahaha.. mkuu Katumbasongwe mi nafikiri haya makundi hayana lengo la kuchukua nchi maana uwezo wa kuongoza serikali hawana, lkn pia wanajua wakichukua nchi watatokea waasi wengine kuisumbua serikali yao kam wao wanavyoisumbua serikali ya wenzao.
Hawa jamaa lengo lao kubwa ni kumiliki maeneo yote muhimu yenye rasilimali za nchi kama vile maeneo ya kuchimba madini, gesi, mafuta na yale yanayopatikana sijui mchanga wa kutengeneza vifaa vya sim na mabetri. Hayo ya kuchukua nchi hayana umuhimu wowote kwao, ndio maana hauwezi kusikia wamepigana maeneo mengine mbali na yale ya madini.
 
Apumzike kwa Amani kijana Jems
Halafu bado kuna nchi wanawatetea hao M23 na kununua/kuchukua madini kutoka kwao hakina hizo ni fedha za damu fedha Chafu damu za watu zinalia

Tunashangaa sana nchi za NATO Kugoma kununua mafuta/gas ya Urusi mafuta yale na gesi fedha zake ndio zinatumika kuwalipa wanajeshi wanaoua na kubaka wamama/wadada Ukraine

Tukatae vita,tuiombee nchi yetu tudai haki zetu kwa njia ya amani ila sio vita wanandugu
 
Hayo majitu siku ukifanikiwa kulikamata hata moja wapo Kwanza mnalitafuna 071 ndio mnalichoma kama kiazi wallah
 
Hawa watu wanaangamiza maisha ya maelfu ya watu wasiokuwa na hatia kwa faida zao wenyewe.
 
NATO ndio chanzo cha yote yanayotokea Congo, Nigeria, Libya na kwengineko.
Wao wanawapa waasi silaha na vijihela kidogo vya kula, na waasi wanawapa wababe hao wa dunia madini, mafuta, gesi na rasilimali zingine wanazopata kutoka katika maeneo yao wanayoyateka.
 
Inasikitisha sana, kuna siku niliwahi kusafiri na Mcongo aisee jamaa wanapitia mengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…