Nimemtimua Nabii aliyekuja kumtembelea Mke wangu

Ulikuwa sahihi kwa sababu ulikuwa nyumbani kwako ila hukutumia hekima kwa sababu uliwaghasi watu ambao walikuwa ni wageni nyumbani kwako, ukiachilia mbali huduma yao ya unaabii. Si kila uamuzi sahihi unaambatana na hekima ndani yake; ungeweza kufanya tofauti na ulivyofanya na bado ukaonekana wa maana zaidi. Ulitakiwa uwaruhusu kwa kuwaomba sauti za uimbaji zisiwe juu, na baada ya kuwa wameondoka ukaangusha sera zako sasa kwa muumini mwenzao, kama ulitamani wasije wakarudi tena nyumbani kwako.
Zaidi kuwa mwangalifu sana na hawa watumishi wa Mungu; mtu akishaitwa mtumishi wa Mungu, wana kitu fulani cha ziada ambacho watu wengine hatuna kabisa. Hata kama ikitoea ni mtumishi ambaye wewe humkubali, lakini wanakuwaga na kitu cha pekee sana ambacho watu wengine wasio watumishi wa Mungu hawana
 
Mungu anawapenda sana ndio maana kila siku anawaasa muokoke, hamtaki. amini usiamini, njia ya wokovu waipitao ni wachache, ila njia ya motoni wapo wengi sana. Mungu akusaidie ufunguke macho pengine utapona.
Ndio walewale utafikiria Motoni ulifika, soma utafiti utaelewa neno Jehanamu ilikuwa ni jalala la kumwaga tako huko Palestine leo Israel
na huo Wokovu ndio mmejichagua ninyi wachache hata miliomi 1 hamfiki kwa hiyo tuliobaki Mungu anatuchukia km vile ulikutana nae, sasa hao Bahai wanaosujudu ng'ombe wewe umeshawahukumu
wewe ndio bado mgonjwa funguka macho upone usipoteze muda na sadaka zako,
Tenda mema sali unavyojua usiwadharau wenzako ambao hawaokoki huo moto
 
Mwanaume kichwa
Ishi nae kwa akili
Zipime roho usije kufukuza malaika au ukakaribisha mashetani

Ila ungewaacha waombe halafu hayo maagizo uje umpe mkeo jameni. Kweli wewe mkaxπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Siwezi mwambia mke wangu kipenzi angeniona mnafiki na mwoga kuwa Kwa nini sikusema mbele Yao.

Mke wangu jioni alikuwa anacheka anasema ati Mimi ni bedui, anasema ananifananisha na Baba yake naye alikuwa Mkoloni.
 

Walokole huwajui wewe!

Nilichokifanya ndio Busara na hekima kwani imeleta matokeo chanya.

Hizo zenu sio busara zaidi ya unafiki na nidhamu ya woga
 
Walokole huwajui wewe!

Nilichokifanya ndio Busara na hekima kwani imeleta matokeo chanya.

Hizo zenu sio busara zaidi ya unafiki na nidhamu ya woga
Maamuzi yako yalitawaliwa na chuki zaidi; possibly unawachukia walokole; usiwe una tabia ya kuchukia watu, especially kama tayari uliishafikia umri wa 45+ yrs.
 
Sasa mbona unatufokea mjumbe?? Yaani hapo mwishoni umetufokea kabisa! Sisi tulikuja kutia upako nyumbani kwako na kama ungekubali ile siku Sasa hivi na wewe ungekuwa mume wa Nabii🀣
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Nabii alichomfanyia mzee wangu, nimetokea kuwachukia sana. Hawana huruma, utu, bali wametanguliza mbele maslahi ya pesa
Ilikuaje tupe story tujifunze nna Dada angu anabadili makanisa tu ya kinabii,alianza kwa lusekelo,mwingira,gwajima,suguye,mwamposa sasa yupo kwa kuhani!hapa yuko ibadani kimara!
Yaani ameacha asili yetu kabisa nasikitika sana!anaamini mafuta na maji balaa

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…