CHANGAMOTO YA UWANJA.
..kuna Mhandisi mmoja amehojiwa na Clouds ameeleza vizuri sana kwamba uwanja wa ndege wa Bukoba ni hatarishi.
..ameeleza kwamba runway yake ni fupi na hivyo kuwa changamoto ktk utuaji wa ndege nyingi zinazotumia uwanja huo.
..tatizo lingine ni uwepo wa milima kwa upande mmoja na kisiwa karibu na uwanja hivyo kulazimisha ndege kutua uwanjani hapo kutokea uelekeo mmoja.
..Na huyo Mhandisi amesema aliwasilisha ripoti za uchunguzi wake kwa Katibu Mkuu wa Wizara, RC wa Kagera, RAS wa Kagera, Mamlaka ya viwanja vya ndege, na Wabunge wa mkoa wa Kagera.
..Mhandisi anasema alionya na anaendelea kuonya kwamba uwanja wa Bukoba ni hatari kwa ndege nyingi zinazotua pale.
UZEMBE KTK UOKOAJI.
..Ni kweli kwamba ajali haina kinga.
..Je, uzembe ktk uokoaji nao hauna kinga?
..Hii sio ajali ya kwanza kutokea ktk Ziwa Victoria na kumekuwepo na malalamiko ya vyombo vyetu kukosa utayari na kutokuwa na vifaa.
..Binafsi sijaona kama tumejiongeza au tume'improve toka ajali ya Mv Bukoba, Mv Ukerewe, na sasa ajali ya Precision Airlines.
..Kuna ulazima wa kubadilisha MINDSET ya vyombo vyetu vya usalama ili vitilie mkazo masuala ya uokoaji ktk ajali na pamoja na majango.
..Masuala la mafunzo, na vifaa bora vya kazi lazima yatiliwe mkazo. Kulikuwa kutokea moto ktk kituo chetu cha mpaka wa Rusumo. Ilikuwa AIBU kubwa kwani helikopta ya kuzima moto huo ilibidi itoke Rwanda.
..Kulipotokea baa la Nzige, Tanzania iliaibika tena kwani tulikuwa hatuna ndege ya serikali kupambana na wadudu hao waharibifu.
..Ukiacha mafunzo, na vifaa, kuna suala la TARATIBU ZA UJENZI. Mfano ninaoweza kuutoa hapa ni kutokuwepo kwa njia za kuokoa watu wakati wa ajali ktk barabara zetu. Barabara zetu ni nyembamba mno na hazina nafasi kwa waokoaji kufika eneo ambako kuna ajali.
..Tunaweza kuwa na vifaa na mafunzo ya kutosha lakini kama hakuna miundombinu wezeshi kwa waokoaji tunazidi kufeli.