Nimempa ujauzito mke wa mtu

Nimempa ujauzito mke wa mtu

Usiogope hata kidogo huna kosa, hujabaka wala kumrubuni kimapenzi ni yeye kakufuata kwa hiari yake. Wewe endelea na mishemishe zako usijipe stress hata kidogo huna kosa kisheria. Nimeshuhudia kesi kama hii jamaa aliachiwa huru. Ila walipimwa DNA test confirm kama mtoto ni wake baada ya confirmation jamaa aliambiwa na mahakama kua ahudumie mtoto.

Nyie ndo mnawaharibu watu kama hao kwa kuwapa ushauri mbaya. Kisheria, ndivyo ilivyo, lakini kuna sababu gani ya kujijengea chuki kama hzio, je, huyo aliyetendewa hivyo, hana ndugu na je, kama ni wewe umefanyiwa hivyo, mtu anajisifu kuwa huwezi kumfanya kitu ungejisikiaje, maana wakati mwingine jivue koti lako, vaa la mtendewa uone imekaaje. Hizo ni chuki za maisha, imeshuhudiwa hasa watu wenye uwezo wa kiefdha wakifanyiwa mambo makubwa ikiwepo kudhuriwa kwa sabau ya vitu kama hivyo.
 
Mkuu kuna Mzinzi fulani alishawahi kuzini na mke watu hivyo hivyo, sasa tatizo huyo mwenye mke alikuwa jambazi na kwa muda huo alikuwa jeala, alipotoka jela huyo mzinzi hatujui alikufaje maana aliokotwa asubuhi akiwa ameuawa, na kuhusu mtoto yaani kilichotokea huwezi amini, baadaye alipolipotea na hajawahi kuonekana mpaka leo kwa hiyo, unapoenda na mke wa mtu na kuonyesha madharau, elewa unakoelekea sio kuzuri, kuna koo zenye ushiriano sana, hata kama uko mjini mtu atatumwa kutoka kijijini kuja kutoa onyo kwa watu wenye tabia kama zako, chezea binadamu wewe !!

Kweli kabisa, hapo ni hatari sana.
Inabidi huyu Granta afanye juu-chini akaombe msamaha kwa mwenye mke, na apatane naye.
Maana huwezi kujua mwenye mke anaweza kufanya nini, na atafanya hiyo kitu lini.
Unaweza ukajiona shujaa kwa miaka mingi tu, na ukaanza kusahau, ghafla hata hutajua 'umepigwa' kutokea wapi.
 
Last edited by a moderator:
Nyie ndo mnawaharibu watu kama hao kwa kuwapa ushauri mbaya. Kisheria, ndivyo ilivyo, lakini kuna sababu gani ya kujijengea chuki kama hzio, je, huyo aliyetendewa hivyo, hana ndugu na je, kama ni wewe umefanyiwa hivyo, mtu anajisifu kuwa huwezi kumfanya kitu ungejisikiaje, maana wakati mwingine jivue koti lako, vaa la mtendewa uone imekaaje. Hizo ni chuki za maisha, imeshuhudiwa hasa watu wenye uwezo wa kiefdha wakifanyiwa mambo makubwa ikiwepo kudhuriwa kwa sabau ya vitu kama hivyo.

Soma maelezo yake amefanya kwa kutokujua kama ni mke wa mtu,mara ngapi tunakutana na wadada wazuri barabarani na tunaexchnge contact then mahusiano yanaanza kama hajadeclare kua anamtu how could you know na yy anakuambia sina mtu. Pia msichana ndio kamfuata jamaa. Ambacho mdau granta anachokosea ni kujitapa kua hawezi kumfanya lolote mke wa mtu ni sumu hata kama mumewe hana nguvu
 
Sijakuelewa vizuri....umepiga mimba ya mke wa mtu? Kama ni hivyo mbona fasta tu unatakiwa ufunguliwe mashtaka!!....Yaani umemdhuru mtu maungo yake. Lakini kama kwenye maelezo yako tatizo ni lugha yaani labda unamaana nyingine, mfano kumtunga mimba mke wa mtu.... hapo jiandae kushtakiwa kwa kosa la kuzini na mke wa mtu na kumtunga mimba. Hayo ya kisheria lakini huyo mumewe atakachokufanyia sidhani kama utapenda tukielewe....jipange kidume.

Mkuu asante kwa maelezo yako mazuri, sikufanya jambo hili nikiwa najua yule ni mke wa MTU, mwanamke mwenyewe ndiye aliyenifool kwa kutoniambia ukweli kama ashaolewa...! Sikufikiri kama kuna siku nitafanya kitendo cha kijinga namna hii
 
Mkuu, hebu chukua japo dakika 1 kama ile inayotumika kumkumbuka marehemu kabla ya kuanza shughuli ya Kitaifa au kijamii. Fikiria kama huyo uliyemfanyia hivyo ingekuwa ni mkeo au mdogo wako kafanyiwa hivyo, halafu jamaa aliyefanya hivyo anajitapa kwenye mitandao, kwanza kimaadili, unapata wapi akili ya kutembea na mke wa mtu, kumpa mimba na kuja kujitapa kwenye mitandao badala ya kuhakikisha kuwa inakuwa siri yenu wawili, na je, umesahau kuwa hakuna magonjwa ? Zamani hizo zilikuwa sifa kweli, lakini siku hizi watu wakisikia unajisifia kuwa umpiga mimba mwanamke asiye mke wako wanashtuka, kwa sanabu kama umpatia mimba, ina maana hukutumia kinga na kama hukutumia kinga kuna iwezekana wa kuambukizwa UKIMWI au hata homa ya ini ambayo hata ARV haina. Aidha, ukumbuke kuwa watu wengine wana visasi vya ajabu, unaweza mfanyia kitendo kama hicho akatafuta watu wakakufanyia kitu mbaya kama vile kuku...f.ra, kukupiga, kukuchomea ndani ya nyumba, yaani wewe acha tu chezea maisha ya watu, halafu onyesha dharau kwa kujitapa kwenye mitandao utakufa siku sio zako. Kama ni mimi nauza uwanja wangu wa Bunju, halafu pesa yote inaishia kwako tuone, utaf..rwa halafu picha zinasambazwa mtaani kwa kama hutahama; Takr care !!

Nitaenda kupima magonjwa yote ya zinaa mwezi huu, najutia sana kitendo hiki cha kijinga na aibu, ningelijua mapema ni mke wa mtu nisingefanya uiinga huu
 
Mkuu kuna Mzinzi fulani alishawahi kuzini na mke watu hivyo hivyo, sasa tatizo huyo mwenye mke alikuwa jambazi na kwa muda huo alikuwa jeala, alipotoka jela huyo mzinzi hatujui alikufaje maana aliokotwa asubuhi akiwa ameuawa, na kuhusu mtoto yaani kilichotokea huwezi amini, baadaye alipolipotea na hajawahi kuonekana mpaka leo kwa hiyo, unapoenda na mke wa mtu na kuonyesha madharau, elewa unakoelekea sio kuzuri, kuna koo zenye ushiriano sana, hata kama uko mjini mtu atatumwa kutoka kijijini kuja kutoa onyo kwa watu wenye tabia kama zako, chezea binadamu wewe !!

Asante kwa mchango wako, naomba kwa Mungu wangu hayo mambo yasinitokee coz sikufanya nikiwa najua kuwa ni mke wa MTU
 
Soma maelezo yake amefanya kwa kutokujua kama ni mke wa mtu,mara ngapi tunakutana na wadada wazuri barabarani na tunaexchnge contact then mahusiano yanaanza kama hajadeclare kua anamtu how could you know na yy anakuambia sina mtu. Pia msichana ndio kamfuata jamaa. Ambacho mdau granta anachokosea ni kujitapa kua hawezi kumfanya lolote mke wa mtu ni sumu hata kama mumewe hana nguvu

Mkuu, sio kama najitapa LA. Sijui nifanyeje mambo haya yaweze kuisha kwa amani, najua inauma sana kut.o....wa mke
 
Soma maelezo yake amefanya kwa kutokujua kama ni mke wa mtu,mara ngapi tunakutana na wadada wazuri barabarani na tunaexchnge contact then mahusiano yanaanza kama hajadeclare kua anamtu how could you know na yy anakuambia sina mtu. Pia msichana ndio kamfuata jamaa. Ambacho mdau granta anachokosea ni kujitapa kua hawezi kumfanya lolote mke wa mtu ni sumu hata kama mumewe hana nguvu

Mkuu Domo Zege, nimesoma maelezo yake na kushirikisha ubongo wangu katika kuyachambua na kuona huyu Granta ni mtu wa namna gani, haingii akilini mtu umefanya kosa ambalo hukujua kama ni kosa, halafu badala ya kulijutia, unakuja juu kuwa huwezi kufanywa chochote, ndio maana nikasema, sheria ikishindwa kutoa haki wananchi huchukua sheria mkononi, na kuna baadhi ya wadau hapo juu ukiwemo wewe, wasemshauri kuwa hana kosa kisherie. Nakuunga mkno kuwa kuna makosa kama hayo yanafanywa na watu, lakini ukishagundua, unasikitika, unaachana na hiyo kitu na sio kujitapa, unajitapa nini ilihali wewe ni mavumbi ? Ni wangapi wenye nguvu zaidi yako wamekuwepo na kuitikisa dunia lakini leo hawapo !!! Aidha, fikiria hayo yalitendwa kwa mkeo, mdogo, Dada au shemeji yako, then ukutane na bandiko linalojitapa kama hilo, Tafakari, chukua hatua. Ni aina gani hiyo ya jamii ambayo haiheshimu haki za wengine.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom