Nimempiga mtoto wa mdogo wangu, ndugu wananilaumu lakini Mama ananiunga mkono

Ila Hawa watoto malezi yetu yanawaharibu Mie kuna sehemu nilienda mtoto miaka 4-5 yule acha anitemee mate daaah nilikafinya kakapiga yowe sema kalikuwa na mwenzie mamake alipo uliza yule mtoto akajibu amemtemea mate mgeni

Ila nilitamani nikae nako masaa 2 ma 3 nakafinya maana dharau za kutemewa mate sio powa
 
Mungu akubariki kwa kusimama kama baba
 
Kama hii ni kweli basi ulifanya vyema. Hawa wazazi wa sasa wanatuletea hekaya za korea kwa watoto afu wanaita mapenzi kwa watoto .....sisi hatukulelewa hivyo na tumekuwa hivi , waache kujitia ufedhuli wasiokuwa nao
 
Sasa unalalamika nini, nenda kamshitaki polisi ili afungwe kwa kuvunja vitu vyako na kukuchafulia nyumba.
 
Wa kiume au wa kike
 
Hongera zako mkuu kwa kumpa malezi bora,inaonekana dogo alikuwa amepinda Kweli kweli
 
Daahhh!!anaanzaje kunitemea mate aseehh!!!hayo maujinga yamepitiliza sasa!!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Hongera zako mkuu kwa kumpa malezi bora,inaonekana dogo alikuwa amepinda Kweli kweli

Mtoto alipinda aisee. Siku moja huwezi kuamini washkaji wamekuja kunitembelea, ile tumekaa tunapiga stori eti dogo kaanza kuwatoa kwenye kochi ili acheze.

Nilivyojaribu kumzuia nyumba ikalipuka kwa fujo za dogo. Kwa kweli huyu mwanangu wa kufikia aliharibikiwa.

Mama alimuogopa mtoto, asingeweza kwenda naye popote kwa kuogoga aibu mbele za watu. Nilichokifanya ni kujiwekea mpango kazi hatua kwa hatua, nikampa mama maelekezo. Nilivyomaliza kuweka nidhamu, nikaanza sasa kumpa mama silaha.

Yaani dogo asinisikilize tu ila mama yake pia, napo nikafanikiwa maana niliona kuna uwezekano dogo akaniheshimu ila akampuuzia mama yake na watu wengine.

Hapa nilimpa mama masharti magumu, hata nisipokuwepo dogo akileta fyongo lazima nifahamishwe, na ikiwezekana napigiwa simu dogo akisikia. Alivyoona amebanwa kila kona, alisalimu amri.

Sasa hivi nataka sasa kuingia hatua ya kujenga mahusiano ya kirafiki jambo ambalo sikutaka kufanya mwanzoni baada ya kugundua alichukulia kama mimi ni rika yake vile so ilibidi niwe mgumu, mipaka ilibidi iwepo ili kusimika nidhamu.

Nakuhakikishia, siyo kazi rahisi aisee, imenichukua karibia miaka miwili kumnyoosha dogo.

Sasa hivi mama yake anafurahi na ananitunuku vizuri hasa.
 
Nimependa ulivyo simama km baba yake saafi sana na utalipwa fungu lako
Tulee watoto wa watu km wa kwetu na tusiwanyanyase maana wakiharibikiwa wanaharibu na wa kwetu

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Napenda mno mwanangu awe hivi, kitu usichopenda uzungumze mara moja tu basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…