Una mtazamo na uelewa hafifu sana juu ya suala zima la afya ya uzazi. Wewe umepima una uhakika kwamba una uwezo wa kumpa mimba mwanamke? Maana wengine huwa wanatukana wanawake zao kuwa wanajaza choo tu, kumbe wao ndo wajaza choo, maana hawana uwezo wa kumjaza mimba mwanamke.
Matatizo ya kutopata watoto kwenye ndoa/mahusiano kulingana na tafiti zinaonyesha kuwa husababishwa na sababu za mwanaume kwa asilimia 50.
Kwa hiyo kabla hujaanza kulaumu wadada wa watu nakushauri nenda kapime wewe kwanza.
By the way, mwanamke atakaekubaliana na hilo sharti lako na yeye atakua ni zoba tu. Ila uzuri mazoba wako wengi siku hizi, so utampata tu wa kufanana naye.