Leo ota hii mistari ya Prof Jizze..
Prof j : Dada habari, samahani naomba nikuulize swali
Shangingi : Eh maskini hii ngoma ghali eh
Prof J : Dada mbona mkali
Shangingi : Wee Kinyago kubali yaishe
Ngoja nikusahihishe haujui kua hii PIN vijana tuliitumia kutongoza na tulipata zali na tukala tunda, niitumia hii PIN kumtongoza somebody X na akajaa
Unaanza hivi
Naamka asubuhi niko chwiri tena mapema
Nautoa mkeka sakafuni kisha naukunja vema
Nawaza nitakula nini mentali kisha naguna
Naanza kujikongoja kichwa chini mikono nyuma
Naelekea kilingeni nilikopaki mkokoteni
Nasaga na rumba kimshazali nyie acheni
Nawapa hi machizi wananipa peace tunafurahi
Tunapiga stori nyingi wallahi bila maslah
Mara napata zali napeleka kago uswahili
Wananipa buku mbili danga chee nazisunda chini
Wakati natoka huku kijasho chembamba kikinitoka
Nikaona toto ya nguvu nikajikuta nimeropoka
"Dada habari samahani naomba niulize swali"
Akajibu "Maskini koma tafadhali hii ngoma ya ghali"
"Ehee unajua dada-"
"We vipi hebu nipishe!"
"Dada mbona mkali?"
"Wee kinyago, kubali yaishe"
Nikasema inshallah sawa hiyo yote kwa sababu ya fukara
Nisije nikakubaka nitupwe selo nikawe kafara
Nikaachana nae sehemu za nyuma akizitingisha
Nilikula kwa macho hadhi yangu haikuridhisha
Nageuza mkokoteni nakuelekea maskani
Nikawapa stori machizi wakanicheka ikawa utani
Siku moja nililemaa maskani sikuwa na tenda
Na nilikuwa nikitafakari ni vipi siku itakwenda
Kumbe kuna gari ilikuja na kupaki karibu yangu
Sikuweza kuisikia labda sababu ya njaa yangu
Nilishtushwa ghafla na mlio mkali wa honi
Nilipatwa na mshtuko na hofu kubwa moyoni
Kuangalia pembeni ilikuwa imepaki Toyota Surf
Kulikuwa na sura ngeni ya malaika akaomba tafu
Nilisita kunyanyuka kwa sababu nilikuwa mchafu
Na alitoa elfu kumi na alikuwa akitaka dafu
Nilipokea hela alichotaka nilimletea, akakipokea
Tabasamu zito akanitolea nilimpa chenji
"Ohh no keep change, una mawazo mengi itakufariji weekend"
Alikunywa maji ya dafu alitupa na kunikonyeza
Niliganda kama nyamafu nikahisi alinibeza
Alinipa busu la huba shavuni akanichombeza
"I love you" akawasha gari akateleza