Nimempa ujauzito binti nisiyempenda....nifanye nini?

Preta preta preta, uliwahi kuona mtoto akilelewa na mama wa kambo au baba wa kambo? kosa ni la mleta mada kupiga kavukavu sasa asije akapelekea mateso kwa mtoto siku za baadae..
Crashwise, siasa zinamsumbua sana mtoto Preta siku hizi, yaani amekuwa na siasa kali mno.....
 
Last edited by a moderator:
.....BTW.....nimekumiss sana......
Preta nipo tu, tatizo nazurura sana kuikimbiza faranga. bahati mbaya franga imeota matairi basi tabu tupu.

Ndimi Bazazi!
 
Last edited by a moderator:
Crashwise, siasa zinamsumbua sana mtoto Preta siku hizi, yaani amekuwa na siasa kali mno.....

ayaaaa......sio hivyo ndugu yangu....kwanza habari za Mbabane.....?...unakuja lini huku Yaeda......kale kanyanyi nilichokwambia nitakuchinjia kamekuwa.......
 
ayaaaa......sio hivyo ndugu yangu....kwanza habari za Mbabane.....?...unakuja lini huku Yaeda......kale kanyanyi nilichokwambia nitakuchinjia kamekuwa.......



Orait Preta....mswati amebakiza sherehe moja tu baas mi huyo nakwea pipa kama wasira hadi yaeda chini....stay tuned...lol
 
Last edited by a moderator:
inabidi tuanze kuwapa somo wadada..umekaaa na mwanamke kwa miaka mitano hujatoa posa an tena umempa mimba then unasema humpendi? wtf?
 
Kwanza utambue kuwa zinaa ni uchafu na ni dhambi sana kwa muumba.

Pili, kina dada zetu hii ni tabia yao, huambiana kuwa akifanikiwa kukupatia mimba yako tu umekwisha utake usitake utamuoa. so na wewe kwa "upuuzi" na tamaa zako ukaigia mkenge.
 
Kwa umri huo wa miaka 34 ulioutaja, wewe ni senior bachelor. Kama mpaka umri huo hujampata unayedai wewe kumpenda, basi nakuonea huruma sana. Nakushauri acha kuchezea maisha kwani utakuja kujuta baadae. Muombe Mungu wako akuongoze kwenye kumpenda huyo aliye na mimba yako na mfunge ndoa haraka sana. Naamini kama ni mwenye tabia nzuri upendo utakuwepo tu. Kila la heri kaka.
 
Smile chapa lapa, jipe raha mwenyewe. Ukiifungia sana itaota uvundo. Jilipue upate ka baby kako mwenyewe hayo malovee ya walioshindikana makwao sijui kama utayapata. Siku hizi nyumbaa ndogo ni fashio, tuombe mungu ipite!
 
sifikirii kumtelekeza mtoto lakini pia sifikirii kumuoa mama yake mbaya zaidi sihitaji kuwa na watoto wa mama tofauti.
husaidiki na huna msaada bwana wewe usituchanganye hapa jibu unali kichwani lazima umuoe huyo mwanamke ,kama huo ndio msimamo wako,NA NINAKUAMBIA HIVI HUTAKAA UPATE MWANAMKE ATAKAYE KUPENDA KAMA HUYO DADA NA UTAISHIA KUPATA PASUA KICHWA TU MAANA HELA ZIMESHAKUCHANGANYA UNAMWONA HAFAI SASA ,YOU WILL REMEMBER MY WORDS ONE DAY,,,,,,,MWANAMKE ALIYEKUPENDA KWA DHATI UTAISH NAYE KWENYE SHIDA NARAHA ,ILA MWANAMKE ULIYEMPENDA WEWE KWA DHAT UTAISHI NAYE KWENYE RAHA TU SHIDA ATAKUPASUA UBONGO WOTE, SO CHUKUA HIZO AKILI ZAKO CHANGANYA NA ZA MBAYUWAYU .
 
lakini jamaa hampendi....raha ya ndoa kupendana.....mapenzi ya kuoneana huruma hayafai....
kaka mwenye thread.....nakushauri fuata moyo wako.....
Preta NA KWANINI AMPOTEZEE MUDA 5YRS SIO KITU KIDOGO ANATEGEMEA HUYO DADA AKAOLEWE NA NANI NA MTOTO WAKE AU TU SABABU YYE HANA ANAPOONYESHA AMEZAA AU WANATUTESA SANA HAYA MAJITU Preta
 
Sasa kaka huyo mwanamke unamuonea huruma mpaka umempa mimba mbona huruma yako imepitiliza?
na kama kweli ulikua hutaki kuzaa na huyo binti matangazo ya kutumia kinga yamebandikwa mpaka kwenye nguzo za umeme
mbali ya mabango ya barabarani au hukuona? ebu kua mwanamme na kubali kuvuna ulichopanda.baba hakatai mtoto
sababu hujui yupi atakusaidia japo kukupa bakora ukiwa mzee.
 
Mkuu,
Sheria za nchi hazikukatazi kufunga naye ndoa (bomani ikibidi) akiwa ktk hali hiyo.

Kuna mambo mawili matatu ya kuzingatia hapo.
  • Ni mapenzi ya dhati au huruma zako ndo zimekuweka kwenye mahusiano kwa 5 years na huyo binti?
  • Uhusiano wenu mlitarajia uwafikishe wapi?
    Kwao na huyo binti wanafahamu hali aliyonayo na kuwa wewe ndo mhusika??
ukiipata majibu unaweza kupata wazo jipya.
Ila nikupe angalizo dogo tu kwamba ukizembea tu, soon utakuwa na mtoto wa nje ya ndoa
 
Why ulifanya ngono na mtu ambaye humpendi au alikubaka? Pia hukujua kuwa pekupeku yaweza kuleta mimba isiyotarajiwa?? Umempotezea muda huyo dada, nani atakuja kumuoa huyo akiwa na mtoto wako?
 
miaka 5 mwanamke hujampenda ulikuwa unasubiri nn kama c mtoto??? huyo ndo mke wako hujataka kutambua mapema tu....u entered relationship aiming not to luv try the othr side for a change
 
sifikirii kumtelekeza mtoto lakini pia sifikirii kumuoa mama yake mbaya zaidi sihitaji kuwa na watoto wa mama tofauti.

Kweli umechanganyikiwa ndugu manaake maelezo yako yanagongana haswa. Nitaanza kwa maswal mawili ya haraka haraka: Hivi kama humpendi mwanamke kama unavyotaka kutuaminisha - Unaweza kweli kuwa na mahusiano naye yanayohusisha ngono zembe kwa takriban miaka mitano????? Umesema mlikuwa na mahusiano ya mapenzi mkiwa chuoni - swali ni je unaweza kuwa na mahusiano ya mapenzi na mwanamke ambaye humpendi????

Kwa kuwa kwa maelezo yako unapenda product ya huyo binti lakini hutaki kumuoa na wala hutaki product ya binti mwingine mimi ninashauri utangaze uchumba usiokuwa rasmi na wala usiokuwa na kikomo. Baada ya hapo umhamishe aje kwako ili muishi pamoja na muendelee kulea huyo mtoto na ikiwezekana mtengeneze na watoto wengine.

Ukiulizwa ni nani kwako wewe jibu ama ni mchumba wako au mama wa watoto wako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umekwepa kumuoa, na utakuwa umekwepa kuwa na watoto wa mama tofauti na huyo bibiye atakuwa anaendelea kukupenda kwa karibu. Hii inaitwa WIN-WIN SITUATION.

Ila kabla ya yote fanya DNA Test kujiridhisha kuwa kweli ni mtoto wako wa halali usije ukauziwa mbuzi kwenye gunia.
 
Huo ni ushahidi namba moja kama ulikula mzigo bila kinga. Pambaf!!!!
 
Why ulifanya ngono na mtu ambaye humpendi au alikubaka? Pia hukujua kuwa pekupeku yaweza kuleta mimba isiyotarajiwa?? Umempotezea muda huyo dada, nani atakuja kumuoa huyo akiwa na mtoto wako?
Siyo mimba tuu. hata stds na hiv pia
 
Humpendi analazimisha nini! Atimuke zake huko atafute wanaume wengine. Wako wanaume kibao aje kukuganda hapo nini. Kama ningekuwa ni mie asingejaribu hata kutia guu lake mlangoni kwangu. Kosa ulilofanya ni kumtia mimba. Mtoto chukua ukalee.

 
Humpendi analazimisha nini! Atimuke zake huko atafute wanaume wengine. Wako wanaume kibao aje kukuganda hapo nini. Kama ningekuwa ni mie asingejaribu hata kutia guu lake mlangoni kwangu. Kosa ulilofanya ni kumtia mimba. Mtoto chukua ukalee.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…