Nimemiss kupendwa....

Nimemiss kupendwa....

Ushawahi kujisikia hisia za hivi?unakua kwenye relation ila muda mwingine unajihisi upweke unatamani ukakae mahali upigwe upepo, kuna muda unajisikia moyo umejaa mapenzi hadi yanamwagikia unatamani umuoneshe mtu ila ndio utaonekana mfilipino tu kama sio muhindi....hizi hisia zimekua zinajirudia sana kwangu, nahitaji kuwa updated teh sijui kuwa updated sijui kujiupdate aahh hivo hivo.

Nimemiss sana kupendwa, kuoneshwa mapenzi kwa vitendo, asubuhi style ya kuamshwa iwe kushikwa shikwa nashtuka ooh nakutana na vipi baby mambo, achana na hizi style ya sahivi nakurupuka natupa kule shuka baada ya kupigwa pigwa mgongoni mama nanii amka ukampe mtoto uji, namiss kupigiwa simu kusemeshwa vitu vizuri vizuri, kukutana na text nzuri "unafanya nini njoo nipo huku desh desh garden" ukiachana na sms za mama nanii andaa msosi nakuja sijala, mama nanii hivi uliangalia luku units zimebaki ngapi, nmemiss kupokea kiparcel ndani kuna viatu, gauni nk...nmemiss zile siku nikiwa off mood nawekwa kati ya miguu naulizwa nini mbaya mamaa jamani sahivi nini off mood hata hiyo mood ipige shoti buyuuu hahaha (baba niokoeeee), namiss kuwa huru I miss mambo mengi mnoo.

leo nimevurugwa hadi basi, mnifariji tu, alamsik.

Upigwe upepo sehemu gani sasa!

Hebu dadavua kidogo, na huo upepo ni upepo gani maana kuna pepo nying zikiwemo za kumpampu
 
Kwanza acha kufuatilia hiyo tamthilia..

Pili ,kumisi kupendwa ninkumiss kujipenda..

Ukijipenda sana hata upendo wa watu wengine kwako Ni bonus kwako,hisia hizo zinakuja mkiacha kujipenda na mkitoka vitambi au kupoteza miili yenu ya zamani manakuwa mnahisi km huna tena attention vile
 
Ushawahi kujisikia hisia za hivi?unakua kwenye relation ila muda mwingine unajihisi upweke unatamani ukakae mahali upigwe upepo, kuna muda unajisikia moyo umejaa mapenzi hadi yanamwagikia unatamani umuoneshe mtu ila ndio utaonekana mfilipino tu kama sio muhindi....hizi hisia zimekua zinajirudia sana kwangu, nahitaji kuwa updated teh sijui kuwa updated sijui kujiupdate aahh hivo hivo.

Nimemiss sana kupendwa, kuoneshwa mapenzi kwa vitendo, asubuhi style ya kuamshwa iwe kushikwa shikwa nashtuka ooh nakutana na vipi baby mambo, achana na hizi style ya sahivi nakurupuka natupa kule shuka baada ya kupigwa pigwa mgongoni mama nanii amka ukampe mtoto uji, namiss kupigiwa simu kusemeshwa vitu vizuri vizuri, kukutana na text nzuri "unafanya nini njoo nipo huku desh desh garden" ukiachana na sms za mama nanii andaa msosi nakuja sijala, mama nanii hivi uliangalia luku units zimebaki ngapi, nmemiss kupokea kiparcel ndani kuna viatu, gauni nk...nmemiss zile siku nikiwa off mood nawekwa kati ya miguu naulizwa nini mbaya mamaa jamani sahivi nini off mood hata hiyo mood ipige shoti buyuuu hahaha (baba niokoeeee), namiss kuwa huru I miss mambo mengi mnoo.

leo nimevurugwa hadi basi, mnifariji tu, alamsik.
Kwani wahenga na nyie huwa mnamiss mambo ya ujana?
 
Sasa wewe kuambiwa uangalie units za luku zimebaki ngapi unaona shida?

Can u imagine ungekuwa baba ndo mkeo anakupigia baba nanii huku umeme umetukatikia halafu huko uliko hata nauli ya kurudi nyumbani huna umekaa mahali unakuna kichwa?

Ukiona kwenu nyie wanawake kunafuka moshi kwetu sisi wanaume panateketea.
 
Back
Top Bottom