TANZIA Nimempoteza baba yangu mzazi

TANZIA Nimempoteza baba yangu mzazi

Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo alikuwa kila kitu kwangu[emoji22]

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Pole bro & familia
 
Pole sana. Baba huwa furaha yake ni mtoto wake afanikiwe na kuwa na mafanikio kumzidi yeye. Popote ulipo atakuona na mzuka wake utakuwapo pembeni yako ukifurahia kila dakika ingawa hauta muona kwa macho na kimwili ila kiroho yupo pembeni yako.
 
Pole sana kwa msiba wa mzee, I feel your pain bro, I passed through the same experience way back in 2010. Siku ya ufunguzi wa kombe la dunia South Africa, tena wakati game inaendelea nikapigiwa simu kuwa mzee amefariki, nililia sana. Sitaisahau ile siku, ila sasa huu ni mwaka wa 14 maisha yanaendelea kama kawaida Mungu ni mwema. Raha ya milele uwape enhee bwana na mwanga wa milele uwaangazie marehemu wote wapumzike kwa amani.
 
Mkuu usiumie sana. Mshukuru Mungu kwa kila jambo. Kifo chake chaweza fungua milango ya fursa iliyofungwa katika maisha maisha yako.
 
Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo alikuwa kila kitu kwangu[emoji22]

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Pole sana kijana, pole sana familia...
Mzee ameumaliza mwendo, acha apumzike kwa Amani...

Na kwa Neema na Baraka za Mungu maisha mengine lazima yaendelee, usivunjike moyo, ndio hali ya dunia usisikitike sana...
 
Daah Pole sana Mkuu,Mungu awafanyie wepesi familia yetu kwenye kipindi hiki kigumu...
 
Pole sana ndugu. I can't Imagine the miseries you're into. Mungu akutie nguvu... Mungu amrehemu mja wake
 
Nimempoteza baba yangu mzazi

Sijui hata nisemeje

Baba ndo alikuwa kila kitu kwangu[emoji22]

Roho inaniuma baba kafa kanipambania mwanae nisome leo baba kafa ikiwa hata hajala mkono wangu nikiwa still napambana kupata kazi

Nimebaki yatima mimi[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Pole sana mkuu,mtumaini Mwenyezi Mungu
 
Mi mzee alifariki nikiwa bado mdogo, nahisi kuna ABC fulani angenipa zingekua useful 😭😭, wenye BABA tafadhali tumieni muda mlionao kuwauliza maswali, kufurahi nao maana kuna nyakati zitafika unatamani hata baba ngekuwepo uende umkumbatie ulie, umueleze shida zako lakini ndo hayupo muda huo

Pumzika kwa amani mzee E.J M.....
 
Back
Top Bottom