Nimemiss kupendwa....

Nimemiss kupendwa....

Ushawahi kujisikia hisia za hivi? Unakua kwenye relation ila muda mwingine unajihisi upweke unatamani ukakae mahali upigwe upepo, kuna muda unajisikia moyo umejaa mapenzi hadi yanamwagikia unatamani umuoneshe mtu ila ndio utaonekana mfilipino tu kama sio muhindi....hizi hisia zimekua zinajirudia sana kwangu, nahitaji kuwa updated teh sijui kuwa updated sijui kujiupdate aahh hivo hivo.
Nitakuja PM tupeleke hii kitu kwenye anga za juu.
 
woii wengine hata hatuaminiwi sanasana tnakutana na maswali 'kulikoni leo? kile kidem chako kimekutoa nduki? polee......
poa nosweti unamtafta kipoozeo unaandika maneno yote mazuri anakujibu 😂😂😂😂😂😂nimesafiri ncheki weekend najua umemis nini my love
unaamua kulala moyo unapiga ka biti la azonto unamskilizia wife ata akuguse unaskia anakoroma poa no swet unawaza anijui huyu asbuh unamtegea bafuni unampa 1 for the road then kilamtu anapita hivi...

nmemisi kupendwa,kudeka,kupetiwapetiwa na sio kuambiwa "nakuchukia hadi nakupenda!!
 
Me nimemiss mapenzi flani hivi ya kila muda mnapeanaaa,yani kila mtu yupo available kwa mwenzake
 
Mademu wa kibongo mapenzi haya hamuyawezi. Mshazoea kufokewa tokea kwa wazazi wenu.

Tukiwaletea haya mahaba ya kizungu mnaanza kuwa wapuuzi na ujinga ujinga unaanzia hapo mwishowe ndoa inafeli.

So tubakie humo humo kwenye kuvumiliana. Wewe kama unajiskia hivyo jikaze tu ni matokeo ya kutazama tamthiria za kikorea. Ukiacha then utaishi uhalisia.
 
Hii ni mood yangu kwa sasa, mpka jana jioni nikawa natizama simu yake chat zetu yan mambo magum ndo yanajdiliwa umeme, ada, nenda manispaa, nirushie namba ya flani, ongea nae unichek yan mambo ya beb beb hakuna
 
Muda umeshatamatika mama ,usishindane nao maana ukishindana nao utachepuka
 
Sasa wewe kuambiwa uangalie units za luku zimebaki ngapi unaona shida?

Can u imagine ungekuwa baba ndo mkeo anakupigia baba nanii huku umeme umetukatikia halafu huko uliko hata nauli ya kurudi nyumbani huna umekaa mahali unakuna kichwa?

Ukiona kwenu nyie wanawake kunafuka moshi kwetu sisi wanaume panateketea.
Naam
 
Back
Top Bottom