Mtoto wa kike anapozaliwa anakuwa na mayai kama milioni moja unusu hivi, yanaanza kuharibika kila siku kabla hata haja vunja ungo.
Anapofikia umri wa kupata hedhi ya kwanza, teyari zaidi ya 70% ya mayai yanakuwa yameshaharibika. Kumbuka mayai huwa yanatoka manne hata matano kwa mkupuo, halafu moja kubwa ndiyo linapevuka, yaliyobaki yanaharibika (yanamezwa mwilini).
Mwanamke anapofikia miaka kama 22-24, anakuwa na mayai chini ya laki moja. Kimbembe kinakuja anapofika 30, hapo kuna mabadiliko mengi sana yanaanza kutokea, ikiwemo homoni za estrogen kupungua na kusababisha mayai yanayochepuka kupungua kutoka manne hadi moja. Hivyo kupelekea ongezeko kubwa la yai linalopevuka kuwa na matatizo ya kinasaba kadri umri unavyoenda (mayai ndiyo seli zenye umri mkubwa kuliko zote kwa mwanamke, zinatengenezwa siku chache tuu baada ya mimba kutungwa.
Tukija kwenye sababu za kijamii, si watoto wote wanaopenda kubaki shule, wengine ni bora tuu waolewe wakifika 16 kuliko wabaki mitaani na kuzaa na wanaume wengi, na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani.