Hilo haliwezekani na lisingewezekana.
Congo ilipata uhuru wake huku wazungu wakiwa wameshajigawia maeneo yao ya kuchimba madini, gesi asilia nk.
Ndio maana tangu mwanzo wa uhuru, mpigania uhuru wa nchi hiyo na waziri mkuu wa kwanza mweusi hayati Patrick Lumumba alipotaka kutengeneza udhibiti wa rasilimali hizo aliuwawa kifo cha kutisha, tena aliuliwa na jeshi la nchi yake mwenyew ambayo aliipigania hadi uhuru.
Jeshi hilo lililoongozwa na Mobutu halikutaka kujali au kujua ni jinsi gani Lumumba alikuwa tayari kuweka maisha yake hatarini kwa ajili yao na nchi yao.
Walichofanya ni kumuuwa ili wazungu waendelee kuchota bila bughuza yoyote.
Kabila baba alipoingia nae alitaka kuleta za Lumumba matokeo yake akauwawa kiwepesi wepesi na mlinzi wake mwenyewe.
Toka wakati huo ikaamulika kama mbwai na iwe mbwai, watu waibe na nchi isitawalike maeneo fulani, ili iwe ngumu kuwadhibiti wanaotorosha madini yao.