Nimemtolea mahari sasa ananipa shida, najuta!

Hii chai, mleta mada anatuchoresha tu...
 
Swali lingine la msingi nakupa kazi nipe hasara za ndoa hata mbili au tatu. Ukiweza kunipa hizo hasara mimi naacha kujadili huu mjadala au nitaomba ID hii ifungwe na wewe utakuwa shahidi wa hili.

Wenye jambo letu tumeingia.
 
Wewe hujaoa..sema umemlipia mahari tu na kumchumkua kama mchumba.sio mke wako huyo
Na ina vyoonesha huna kipato cha kuwsza kumtunza huyo mtoto wa WATU ndo maana frustrations nyingi na kutoelewana.nimehisi hivi sababu unalia lia sana kuhusu mahari ohh million na nusu...hela yangu nimepoteza..wakati kuna wenzio mahari mpaka million nne wanatoa na wapo kimya.
Pia unaweza ikawa na vijitabia vyako wewe mwenyewe ambavyo huvitaji vinamkwaza huyo Dada pia.we sio malaika

Kama humtaki na huwezi mrekebisha nenda kwao waambie wakurudishie hiyo hela yako.
 
Mkuu dawa yake ni mruhusu arudi nyumbani afu jifanye kumpotezea ili aanze kujua umuhimu wako kwanza ndio mambo mengine yatafata stand as a man bwana unaibisha wana

Sent from my TECNO KD7h using JamiiForums mobile app
Huo mda wa kusubilia huyu mpuuzi uko wapi achana nae move on na mgine, akirudi akute kuna mtu.
 
Bora nyie wanaume wenye akili mtusaidie kufunda hawa watoto. Jando halipo siku hizi basi taabu tupu[emoji2297][emoji2297]
 
Wewe jamaa ulijifanya muungwana sana kwa kulipa mahali mapema,mimi wife sikumlipia mahali hadi leo tumeshafikisha watoto watatu.Mahali nitalipa nadhani mwakani.
 
Swali lingine la msingi nakupa kazi nipe hasara za ndoa hata mbili au tatu. Ukiweza kunipa hizo hasara mimi naacha kujadili huu mjadala au nitaomba ID hii ifungwe na wewe utakuwa shahidi wa hili.

Wenye jambo letu tumeingia.
Soma hiyooo.....


Umeomba 2 au 3 nimekupa huo MZIGOO WA HASARA.

#YNWA
 
Tatizo linaanzia hapa, kujidogolisha[emoji16][emoji849]

Ndo maana stori za humu kuziamini mimi ni ngumu sana!
 
Ndoa sio utimamu wa akili.

Kuna walio kwenye ndoa halafu wafanyayo duniani mpaka UNASHANGAA..!!!

Ile top ten ya matajiri wa dunia IMEGUNDUA VITU AMBAVYO HUFANYA DUNIA ITEMBEE ila HAWAJAOA, hapa nazungumzia Bill Gate, Benzos na wengine

Eicher ndio sasa hivi basi mashuhuri kwa usafiri TZ na hasa Dar, mwenye Eicher kampani HAJAO.

Dangote ndio mbabe wa Africa HAJAOA.

Kenya ilishawahi kumiliki BEST JUDGE mkuu ambae hakua ameoa.

Ina maana wotee Hawa HAWANA AKILI?

#YNWA
 
Umemshika.

Huyu na wema sepetu hawana tofauti. Hawafiki 30, wao wakifika 29 wanarudi 25.

Huyu dogo kma shoga hivi.
 
Inatokeaga Ila huenda anamimba

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Nmecheka sana nasema hivi mpaka unakufa huwezi kuweka hasara za ndoa. Wala hakuna aliyeweza kufanya hivyo.

Makosa ya wajinga fulani katika jambo la ndoa hatusemi hizo ni hasara bali ni uzembe wa wana ndoa.

Nakupa miaka mia ulete hasara za NDOA hutaweza wala hakuna aliye wahi kiweza.

Nasubiri hasara za ndoa,siyo ujinga na madhaifu ya wana ndoa kwa kukiuka taratibu za ndoa.

Kingine kwenye Wanaume kuna Wanaume,wanaume hatuwezi hatujadili mambo ya ndoa kitoto na hamasa namna hiyo.

Nataka hoja.
 
Kama hakuna kitu anachocontribute financially,hakikisha unamuacha kabla hamujapa mtoto.
Maumivu yataisha baada ya kuachana ila mukishazaa hata muachane mutatesa mtoto.
Fanya maamuzi magumu,muache kisha relax kwanza hata miaka miwili hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…