Nimemleta Anko kutoka kijijini, wife kaanza vijitabia vya ubinafsi

Nimemleta Anko kutoka kijijini, wife kaanza vijitabia vya ubinafsi

Sasa hebu mpe ushauri faza. Huyo dogo kwa mtazamo wako unataka aandaliwe chakula na nani? Aingie jikoni akajiandalie? Au amuandalie yeye mwenyewe faza haus?? Toa maoni mkuu
Yeah faza hausi ajifunge kanga ampikie amuandalie 😂😂😂😂
 
Kumheshimu mke wako siyo kumuogopa. Wewe unaona sàwa kumuamuru mkeo awe ànanwandalia mtoto wa dada yako chakula? Mtoto wa dada yako ni mtoto wako, sàsa badala àtumwe jikoni akachukue chai sasa nae awe kidume kama baba mwenye nyumba aandaliwe chakula mezani?
Keshapikiwa inatosha.
Na hapo ndio maneno huanza, mtoto anafanyishwa kazi usiku na mchana...kazi kweli kweli..
 
Wanawake tuna gubu sana Kwa ndugu wa wanaume ila nasema ukwel Kuna wanaume wanaroho nzur na wapole ndugu upande wa mwanamke wakija wanawahudumia vema bila manyanyaso mnapepo yenu ila sisi wanawake ni kinyume na ni asilimia kubwa
 
Ila kumuandalia chakula dogo ni dharau ilo nakataa ila mengine mkeo ana makosa ila kumuandalia chakula no
 
Wanawake ni wabinafsi sana, nilipiga marufuku ndugu zake kwangu baada ya wakwangu kufanyiwa figisu na akanuna akaondoka sikupiga simu wala kumtafuata. Karudi na Baba na Mama yake kuomba radhi, nimewarudisha natafakari mpango wa kuishi na wanangu tu.
My maaan. Mwamba huyu hapa..
 
Hiyo sio adabu mkeo kumtengea kijana mdogo msosi

Lakini pia kwa tabia za baadhi ya wa mama mtu pekee anaeweza kuishi hapo kwa amani ni mtu kutoka upande wa kwao
 
Kwahyo ndugu braza Huyu uncle wako alishikishwa maandazi na akamiminiwa Chai mkononi
 
Na hapo ndio maneno huanza, mtoto anafanyishwa kazi usiku na mchana...kazi kweli kweli..
Kàma maneno yataanza sababu kaambiwa chai iko tayari achukue anywe, hapo hakuna familia tena.
 
View attachment 3196698
Kwa Nia njema tu,
Unapendaga majibizano yasiyo na tija 🤔 mstari wa mwisho unasemaje? Hapo au upewe MIWANI hujaona nucta then hapo baada ya nucta na neno CHAKULA.

Salamaleko.
Huoni hata aibu kujiaibisha? Soma paragraph ya pili,
Chanzo kikuu cha kuletwa hii mada ni dogo kula maandazi mkononi,

"Nikamwambia hakikisha unamwandalia chakula" umeelewa hapo? Kwani maandazi sio chakula? Hiyo chakula imetajwa in general ila issue ni maandazi,

Kama unaona unipe Miwani,basi mimi naona wewe ndio unatakiwa upewe akili ya uelewa.
 
Yaani unamwambia mkeo amuandalie huyo dogo chakula na isijirudie tena? Pole yake
Kwa hiyo umeona Hilo ndio kosa pekee kwenye huu Uzi sio?

Pole yake huyo aliyekua(kama hata mume)

Maana inaoneka una roho mbaya sana kama mke WA huyu jamaa ndio umeshindwa kuona tabia za ubinafsi na roho mbaya za huyo mwanamke kwenye huu Uzi
 
Si umuandalie wewe hayo maandazi, kweli kupatwa kwa faza hausi huku 😹😹😹
 
Faza house Kuna utaratibu nimeona Umetaka ufanyike na Mke wako kwa huyo ndugu yako. Nikuulize kwanza wewe ni mzinza? 🤔
Wazinza hata kama mwanaume ni mdogo ataheshimiwa na mwanamke kama ni mkubwa wake
 
Hiyo ya shati haiko sawa ila hiyo ya chakula sijaona kosa la shemeji yetu. Kwangu msosi unawekwa dinning kila mtu anaenda kujichotea. Wasukuma ndio huwa tunawapa tahadhari wasipakue sana
 
Back
Top Bottom