Nimemchukia mke wangu

Nimemchukia mke wangu

Billion Dolar

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
1,292
Reaction score
2,953
Habarini wanajamvi, kama tittle inavojieleza, sina amani ndani ya ndoa kwa muda mrefu sasa najikuta nina stress hadi afya imeanza kuzorota.

Nipo kwenye ndoa mwaka wa 10 sasa, nilifurahia mapenzi ya mke kwa miaka 2 tu ya kwanza ya ndoa. Wakati namwoa mke wangu alikuja na mtoto ambaye alidai ni wa kwangu nami nikampokea, ila kadri siku zinavyosonga namwona kabisa mtoto huyu sio damu yangu kwani hana anachofanania na mimi tofauti tu na tabia kachukua za kwangu , nisichokula naye hali, si kwa kuniiga bali vinakuja naturaly.

Kingine sina ile parental feeling na huyu mtoto, yaani naweza kumpenda mtoto wa ndugu yangu zaidi kuliko huyu mwanangu. Nimempeleka boarding school yaan hata sifikirii kana nina mtoto huko japo nawajibika kwa kila kitu. Amezaliwa mtoto wa 2 mwaka jana ni binti, huyu wala sina swali anafanana na mimi kama mayai, and ninampenda kiasi hata cha kutoa uhai wangu nikampa, huyu kuna muda nakaa nimemwangalia tuuu hata sijui naangalia kitu gani.

Kingine nilichoanza kupata machungu ni kunyimwa papuchi, hii ilianza mwaka wa 2 wa ndoa nikawa napangiwa weekend tu ndo napewa, ilileta ugomvi sana. Yeye akaenda chuo ambacho ni kama 50km toka tunapoishi kwa makubaliano kuwa kila weekend aje. Matokeo yake akawa anakuja kwa mwezi na baadae akawa anakuja wakifunga. Nikaona isiwe shida nikawa namfuata huko.

Baadae napo ikaonekana ruhusa za kutoka ni shida halafu anatoka na uniform kuingia guest ni tabu tu. Nikaacha kuwa nakwenda, rafiki yangu akanishauri nitafute mchepuko, nikafanya hivo hadi nikamsahau kabisa.

Nimeendelea hivyo kwa maumivu maana sikuzoea kuchepuka, baadae nikawa mzoefu nikaona ni haki yangu kuchepuka hata akinikamata nilikuwa namwambia unaweza kuondoka ama kutafuta mwanaume mwingine akuoe.

Shida nliyonayo sasa ni kuwa natumia hela nyingi sana kuchepuka karibu nusu ya mshahara wangu unaishia kwa wanawake. Sina mshahara mkubwa saaana, si wa chini pia. Huwa naangalia chain ya wanawake niliokwishatembea nao ni wengi kidogo toka nlipooa. Nikiri tu kabla ya kuoa sikuwahi kufanya ngono saaaana. Yeye ni kama alikuwa mwanamke wangu wa 3, hivo sikuwa na experience na wanawake. Hata kumwoa sikuchukua muda wa kumfahamu maana tulikuwa tunaishi mikoa tofauti so tulitongozana kwenye simu tu na tukafikia hatua ya kuoana tukiwa tumekutana mara 2 au 3 hivi. Kwa sasa nikihesabu nilokwisha date nao wanafikia hata 30.

Sasa hivi sina hisia naye hata kidogo toka alipobeba mimba alikataa kushiriki tendo la ndoa, na baada ya kujifungua sijamgusa wala kuomba papuchi na mtoto ana miezi 7nsasa.

Kuna kipindi nafikiria kuoa mke mdogo niwe nao wawili, wasiwasi wangu ni dini nitatengwa hadi na ndugu zangu( hili sio tatizo kubwa sana najua litaisha kadri mda unavyoenda), ila tatizo kubwa sijapata mwanamke sahihi wa kuanzisha naye familia kama mke mdogo. Kila ninaokuwa nao naona sio wife material. Natamani sana kuoa mtoto wa kiislam kutoka Tanga, Arusha, Zanzibar, au Kigoma awe kama mke mdogo.
 
Sina mshahara mkubwa saaana, si wa chini pia.huwa naangalia chain ya wanawake nilokwishatembea nao ni wengi kidogo toka nlipooa
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
yaani umejearibu kuvuta ngozi kwako na kujiweka msafi
ila una matatizo pengine zaidi ya huyo mkeo.
achaneni tu ukaoe mwingine ila jifunze kubadilika wewe kwanza unless utaenda kupachukia na huko utakapokwenda,




ANOTHER SINGLE MOTHER IN TOWN
 
1.wanaume mnapenda kuwa namwanamke aliyejificha tabia..yani kwenu ninyi mwanamke akishaonyesha tabia zake kabla ya ndoa mnampiga chini na kumuona hafai..kumbe ulikuwa una uwezo wa kuangalia mapungufu ya tabia kama yanatekebishika ukamwambia badilika moja mbili tatu na mambo yakaenda,so unaenda ishi na mtu angalau unamfahamu.utasikia nataka kuoa mwanamke mfia dini😄sasa hakuna wanawake wanamambo mengi kama hao(ingawa si wote)hao wakija kuufahamu ulimwengu wa nje ya kufia Dini umekwenda na maji sheikh.
Hakuna binadamu asiye na mapungufu katika hii dunia cha msingi ni kujua na namna ya kuishi na kuchukuliana.upendo na kusameheana vikitawala kati yenu.

2.hakuna haja ya kumchukia malaika wa Mungu(mtoto)bila sababu.kama una wasiwasi juu ya huyo mtoto nenda kimya kimya kacheki DNA ikijulikana si wako hakuna haja ya kuendelea na hiyo mwanamke maana huo uongo wa kukubambikia mtu mtoto umezidi levels zote.hauvumiliki.

3.hizo tabia za mkeo mpaka kufikia hapo..wewe mwanaume ndie uliyeruhusu huo ufala wote.mwanamke ni lazima aijue nafasi yake kama mwanamke sio akupande kichwani.halafu Huyo mwanamke inaonesha ana mwanaume mwingine Chief.
Kingine nyie wanaume pia jitahidini kuwa wabunifu na romantic kwa wake zenu.hata nyie huwa mnajisahau pia.mnaamini kuwa mwanamke ni kumhudumia tu na kumfanya fyoko fyoko kitandani 😏

4.michepuko si suluhisho kabisa aiseh.tafuta muda wa kukaa peke yako sehemu iliyotulia(hapo usihusishe mchepuko kwenye safari yako)Hebu nenda kajitafakari kwa kina kama watoto wako ndio wanaokupa sababu ya kuishi na kufurahia maisha tafadhali tafadhali kuwa na muda nao.usiwapeleke boarding school ili upate muda sahihi wa kufurahi a nao.tafuta fuckmate ruhusu maisha yaendelee.ukiwa siriazi na mahusiano ya nje hakuna hatua kwenye maisha utapiga na hata hayo mahusiano ya nje yanamambo meusi mno..ukubali ukatae mwanaume hautakuwa peke yako kwenye maisha ya nje....

5.pole kwa changamoto unazopitia chief.aliyepewa kucha hana upele,mwenye upele hana kucha.mapenzi ya kindezi sana *****
 
yaani umejearibu kuvuta ngozi kwako na kujiweka msafi
ila una matatizo pengine zaidi ya huyo mkeo.
achaneni tu ukaoe mwingine ila jifunze kubadilika wewe kwanza unless utaenda kupachukia na huko utakapokwenda,




ANOTHER SINGLE MOTHER IN TOWN
Mkuu matatizo ya Jamaa aliyonayo kwa sasa yametokana na mwenendo wa Mkeo hapo awali.
 
Mkuu matatizo ya Jamaa aliyonayo kwa sasa yametokana na mwenendo wa Mkeo hapo awali.
Mkuu hujaona kama jamaa ana matatizo?
kumchukia mtoto sababu pekee ikiwa ni kutokufanana kwa sura?

kukubali kupangiwa siku za kusex unahisi imesababishwa na nini?

kutafuta furaha yake kwa michepuko na kuhonga nusu ya mshahara wake!
 
Karaha za kwenye ndoa.

Piga moyo konde boss ila unewashirikisha wazazi wa pande zote kuhusu tatizo lako.
Hakuna kitu kibaya kama kufanyiwa maamuzi na watu wa nje.ninaamini ndoa ni ya watu wawili tu akiongezeka wa tatu hapo hakuna ndoa bali kutoleana siri tu.

Ukiona ugomvi kidogo unashirikisha wazazi basi ujue akili yako bado haijakomaa kutatua matatizo ya familia.mind you..leo hii ukipeleka ugomvi wa mwenza wako kwenye familia yako hujui ni namna gani wazazi wako watauchukulia pengine huo ugomvi ukazalisha chuki kutoka kwa wazazi wako kwenda kwa mkeo.

Then hao wazazi wako hawaishi na mkeo hawatapata muda wa kujua uliyomtuhumu mkeo ni kweli ama si kweli.so hii moja kwa moja ni chuki unamtengenezea mkeo kwa ndugu zako.

Jifunze kupambana kiume.mimi mwanamke na sipeleki kesi za namna hiyo kwa wazazi wangu Kwanini wewe mwanaume upeleke?futa hayo mawazo..pambana.
 
Fanya yote lakini usilogwe ukaoa mwanamke mwingine. Ina maana hujajifunza kwa huyo ulie nae? Mwanamke ukishamuoa tuu ndio mwisho wa kumfaidi! Wee endelea kuchepuka hivyo hivyo tena una bahati una mke ambae wala hakufatilii.
📌📌
 
Acha uoga na maisha, shida yako unashawishi na hela na kazi yako.Jifunze kuwa swaga aka mistari.Hao ulio nao wakatae anzisha kambi mpya kwa mistari halafu mpe utaratibu hapo utulize kipira.Akizingua unahamia kwingine wapo wengi Sana utakutana na atakayekuelewa
 
"Nikiri tu kabla ya kuoa sikuwahi kufanya ngona saaaana. Yy ni kama alikuwa mwanamke wangu wa 3, hivo sikuwa na experience na wanawaka. Hata kumwoa sikuchukua mda wa kumfahamu maana tulikuwa tunaishi mikoa tofauti so tulitongozana kwenye simu tu na tukafikia hatua ya kuoana tukiwa tumekutana mara 2 au 3 hivi." Tatizo linaanzia hapa mwanamke kampatia kwenye simu hajamchunguza Hana uzoefu kwenye mapenzi kakurupuka kuoa [emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom