Pole mwamba, kuwa kichwa cha familia lazima uwe na akili nyingi sana, niseme tu kuwa wewe unayumba kama kichwa cha familia.
Suala la mtoto si wako limeadhiri sana mtazamo wako kuelekea mkeo, usipo angalia, nyumba itaharibika, utapata maradhi na hata hiyo furaha unayoitafuta huta ipata kamwe, suluhu si kuoa tena, suluhu ni kujenga nyumba yako ulianza kuvuja.
Fanya kama mtu mzima, Kwanza mkubali huyo mtoto mtunze kama mtoto wako, mpe mapenzi yote, usimbague, huwezi kujua huko mbeleni atakusaidiaje, tuna mifano mingi sana hata sisi familia yetu kuna mtoto mmjoa inaonekana si baba yatu, tulipata taarifa kwa watu, lakini inaonekana mzee alipambambana sana hilo lisituadhiri, alitupenda wote kama watoto wake.
Mwisho wa siku huyo mtoto ndiyo yupo karibu na wazazi kuliko sisi wengine, amepata kazi nzuri ana mshahara mzuri, kukiwa na tatizo home yeye ndiyo wa kwanza kufika na kutupa taarifa.
Kifupi kama wahenga walivyosema kitanda hakizai haramu, huyo mtoto si haramu.
Pili, Mawasiliano na mkeo ni muhimu sana, mwendo unakwenda hautawasaidia, watoto wanakuwa mwisho wa siku nyumba itafarakana, jambo la kufanya tenga muda na mkeo, Tafuta mahali patulivu maambie una mazingumzo naye, Mweleze mwendo mnaokwenda nao sio,huko mbele ya safari itakuwa mbaya zaidi,mwambie umekaa umefikiri lazima tubadilike, mwambie unataka ndoa iweje, muishi vipi, wajibu wake no upi na wewe wajibu wako ni nini.
Jaribu kufufua mapenzi yale ya mwanzo, mwambie unachota, kama kunamahali ulimkwaza weka sawa, muanze upya, mweleze tamaa yako ya kutaka kurekebisha.
Kuishi na hawa wakina mama inahitaji akili sana, wakati mwingine unajishusha, lakini pambana kwa kumwambia bila woga, mambo usiyoyapenda anayoyafanya, Kukunyima unyumba ni kosa kubwa sana kwa mwanamke, mwambie hadhari yake.
Ukifanikiwa kufanya haya natumaini ndoa yako ita restore na utakuja kunishukuru hapa.