Brother ushauri wangu kwako ni wewe kuendelea na MAISHA YAKO.
I might sound rude but its the truth, huyo ni Ex wako na ipo sababu kwanini ni Ex wako you owe her nothing.
Maamuzi aliyoamua kuyachukua juu ya maisha yake regardless namna wewe na yeye mliviochana sio sababu tosha ya kumfanya yeye kua huyo mtu aliamua kua sasa.
Tatizo letu sisi binadamu hua tunatafuta mtu wa kumlaumu juu ya vitu vinavyotokea maishani mwetu hasa mambo yanapoenda kombo lakini ukweli ni kwamba "we are responsible for our own actions". Wewe kua sababu ya yeye kua alivyo ni kwa sababu aliruhusu wewe kua sababu ya yeye kua alivyo sasa na mengine ambayo mimi na wewe hatuyafahamu but ntakuuliza yafwatayo, JE?
-Ni watu wangapi wamekumbwa na vitendo vya udhalilishaji (ubakaji, usengenyaji n.k) lakini bado wakaweza kusimama imara na kujenga maisha yao katika njia stahiki?
-Watoto wangapi wametelekezwa na wazazi wao wakiwa na akili zao za utambuzi wakiachwa kua yatima lakini wakakua na kua na maisha yenye mafanikio?
-Wasichana wangapi walipoteza usichana wao kwa watu ambao waliwapenda na kufikiri hao ndo wangekua wenza wao kwa maisha yao yote lakini bado mambo yakaenda sivyo na bado wakainuka na kuendelea na maisha yao na yakawa mazuri?
Brother hapo wewe huyu dada hakudai wala humdai chochote, pengine its the feeling of GUILT uliyokua nayo ndani yako kua yupo vile ukiwa wewe ndo sababu mmoja wapo ( ambacho amekisema yeye na sio wewe) ya yeye kua pale alipo sasa lakini ukweli ni HAPANA.
Mimi binafsi ngekua katika position yako ngeendelea na maisha yangu tu kiroho safi kumbuka alishafanya maamuzi hayo kitambo sana bila uhusika wako kwake, fanya maisha mkuu. Unless kama una huruma kiasi hicho cha kutaka kumsaidia kitu ambacho si kibaya ila tarajia chochote kutoka kwake, narudia tena tarajia chochote kutoka kwake.