Nimemsikiliza kwa umakini Ester Bulaya kisha John Heche, wanasikitisha sana na wanahitaji huruma

Sijasoma,naweza kunusa ulichoandika,Umeandika uharo
 
Hii khabar imekaa kipashkuna kwel
 
We gasho siku nyingine usije kuhalisha tena mbere za watu koma
 
Tangu lini kupinga bajeti kumekuwa ni kupinga maendeleo? Bajeti ni matumizi ya fedha zinazokusanywa kutoka kwa wakazi wote waliomo Tanzania bila kujali uanachama wa chama na misaada ambayo tunapewa kama nchi na sio chama. Kupinga hakumuondelei haki ya kufaidika na makusanyo hayo na kupigana ili waliomchagua wanafaidika kutokana na mapato ya taifa lao. Bajeti sio ya chama, bali ni ya serikali ambayo wajibu wake ni kuwahudumia wakazi wote wa nchi yetu bila kujali itikadi yao au chama chao. Ni wajibu wa wawabunge kuhoji mapendekezo ya bajeti kama wanaona yana kasoro. Ni haki yao vile vile kufaidika na mapato yote ya serikali.

Amandla...
 
Hats hujui unachoandika nenda shule kwanza
 

Vipi Dr. Slaa ambaye naye alikuwa mstari wa mbele akiongoza kashkash dhidi ya serikali ya JK, unamchukuliaje? Yawezekana alidanganywa na Mbowe?
 
Sawa je jimboni kwake kawafanyia mambo gani baada ya kupinga kila kitu miaka 5

Hili neno “kupinga tu / kila kitu” ni kuwalaghai wasio na uelewa wa kupambanua masuala. Elezeni ukweli wa hoja za wapinzani. Km mtu akisema ununuzi wa ndege haukuwa sahihi mnakimbilia kupiga kelele eti amepinga kununua ndege au kufufua ATCL. “Halafu kapanda ndege yetu”. Utter rubbish!

Ongea na wataalamu wa mashirika ya ndege au jamaa wa Boeing na Bombardier watakuambia mshangao walio nao jinsi hizo ndege zilivyonunuliwa - eti kwa cash money! It never happens in a serious business!

Bajeti isipozingatia vigezo makini ni jukumu la upinzani kuonyesha kasoro, kuleta bajeti mbadala na kutounga mkono bajeti isiyokidhi vigezo. Ni vile wananchi wengi hawana uwezo wa kuelewa undani wa mpangilio wa bajeti, wazee wa mapambio mnawadaka kwa kauli za “kupinga bajeti ili miradi isitekelezwe”!

Ukichukulia jinsi wananchi wengi pamoja na praise & worship choir mnavyoamini kuwa Rais ndiye mwenye pesa zote na anazitoa kwa miradi akiombwa kwa unyenyekevu, hapo ndipo ujinga unapofikia kiwango cha SGR. Hata mjadala wa maana kuhusu uchumi hauwezekani. Tuendelee kuwa watazamaji.
 
sasa kwa hoja hiyo kwa nini wabunge wanatoa ahadi wakati hawawezi kujenga chochote na je si tungechagua vichaa kwani yeyote anaweza kuikumbusha serikali! Kwa nini tunachagua wajuvi na welevu(chadema) wakati hata wewe ungeenda na pumba zako hizo
Nakumbuka suala la kikotoo. Wapinzani wakapinga. Wabunge wa chama tawala wakawabeza halafu wakasema ndiooooo. Mheshimiwa Rais akasema kweli suala linatakiwa Liangaliwe upya na liahirishwe, kama walivyosema wakina Esther Bulaya. Wabunge wa chama tawala wakampongeza kwa kuwajali wananchi wake na kupiga chini muswada ambao waliukubali kwa kishindo!

Amandla...
 
Sawa je jimboni kwake kawafanyia mambo gani baada ya kupinga kila kitu miaka 5
Ni kazi ya serikali kufanya maendeleo au ni kazi ya mbunge?
Ndio nyie diwani akisema "ntawajengea barabara... zahanati na shule" mnashangilia pasipo kujiuliza ama kumuuliza mgombea "..mbona wewe huna hata banda umepanga chumba kimoja jangwani haya utayafanyaje?"
Tatizo yaweza kuwa ni zile nnywa za kupokezana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…