Nimemkamata binti wa dukani kaniibia kwa mbinu aliyoniibia mwanzo, Kazi hana mshahara umekwenda

Nimemkamata binti wa dukani kaniibia kwa mbinu aliyoniibia mwanzo, Kazi hana mshahara umekwenda

Inauma sana kuibiwa kuskie tu kwa mtu mm niliibiwa dukani kwangu kizembe sana japo naamin kabisa na dada aliyekuwa dukani nae aliiba baada ya tukio..haiwezekani mwizi ajue sehemu zote zinapotunzwa pesa achukue zilizofichwa sehemu zaidi ya 3 ..alivoona nimeanza process za kufatilia polisi na akaona kabisa mwizi anaenda kipatikana akajiuzulu kazi..mdada/mkaka akizoea kazi kwa kukaa mda mrefu mahali anajua mbinu zote za kuiba na once utakapogundua njia hizo(kwa kuhisi au ni kweli anaiba)ww bos ukianza kuformulate mbinu za kumdhibit hakai ataondoka tu maana mirija ya udokozi ushaidhibit boss, anaona hapana maslahi tena ..either atadai kuongezewa mashahara hata kama anaona kabisa mapato yako chini atajijali yeye au ataresign kwa kutafuta sababu za kipuuzi..MWIZI NI MWIZI TU HAIJALISHI JINSI YAKE tena bora ww unaevidence kabisa ALIPE si wa kumuonea huruma kabisa
 
Punguza kuangalia movie za kihindi
 
Ukinitapeli mara ya kwanza aibu iwe kwako unaenifanyia hayo mabaya, lakini ukinipiga mara ya pili kwa style ile ile nikiwa na utimamu wa kujua kinachoweza kutokea basi aibu iwe kwangu, Niliapa sitoweza kuangukia kwenye mtego wa jaribio la kwanza kwa mara ya pili.

Niliweka binti wa kazi alinitandika shilingi laki 3 mwezi mwanzoni na nikadhani may be ni kosa langu but hadi kuamua kufikia hayo maamuzi ni baada ya kuona kwamba labda pengine ni uzembe wangu wa kutokutunza kumbukumbu vizuri, pia alilia sana machozi kwahio nikasema acha nifunike kombe mwanaharamu apite maisha yaendelee.

Lakini sikuwa mjinga kusamehe na kusahau, nilishaweka countereasures za kutoangukia mtego maana hilo tukio nilikuwa nalikumbuka halikupotea kichwani.

Siku ya jumatatu baada ya kumlipa mshahra wake nashangaa tena leo nimekula short ya laki na 30 flani , HELL NOOO !!!

Yeye hakujua kwamba nilianza kutunza rekodi za withdrawals kila siku kisirisiri na niliweka camera ya siri ofisini so nikavua koti kuanza nifatilie, kila kitu kilichorekodiwa pindi nikiwa sipo mpaka duka linapofungwa.

Nimemdaka live bila chenga kaingia ofisini na kuchomoa pesa, Binti ni mafia aisee!! kumbe na yeye ana funguo spare sehemu nayotunza pesa, kweli alikuwa kajipanga.

Nilivuta pumzi na kuongea kwa sauti, FOOL ME ONCE SHAME ON YOU, FOOL ME TWICE SHAME ON ME !! yeye akasema bosi kuna nini, nikarudia tena FOOL ME ONCE SHAME ON YOU, FOOL ME TWICE SHAME ON ME !! akawa kimya akinishangaa nikamwita kwa majina yake matatu mara mbili na kumwambia HOW DARE YOU , hasira nilizozipata nusu nimzabue mikofi ziga zaga ya bila mpangilio ovyo ovyo, Ila nikashusha pumzi nikamwambia hebu njoo uone huku kwenye screen, alipojiona akaanza kupiga magoti ohh boss nisamehe, nilikuwa na shida ya pesa, mshahara haukutosha, n.k. nilibaki kumshangaa nikamuuliza mshahara wako tuliokubaliana nimewahi kukuchelewa, akabaki hana jibu maana sijawahi kumcheleweshea, nikamuuliza tena day allowance yako nimewahi kukunyima, akasema hapana maana ni kweli kila siku akifika tu ana haki ya kuchukua elf 3.

Nilichofanya ni kumwambia naenda kumwambia polisi na ndugu zake, Network yake ni kama ilikata, nikamwambia option pekee aliyonayo anirudishie laki 3 aliyonipiga mwanzo na laki 1 aliyonipiga jana na kisha aondoke.

Uzuri nilikuwa napajua kwao na alinisihi sana nisioneshe video kwa watu wake naowajua, kijana toka asubuhi saa tatu ndio karudi muda huu na pesa laki 3 na elf 70 inaelekea kahenya sana huko,

Shughuli ndipo imeishia hapo kazi hakuna tena na nimemfanyia kwa huruma sana maana evidence clealy inaonyesha anavyoiba
Mifunguo ya akiba uli ichukuwa mwenyewe?.

Kwanini umlipishe laki 3 wakati umemkamata kaiba laki 1 na 30?.
 
Nimemwambia aitafuta sana aipate kabla ya j3 anitumie kwa mpesa wala sitaki akanyage hata ofisini

Waweza kuhisi unamkomoa kwa s*x akaifinya cd ikapasuka akakupa magonjwa ama mimba kabisa kibao kikugeukie
Sasa Boss vipi kuhusu hiyo kazi? cv natuma wapi?
 
Wote humu kwa nafasi zenu huwa mnaiba, Wizi nchi hii imekuwa kitu cha kawaida sana.
 
Naomba kujua hivi gharama kubwa ya cctv ni kwnye kununua na kutengeneza mfumo au kuuendesha?
Na nikiasi gani?

Naomba jibu la kueleweka..
Na mimi nimechoka.
 
jamaa nimemshaur akawa mkal kama gabachor mla pilipili za upupu camon
nkamuambia basi anipe namba nimtibu tatzo la udokozi nimpe na kazi kakaza namba
Mm Kuna namna alinijibu kwa kebehi ndo maana nlimuuliza hvo
 
Naomba kujua hivi gharama kubwa ya cctv ni kwnye kununua na kutengeneza mfumo au kuuendesha?
Na nikiasi gani?

Naomba jibu la kueleweka..
Na mimi nimechoka.
Vifaa ila anaza na camera chache then ongeza.
Mi nilianza na camera 3 sasa hivi Nina 8.
Kamera mpaka njiani wanakopita raia..!!!

#YNWA
 
Yani sijui nyie huo ujasiri,wa kumuachia mtu biashara mnautoa wapi,Mimi nilimwachia rafiki yangu tu ambae anajiweza vizuri anakazj yake serikalini,anasehem yakukaa na hapo alikuwa likizo nilimuomba wiki tu,lkn nilivyorudi sikuamini
Anafika hatua anauza Bei ya chini,ili auze haraka nilianza upya mbona,nikasema kuliko kuajiri mtu Bora nimepe wife au nifunge kabisa nikafanye Mambo mengine
 
Back
Top Bottom