Habarini wanajamvi, kama tittle inavojieleza, sina amani ndani ya ndoa kwanmda mrefu sasa najikuta nina stress hadi afya imeanza kuzorota.
Nipo kwenye ndoa mwaka wa 10 sasa, nlifurahia mapenzi ya mke kwa miaka 2 tu ya kwanza ya ndoa. Wakati namwoa mke wangu alikuja na mtoto ambaye alidai ni wa kwangu nami nikampokea, ila kadri siku zinavyosonga namwona kabisa mtoto huyu sio dam yangu kwani hana anachofanania na mimi tofauti tu na tabia kachukua za kwangu , nisichokula naye hali, si kwa kuniiga bali vinakuja natulary. Kingine sina ile parental feeling na huyu mtoto, yaan naweza kumpenda mtoto wa ndugu yangu zaidi kuliko huyu mwanangu, nimempeleka boarding school yaan hata sifikirii kana nina mtoto huko japo nawajibika kwa kila kitu, Amezaliwa mtoto wa 2 mwaka jana ni binti, huyu wala hina swali anafanana na mimi kama mayai, and ninampenda kiasi hata cha kutoa uhai wangu nikampa, huyu kunamda nakaa nimemwangalia tuuu hata sijui naangalia kitu gani.
Kingine nlichoanza kupata machungu ni kunyimwa papuchi, hii ilianza mwaka wa 2 wa ndoa nikawa napangiwa weekend tu ndo napewa, ilileta ugomvi sana, yy akaenda chuo ambacho ninkama 50km toka tunapoishi kwa makubaliano kuwa kila weekend aje, matokeo yake akawa anakuja kwa mwezi na baadae akawa anakuja wakifunga. Nikaona isiwe shida nikawa namfuata huko. Baadae napo ikaonekana ruhusa za kutoka ni shida afu anatoka na uniform kuingia gest ni tabu tu.
Nikaacha kuwa nakwenda, rafiki yanfu akanishauri nitafute mchepuko, nikafanya hivo hadi nikamsahau kabisa.
Nimeendelea hivo kwa maumivu maana sikuzoea kuchepua, baadae nikawa mzoefu nikaona ni haki yangu kuchepuka hata akinikamata nlikuwa namwambia unaweza kuondoka ama kutafuta mwanaume mwingine akuoe.
Shida nliyonayo sasa ni kuwa natumia hela nyingi sana kuchepuka karibu nusu ya mshahara wangu unaishia kwa wanawake. Sina mshahara mkubwa saaana, si wa chini pia.huwa naangalia chain ya wanawake nilokwishatembea nao ni wengi kidogo toka nlipooa. Nikiri tu kabla ya kuoa sikuwahi kufanya ngona saaaana. Yy ni kama alikuwa mwanamke wangu wa 3, hivo sikuwa na experience na wanawaka. Hata kumwoa sikuchukua mda wa kumfahamu maana tulikuwa tunaishi mikoa tofauti so tulitongozana kwenye simu tu na tukafikia hatua ya kuoana tukiwa tumekutana mara 2 au 3 hivi. Kwa ss nikihesabu nilokwisha date nao wanafikia hata 30
Sasa hivi sina hisia naye hata kidogo toka alipobeba mima alikataa kushiriki tendo la ndoa, na baada ya kujifungu sijamgusa wala kuomba papuchi na mtoto ana miezi 7sasa.
Kuna kipindi nafikiria kuoa mke mdogo niwe nao wawili, wasiwasi wangu ni dini nitatengwa hadi na ndugu zangu( hili sio tatizo kubwa sana najua litaisha kadri mda unavyoenda), ila tatizo kubwa sijapata mwanamke sahihi wa kuanzisha naye fakilia kama mke mdogo. Kila ninaokuwa nao maona sio wife material. Natamani sana kuoa mtoto wa kiislam kutoka tanga, arusha, zanzibar, au kigoma awe km mke mdogo.