Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani alikuambia Mke anasomeshwa!wew ulikosea unheowa kwanza then ungemsomesha wakati ameshakuwa mke wako
Duuuuh! bonge la ushauri mkuu upo vzr sana, salut!Pole sana kwa hilo ndugu.
Duniani kitu ambacho kimekuwa janga kubwa ni MAPENZI. Ulifanya kwa lengo na nia njema ila hayo ndo malipo ya malimwengu. Na Zaidi unasema mliandikishana mkataba, mmmh hapo ni ukakasi, haikutakiwa MKATABA bali NDOA. Hata sasa unasema umefungua kesi mahakamani sijui ya madai au ya mapenzi, Kitu ambacho naona unakosa haki nacho. Mkataba unaokubalika wa kuunganisha watu ni NDOA na wenye dhamana hiyo ni SERIKALI(MKUU WA WILAYA), MAPADRI, MAKASISI na MASHEKHE na wote hao hupewa kibali toka serikalini cha kufungisha ndoa na kwenye kufungisha kila mmoja wenu anaulizwa mara tatu kama karidhia hiyo ndoa mbele ya kadamnasi iliyopo pale (mashahidi), asiye na kibali hicho ndoa atakazofungisha ni batili whether SHEKHE, PADRI AU KASISI. Sasa ninyi mlichofanya kwa mkataba huo haikupi nguvu kisheria kummiliki yule, ila ingekuwa unamsomesha na rehani wameweka nyumba, kiwanja au gari mkataba utakapokengekwa ingekuwa rahisi kisheria kuzuia zile mali zilizo rehani, ila kwa mtu hapo ngumu, labda wanasheria watusaidie hapo.
Nini cha kukushauri baada ya maelezo hapo juu.
-Achana kabisa na kesi hiyo (kaifute), maana hata ukipewa hela na sijui ni ngapi maana kwenye mkataba sidhani kama kuna figure kamili (i.e 3M), maana hela nyingi waweza kuwa umetumia Zaidi ya prediction mliyoandika siku hiyo kwa ku-foresee
-Jipe moyo kuwa umepata hasara kama vile ulikuwa na duka na halina bima then likaungua lote
-Ni muda wa kudeal na vitu vinavyokufurahisha Zaidi tofauti na mapenzi. Usikae peke yako muda mwingi, jichanganye na washikaji zako wengine. (Usijiingize kwenye mapenzi na mtu yeyote kwa sasa mpaka baada ya muda Fulani, let say minimum of 3 months)
-Usimfuatilie yeye na familia yake kwa ujumla. Maana tayari umekiri ni mjamzito na si rahisi hata akisema anarudi leo kama nawe upo tayari kumpokea mtu mwenye mzigo wa njemba nyingine (Hii ni siraha ya kuwaumiza kisaikolojia wenyewe na nafsi zao zitasononeka japo watajikaza kisabuni kutosema kwa uwazi kwa muda, ila mwisho wataisema kwa sauti)
Mwisho, Mitihani imeumbiwa wanadamu na inastage tatu tu, (1)KUTOKEA, (2)KUIKABILI na (3)KUISHINDA/KUISHINDWA (hapa lazima kuwe na jibu moja tu). Sasa chagua KUISHINDA na maisha yatasonga.
Mke hasomeshwiiiiiiiiiii........kamweDear brothers and sisters, uchumba sio ndoa. Usimfanyie vitu vya gharama mchumba. Anaweza kuja kuwa mume/mke wa mtu baadae huyo. Ni mke wako ama mme wako ndio unatakiwa kumgharamia kwa akili yako yote na mali zako zote Na nguvu zako zote.
Wanaume wa DSM sio watu wazuri! Pole sana kaka. Ila kama uko serious unataka kumkomoa, niPMNi Dar es salaam mkuu. Ila kwao ndio mkoani huku
Alafu kiukweli kweli hapo kwenye kumdai hizo hela mahakamani angepotezea tu kabla hajajiumiza mwenyewe, ebu imajin unamdai hizo hela alafu jamaa wake wa sasa anakuja kuzitoa zote kwako tena kash, itauma sana!!Pole mkuu.
Hizi mbinu zipo kitambo sasa.
Huyo binti na mama yake waliona udhaifu wako na wakautumia vizuri hivyo wako sahihi.
Na wewe ulimpenda huyo binti yao lakini ukashindwa kutumia nafasi hiyo kumuoa huyo binti, hivyo wewe ndie uliecheza pata potea.
Ni kosa la kiufundi tu lakini binadamu tunajifunza kutokana na makosa.
Huwezi kufanikiwa kwa kwenda mahakamani kudai fedha zako za matunzo na ada ya chuo, kwani kisheria mkataba mliowekeana na huyo architech ambae ni mama wa huyo binti ni batili na hauna nguvu kisheria.
Sahau yaliyopita, pata muda ujichanganye na marafiki zako, pitia JF ukipata nafasi usome mada zetu za kufikirisha na za kuchekesha, pata bia mbili tatu lakini usilewe, chapa kazi, jenga taifa.
Atatokea tu binti mwingine na Mungu atakuelekeza- kwa sala na maombi.
Pole sana mkuu....unachopaswa kujifunza ni kwamba wanawake ni MBWA....hawaaminiki hata chembe....tena shukuru hajakubambika hiyo mimba aliyojazwa na MBWA mwenzake. Inauma sana.Sikujua laiti ningejua.... Najuta
Wakuu nilikutana na huyu binti miaka kadhaa iliyopita mimi nikiwa nimepangiwa kazi mkoa fulani... katika mihangaiko yangu nikakutana na huyu binti nilitokea kumpenda.. mzuri kisura na kitabia...very innocent niliamini kwake nimefika baada ya kash kash nilizopitia katika mahusiano ya nyuma.
Wanasema usiusemee moyo ila najua yule binti alinipenda kidhati tena moyoni kabisa.. na mimi kwangu she was a queen na niliapa kumuoa baada ya yeye kumaliza masomo yake. Binti huyu kwao ni familia maskini nikisema familia maskini ni familia maskini kisawasawa. Baba yake alifariki miaka kadhaa nyuma kabla sijaonana nae hivyo aliishi na mama yake na wadogo zake.. ni story ndefu kuhusu familia yao. Mimi nikawa ndio kama msaada katika familia yao, sikua na hiyana na nilisaidia niwezavyo kwani binti yule nilimpenda kutoka moyoni.
Yule binti alimaliza shule na kuhitajika kwenda chuo lakini familia ikawa haina uwezo wa kumsomesha na mkopo alikosa. Akakosa raha na ikawa kama jukumu ni langu. Mama yake aliniita tushauriane kwasababu kwao nilikua nafahamika. Kwakuwa mimi nilisema nitamuoa binti wakashauri nimsomeshe kama nina nia yakweli. Uwezo wa kumsomesha nilikua nao nikakubaliana na tukaandikishana kwamba namsomesha mimi lakini mwisho wa siku yeye atakuja kuwa mke wangu na hata mahari sintolipa kwani itakua imeingia huko. Familia ilinishukuru sana kwani waliamini kusoma kwa binti itakua afadhali katika ukombozi wa maisha yao. Binti alikuwepo wakati maandikishano yanafanyika na mashahidi walikuwepo.. nakumbuka binti alilia yule akiapa kunipenda milele na mapenzi tuliyofanya siku hiyo siwezi kusahau... ilikua best sex ever.
Wakuu nifupishe binti alianza chuo kila kitu nililipa.. Nauli.. hosteli ada matumizi kila kitu ilikua mimi ,mwaka wa kwanza ukaisha vizuri mapenzi yanachanua.. likizo naenda likizo zao anakuja.. mama mtu alinishukuru sana. Mwaka. Mwaka wa pili matatizo yakaanza nikipiga sim naambiwa yuko library.mara assignment nikiuliza zaidi anakua mkali nikasema labda labda kweli shule lakini hata mimi nilisoma muda wa kuongea na mwenzi wangu nilikua nao nikasema labda shule ya sasa ni ngumu. Binti akabadilika majibu ya jeuri nikaenda kuongea na mama yake amkanye naona akajirekebishe na kweli akatulia maisha yakaendelea. Upside zikiwa chache. Mahusiano yalitawaliwa na migororo
kufupisha...Miezi kadhaa imepita binti kaniandikia meseji eti "NAKUSHAURI UTAFUTE MWANAMKE MWINGINE MIMI SIKO TAYARI KUWA NA WEWE NIKUTAKIE MAISHA MEMA"
Naandika huu uzi wakuu acha nikipiga simu haipokelewi mara haipatikani. Nikampigia mama yake kumuuliza kama anajua lolote akasema hafaham. Nikaomba likizo kazini nifatilie sikuamini siku naambiwa ana mimba na anaishi na mwanaume mwingine. nilitamani ardhi ipasuke kumbe ndio maana niliandikiwa ule ujumbe nikajiuliza maswali bila majibu... basi angefanya nisijue na mimba juu kapata inauma sana. Kumuuliza mama yake hana analonijibu, kumbe chuo kapostpone sijui anaishi na huyo mwanaume moja ya mitaa Dar.. yote hiyo nafatilia kwa baadhi ya marafiki zake. na kibaya zaidi huyo mwanaume alishamlipa tena huyo mama pesa nyingine. Na ndio kamchukua binti yake.
Nimechukia kuuziwa mbuzi kwa gunia.. Love is blind inakuwaje sikuona yote hayo?? Why me..Why.. najiuliza sipati majibu. sikuwahi kupenda kama nilivyompenda huyo binti. Nilimpenda kutoka moyoni na kujitoa kwake sijawahi kumfanyia mwanamke yoyote niliyomfanyia leo ameniacha kwenye mataa na nyodo juu.. kuna muda natamani ningekua na bastola nimsambaratishe ila that is not me. Juzi nimeona whatsup kaweka picha yake tumbo kule na namba yake nikafuta
NILICHOFANYA
Nimepeleka hii kesi mahakamani kwasababu tuliandikishana kama mke nimekosa basi nilipwe gharama zangu najua haiwezi kuziba pengo.. kufuta maumivu naona is the least i can do for my self... wakuu nifanyaje au nimekosea kupeleka shtaka polisi tumeshaitwa mara mbili hakuna mtu aliyetokea upande wao . Nimetokea kuwachukia wanawake saaaana... kwanini mnatufanyia hivi jamani tuwapende vipi. Nimekaa hapa kitandani nimewaza mawazo mengi moyo wangu kama barafu naishia kusononeka.
Sijui nimfanyie kisasi gani aumie kama mimi nilivyoumia.
Adios.
Mchumba hasomeshwi
Mtu masikini si mtu wa kumwamini hata kidogo
unasomeshwa na mchumba nini?...😀😀😀ila wakimaliza kusoma mishahara yao mnaitaka achangie! mi ukijifanya mchumba hasomeshwi najikausha ila baadae mshahara haukuhusu 100%
ila wakimaliza kusoma mishahara yao mnaitaka achangie! mi ukijifanya mchumba hasomeshwi najikausha ila baadae mshahara haukuhusu 100%
Mwanaume wa kutegemea mshahara wa mke ni MWANAUME WA DAR peke yake.ila wakimaliza kusoma mishahara yao mnaitaka achangie! mi ukijifanya mchumba hasomeshwi najikausha ila baadae mshahara haukuhusu 100%
Wewe ni Mwanaume wa dar bila shakaMshahara achangie nini? Kama mna familia kwa nini asichangie na mkagawana majukumu. Nini maana ya familia?
Me ndo maana naonaga wanawake wana akili za kuku kabisa