Nimemuomba wife aniazime kiasi flani cha pesa, ameninyima, ila amejipost kwenye status yuko somewhere anakula bata na mashost zake

Lakini mkuu, kwa mume mtu wake wa karibu ni mkewe, vivyo hivyo kwa mke.

Anayetakiwa kuwa wa kwanza kuonwa ili kutatua changamoto ya mwandani wake ni mmoja wao, labda pale tu anapokuwa hana uwezo wa kufanya hivyo ndo unatakiwa kukimbilia kwa marafiki.
 
nyie ni mbaya ukamtegemea mtu asikupe ndio manaa mnaambiwa pendeni mama zenu nakuwa jali mama yako . Ungemwambia mama yako asimgekunyima angekopa mahali mke ,mume hawa sio wakuwategemea unaanza Mungu .

Halafu wazazi au mzazi halafu watoto wako jichanganye Isenye
 
Jipambanie tu kiongoz hawa watu wako na roho za ubinafsi sana
 
Nilienda chuo kuongeza elimu, Karibu na mitihani nikakwama Ada nikamuonba mwenzangu aniongezee, akakataa katakata. Baada ya kumaliza mitihani nikamtembelea mwenzangu kuangalia simu yake the same day ananikatalia kuniazima Ada ndio siku aliyomuuliza kidume mwenzangu unakula nini, the next step ni kuachana mpaka Leo tunalea mtoto na ndoa Hana.
 
Vijana elewini dhana ya KATAA NDOA.
 
Sasa tufanyeje? NDOA ZA JINSIA MOJA ZIPIGWE VITA.
 
Mke hakopwi.
Ni kutoa amri nitumie laki 1 mke wangu nna kazi nayo.
Kuna namna hamuwajui wake zenu.
Mimi wangu kuna siku kanipigia nikamwambia nataka kula chakula kutoka kwako. Kwa maana atume pesa, rafiki yangu aliyekuwa kando yangu akawa anashangaa. Alipomaliza akauliza atatuma kweli?
Punde akatuma elfu 10 nikale. Nikairudisha nikamwambia I was just joking.

Mnaishije na wake zenu?
 
Pesa ya nwa
 
Mkuu ulitakiwa umwambie mke wangu nitumie laki moja sasa hii kauli inategemea mnaushi vipi na huyu mke wako, kama ana kueshimu na kukupenda lazima atakutumia, na kama na wewe mgumu kwenye pesa zako na haijulikani zinaisha kwenye matumizi gani awezi kukupa.
 
Kwa hili nawapenda Wamarekani sana. Mnakuwa na akaunti tatu. Moja ya wote halafu kila mmoja anakuwa na ya kwake. Ya pamoja inakuwa na pesa mnazoweka pamoja kwa ajili ya bili zote za mwezi huo (mortgage, umeme, maji, chakula n.k) halafu hela zinazobaki kila mtu anatumia anavyotaka japo mwanaume utajikuta zako unaendelea kuzitumia kuhudumia famila kwa vitu vingine vidogo vidogo. Worked perfectly lakini najua huku Bongo hii haiwezekani.
 
Unajuaje Kama yeye ndiye kanunua? Chips yai na Pepsi ni kula bata? Labda kaweka michupa ili kukuamsha wewe ! Yawezekana wewe bahiri kwake pesa zote unamalizia kusiko julikana lazima wakunyime tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…