Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Jana mchana nilikuwa namsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Anga Tanzania akielezea juu ya ajali ya ndege ndani ya Ziwa Victoria. Nikawa nasoma maoni yanayopita pembeni ya kile kioo cha kinakilishi changu.
Alionekana kama anapiga siasa zile zile tunazozizoea kuzisikia kutoka kwa watanzania pindi inapotokea ajali mbaya yenye kuondoa uhai wa nguvu kazi na wengi kati ya hao marehemu wakiwa ni vijana sana, kwa kweli inasikitisha.
Ni kilio kikubwa kumsikia Mzazi akiongea namna alivyopoteza binti zake wawili tena wakiwa katika umri wa kuzalisha wa ujana. Ni simanzi kumsikiliza kaka yake RIP Rubani akiusoma wasifu wake pale msibani. Kuna yule dada aliyetoka masomoni Uturuki na kufaulu akirudi nyumbani kuiona familia yake kabla hajaanza kuishi, akiwa kijana mdogo sana.
Maisha yanapotutoka ni muda wa kuhuzunika toka ndani kabisa ya moyo. Lakini wenye akili na hekima zinazochanganyika na busara huangalia aina ya ajali iliyotokea na namna gani huko tuendapo tunaweza kuziona kama ni historia ajali hizi.
Mkurugenzi wa TCAA alieleza kwa kina historia ya uwanja wa ndege wa Bukoba na ni ukweli kuwa ile ni ajali ya pili tangu uwanja ule ujengwe na wakoloni mwaka 1940. Pengine ajali ya tatu inaweza kutokea mwaka 2055.
Kizuri ni kwamba kuna uchunguzi wa kitaalam unaoendelea kwa sasa ili kujua kwa kina chanzo cha ajali ile ni kipi haswa, wajuaji wa whatsapp hawajabaki nyuma wametengeza video ambazo kwa kitendo kile ni kosa la jinai lakini ndio TZ yetu ilivyo kila mtu anajua kila kitu!.
Wapo wanaokuja na maoni ya serikali kununua Aerial Loaders kwamba ndege inapozama basi iweze kuinuliwa kwa haraka, ni mawazo mazuri ndio lakini maamuzi ya kina ya kitaasisi yanajumuisha uwepo wa wafanya maamuzi wengi. Na hizi ni ajali tu, hazina kinga kama wasemavyo waswahili na kiswahili chao.
Jeshi la wanamaji linaweza kupitisha bajeti ya mabilioni ya pesa, machine hizo zikanunuliwa na halafu ikapita miaka 35 bila ajali kutokea, hicho chombo kilichonunuliwa kwa pesa nyingi ambazo ni kodi ya wananchi kiwe kinakaa tu bure kikiota kutu eti kikisubiri ajali itokee!.
Ni kweli jeshi la wanamaji inabidi liboreshwe, uwepo wao karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba ni wa muhimu sana kuwepo wakiwa na vifaa vya kisasa, lakini kitaifa tusifanye maamuzi ya kukurupuka na yakajumuisha ufisadi humu humo na mwisho wa siku kitakachonunuliwa kinakuwa ni kama mapambo tu.
Nimemuelewa vyema mkurugenzi wa TCAA. Hakuna sababu ya msingi ya kutahayari na kila mtu akaja na maoni ambayo mengi kati ya hayo hata hayatekelezeki.
Siku njema wapendwa.