Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 11,129
- 7,321
Ulikuwa sahihi kwa sababu ulikuwa nyumbani kwako ila hukutumia hekima kwa sababu uliwaghasi watu ambao walikuwa ni wageni nyumbani kwako, ukiachilia mbali huduma yao ya unaabii. Si kila uamuzi sahihi unaambatana na hekima ndani yake; ungeweza kufanya tofauti na ulivyofanya na bado ukaonekana wa maana zaidi. Ulitakiwa uwaruhusu kwa kuwaomba sauti za uimbaji zisiwe juu, na baada ya kuwa wameondoka ukaangusha sera zako sasa kwa muumini mwenzao, kama ulitamani wasije wakarudi tena nyumbani kwako.Mughonile!
Nilimuoa Mke wangu miaka 9 iliyopita. Kwa sasa tunawatoto wawili.
Mke wangu alikuwa amebobea kwenye Makanisa haya ya upako.
Baada ya kukubaliana na vigezo vyangu, ambacho kimoja wapo nilimuarisha aachane na manabii wa upako, akakubali.
Ndipo nilipomuoa Kwa ndoa takatifu ya kikristo.
Ni miaka 9 sasa imepita, juzi Yule Nabii na waumini wengine walikuja kumtembelea Mke wangu. Tuliwapokea vizuri wakapiga Stori zao.
Tatizo wakataka waanze kuomba na kabla ya kuomba waimbe mapambio Yao. Kwa kweli niliwazuia, niliwaambia tuheshimiane. Kelele nyumbani kwangu ni mwiko na ndio maana ninaishi sehemu yenye makazi tulivu.
Tukazozana, nikawafukuza! Mke wangu ananiambia ninaroho ngumu,
Nikamjibu sio roho ngumu tuu Bali roho mbaya kabisa.
Nimewapiga marufuku kuja kwenye nyumba yangu kujifanya wanajifanya wanaombea ombea watu. Nani anashida na kuombewa hapa!
Nimewaambia wakija waje Kwa inshu nyingine.
Pumbavu!
Zaidi kuwa mwangalifu sana na hawa watumishi wa Mungu; mtu akishaitwa mtumishi wa Mungu, wana kitu fulani cha ziada ambacho watu wengine hatuna kabisa. Hata kama ikitoea ni mtumishi ambaye wewe humkubali, lakini wanakuwaga na kitu cha pekee sana ambacho watu wengine wasio watumishi wa Mungu hawana