Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Nimemsikiliza Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe katika bandiko hili Mbowe: Najutia kumuamini Rais Samia
View: https://youtu.be/Xjao83Ghy04?si=qSQTeSxIx_8B5a-L
Kiukweli kabisa mimi nimemwelewa sana Mwenyekiti Freeman Mbowe hapa, na hata ningekuwa mimi!, I would have felt the same, but not done the same, I would have done something worthwhile but not maandamano!.

Namuomba sana Mhe. Mbowe, please usipoteze imani na Rais Samia!, kwasababu Rais Samia ninaye mfahamu mimi, sio mtu mwenye ndimi mbili!, namfahamu fika Rais Samia kwa kauli na matendo, yeye kama yeye, hawezi kabisa kusema hivi haiafu akaja kutenda vile!. She is straightforward person and firm, tena usikute yeye kwa intellect yake, japo ndie aliyeongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopitisha miswada hiyo lazima ukakuta yeye wala hajui kuwa mswada sheria ya uchaguzi una ubatili ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu kwasababu yeye sio mwanasheria!.

Japo miswada yote ya serikali, lazima ipite Baraza la Mawaziri ijadiliwe, wakati mswada huu wa sheria ya uchaguzi unajadiliwa, hakuna mtu yeyote mule akiwemo AG, aliyemwambia ukweli Rais Samia kuwa muswada huo una ubatili!, hivyo mtu ambaye sii mwanasheria hawezi kuujua ubatili wa kisheria kwenye vipengele vya miswada mpaka aelezwe na wanasheria!. Hivyo kwa intellect ya Rais Samia, kumlaumu kwa kutoyajua haya ni kumuonea bure!.

Kwa bahati nzuri, mimi ni miongoni wa watu wanaomfahamu Rais Samia sio tuu kwa kauli na matendo, bali kwa kufanya nae mahojiano ya ana kwa ana mara mbili. Mara ya kwanza akiwa Waziri Ofisi ya Makamo wa Rais na mara ya pili akiwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

Wakati akiwa VP nilimfanyia uchambuzi mara mbili
Mara ya kwanza ni hapa Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” na mara ya pili ni hapa "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Na baada ya kuwa Rais wa JMT, pia nilimfanyia uchambuzi mara mbili Psychoanalysis Trends za Viongozi Wetu, Humbleness ya Rais Samia ni Bonafide Genuine, ni asili yake, ni nature yake, ndivyo alivyo, Ila... na Ili kupata Viongozi Bora baadae, Watanzania tujifunze kuwasoma watu kwa asili zao. Mjue Samia alivyo kwa asili yake

Hivyo kwa kauli na matendo, ya Rais Samia, hiki kinachofanyika kwenye miswada hii, naamini kabisa sio yeye, bali waonayafanya haya ni wanasheria, waojua fika ubatili wa muswada huu, lakini wametake advantage ya intellect yake Rais Samia kumsokomezea ubatili tena, ikapelekwa Bungeni, itapitishwa, na kutungwa sheria batili, kisha Rais Samia ataisaini kuanza kutumika, kwa excuse kuwa batili hiyo kwa vile iko kwenye katiba yetu!, then ni batili halali!. Kisheria, batili ni batili, hata ikichomekewa kwenye katiba kiubatili, bado inabaki ni batili, na badala ya kuihalalisha haramu kwa kuichomekea kwenye katiba, haramu hiyo inaiharimisha katiba na kuibatilisha katiba kwa kuifanya kuwa na unajisi!.

Mimi naamini kabisa kwa haya yanayofanyika kuhusu Muswada huu, huyu sio Rais Samia ninaye mfahamu mimi, na naamini kabisa yeye wala hajui kuwa muswada wa sheria ya uchaguzi ni muswada wenye ubatili unaokiuka ibara ya 11 ya katiba ya JMT na kuathiri ibara ya 5, ibara ya 21, ibara ya 39 na ibara ya 67.

Kwa vile yeye sio mwanasheria, hajui kuwa katiba yetu ina ubatili, uliochomekewa kiubatili na awamu zilizopita na Bunge lilolopita unakokwenda kinyume cha Ibara ya 5, ibara 21, ibara ya 39 na ibara ya 67 za Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Nimesema ninaamini kabisa Rais Samia hayajui haya na hapa niliandika Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi, Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!.

Hivyo kitendo cha Freeman Mbowe Kutomwamini Rais Samia, ni kumuonea bure, niliwahi kushauri Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda, ila kama Freeman Mbowe anaona muda aliompa kwenye vikao vya maridhiano unatosha, sasa ndio aanzishe maandamano, huku sio kumtendea haki, namshauri Mbowe, aichukulie miswada hii kama fursa, afanye uhamasishaji na uelimishaji umma wa kufa mtu kwa Watanzania kwa ku invest in people, grassroot people kuhusu haki zao, ili Watanzania kwa mamilioni wajitokeze wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, na 2025 wajitokeze kwa wingi wawapumzishe watu kwa amani kupitia sanduku la kura na sii kupitia maandamano!.

Bahati nzuri sana na mimi nimehudhuria vikao vyote vitatu vya kukusanya maoni ya wadau na mara zote 3 nilipata bahati ya kuchangia.

Mchango wangu kikao cha kwanza ni huu
View: https://youtu.be/PBpjDhH2XiA?si=9dtqZ-1-ZkzWo69t
Mkutano wa pili maoni yangu ni haya
View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=98HTkiMGNsmlLBGz
Na Mkutano wa tatu wa Kamati ya Bunge pia nilitoa maoni.
Nimeandika makala zifutazo kuhusu sheria hizi
Mbowe kutangaza maandamano nimetoa ushauri issues za kisiasa zitatuliwe kisiasa, halafu issues za kisheria zitatuliwe kisheria, utungaji miswada ni issue ya kisheria, baada ya watu kutoa maoni yetu, Bunge likitutungia sheria batili, this time around, we'll have to do something!.

Tangu Rais Samia ameingia madarakani ile March 21, 2021, mimi tuu mwenyewe, nimelisemea jambo hili la katiba, sheria na haki zaidi ya mara 100!,
Mhe. Freeman, rudisha moyo, applies zile 4R za Rais Samia tulisongeshe mbele kwa mbele kwa maslahi mapana ya taifa,wanaompoteza Rais Samia ni wahafidhina wa CCM!

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
Mbowe ana shinikizo kubwa kutoka ndani ya chama kwa baadhi ya wahafidhina kuonyesha kumpuuza na kutaka kumpa nguvu mropokaji hivyo ,mbowe ameyasema aliyo yasema si kwa utashi wake ,nafsi yake haitaki kabisa. wacha tuone mwisho wa maandamano je wataitwa ikulu ndicho wanacho subiri!
 
Mimi nadhani Rais ndio anajuta kumwamini Mbowe

Mbowe alimtoa Dr Slaa bungeni Ili agombee Urais na Kikwete Katikati ya misimu miwili ya JK na ulipofika wakati sahihi wa Dr Slaa kugombea na Mgombea mpya wa CCM 2015 Mbowe akamleta mzee mwenzake wa Kanisa Edward na kumtupa Kule Dr Slaa
Sasa Ndio Rais wa JMT amuamini Kinyonga wa aina hii?!!

Mlale Unono 😄
 
Samia asingekuwa na ndimi mbili asingeshindwa kufanya haya.

1. Angerudisha pesa za plea bargain alizokiri zilifichwa uchina.

2. Waliotajwa walichezesha invoice ya malipo kwa ndege mpya ya mizigo ya ATCL kwa madai ya kuchelewa vifaa sabab ya covid 19 angewachukulia hatua.

3.Samia alikubali kuendelea na ex-DPP Biswalo Mganga huyu mtu ni very corrupt madili aliyocheza enzi za Magufuli yalipaswa awe mtu wa kwanza kuburuzwa kortini ila akaishia kupewa ujaji.

4.Wezi wote na watu waliofilisiwa mali zao japo walilipwa ila sio wote kuna waliobaki na maumivu ya utawala ambao Samia alikuwa sehemu yake.
 
Mbowe kaingia kwenye mtego WA maadui wa Samia halafu anakuja kumlaumu Samia?

Sio yeye aliepewa "agenda ya bandari za watanganyika" akaibeba Kwa mikono miwili?

Yeye alifikiri waliompa hiyo agenda Wana plan gani?..hajui plan ilikuwa kumuweka mbali kabisa na Rais Samia na wamefanikiwa?..

Yeye Mbowe aliposema eti usalama wa Taifa wamemuelekeza apiganie "bandari za watanganyika" hakujiuliza hao usalama wa Taifa walikuwa wapi wakati Ben Saanane anapotea?walimueleza hata alipozikwa?...

Sasa why maandamano? Why asisubiri maelekezo mengine ya hao alio claim ni "usalama wa Taifa"...?
Binafsi nilishasema humu wameacha agenda Yao ya Kariba mpya na maridhiano...wakadaka agenda za "kundi lenye agenda zake"...wakakubali kugeuzwa "pressure group""...

Mbowe alikaa kimya hata wakati Tundu Lissu anamtukana hadharani Samia.....kumbe yote hiyo ni agenda za watu....wametumika now hakuna wa kuwasililiza...wanataka kujaribu maandamano knowingly very well hakuna watakachopata.....siasa za kuwa pressure group zilishafeli....
 
Kwa vile yeye sio mwanasheria, hajui kuwa katiba yetu ni batili, kwa kuchomekewa ubatili unakokwenda kinyume cha Ibara ya 5 na ibara ya 11 ya Katiba yetu.
Rais wa nchi hapaswi kujua kila kitu, anapaswa kujua akitaka kujua afanye nini. Rais ana nguvu za kuteua Washauri , maafisa na Watendaji wa kumsaidia. Kazi ya Rais ni kuratibu (organization) na ujumuishi (harmonization) ya shughuli ili kutoa majibu. Hatuwezi kumpa 'pass' kwa 'flimsy excuse'

Hivyo kitendo cha Freeman Mbowe Kutomwamini Rais Samia, ni kumuonea bure
Nakubaliana nawe kwamba ni kumuonea Rais SSH kwasababu hizi .
Mbowe alijua CCM hawajawahi kuwa na ni njema hata kwa bahati mbaya.

Mbowe akatoa 'turufu' ya negotiation bure kwa SSS, kumpa nafasi ya kupoteza muda, ambayo SSH ameitumia.

Mbowe hakusikiliza Jamii inamwambia nini na kukaidi 'vox populi vox dei'

Mbowe akaingia katika maridhiano na ' ku-ignore history' ambayo leo inamuonyesha ukweli

Mbowe akaingia katika maridhiano bila ''bargaining chip' wakati akiwa na upper hand. ''Akauza ghala la silaha''

Kumalumu SSH kwa ujinga ni kosa, siasa ni kama mchezo wa soccer.
Mpinzania ana score ukifanya kosa. Kawaulize Simba SC walipocheza na Singida.

Mbowe alicheza fyongo SSH akatumia mwanya! asilaumiwe.
Katiba ni mwongozo wetu sote, Wazalendo, Raia wema, majambazi, panya road, Dada Poa, Mama Ntilie, Vigagula , watoa majini, wauza maji , Nagariba, Wakeketaji n.k. Kulifanya jambo hili ni la kisiasa si kuwatende haki Wananchi.

Kwa nchi za wenzetu mbona vumbi lingeshatimka kuanzia siku Warioba amefikisha maoni yetu?

Rais SSH atumie 'ujinga' wa Watanzania kuwasikiliza maana ipo siku wakiamua hatakuwa na nafasi.

Hili la Maandamano lilikuwa lifanyike miaka mingi iliyopjta. Haki haiombwi, inadaiwa.

Kama kuna anayedhani Katiba haimhusu, basi asubiri maumivu kwa miaka mingi.
 
Sioni kama kuna lolote ambalo linahitaji maridhiano.

There is none.

Wala hakujawahi kuwepo.

As batili as it is, hata yaliyofanyika yakivunjwa ni sahihi pia maana ni batili toka mwanzo.
 
Baada ya kusikiliza michango yako na ibara za katiba unazodai zimepokwa haki na sheria ya uchaguzi kwa wagombea huru sio lazima wawe na chama.


Ibara ya 5 unayo refer aina literal ambiguity zozote, hakuna mahala inaongelea wagombea isipokuwa haki za kupiga kura tu. Moreover imeacha nafasi ya hizo haki hizo kanuni zake kutungiwa sheria na bunge.

Kwa hivyo hata kama ibara ya 5 ingekuwa inaongelea haki za kugombea (kitu ambacho sio sahihi kama unavyodai) bado katiba imetaja tu mtu huyo awe na miaka 18, lakini bunge limepewa rungu la kutunga kanuni za ushiriki wake likisema mtu ili agombee lazima apitie chama cha siasa hakuna katiba iliyovunjwa hapo.



Ibara ya 21 inaongelea uhuru wa kushiriki shughuli za umma, either kwa kuchaguliwa na wapiga kura, kuteuliwa au kwa ku support mtu (hapo kwenye ku support mtu ndio ibara ya 5 inapoingia) lakini hii ibara aisemi haki ya kuwa na mgombea independent. Imeenda mbele zaidi hata hizo haki zinazotelewa kwenye ibara hazipo juu ya ibara 5, 39 na 67.



Ibara ya 67 ipo wazi ili ugombe nafasi ya ubunge lazima uwe na miaka 21 na kupitia chama cha siasa, hakuna mgombea huru na wala hii ibara aijikanganyi na ibara nyingine yeyote.
Ibara ya 5 inaelezea haki za kupiga kura
Ibara ya 21 inaelezea haki ya kushiriki shughuli za umma bila ya kuathiri ibara 5, 39 na 67 (ambayo inaelezea sifa za mgombea).

Sasa basi hypothetically ingekuwa kweli ibara ya 5 imeelezea haki za kugombea (kitu ambacho sio kweli) wewe kusema waandishi wakatiba walikusudia nini ili kuonyesha ambiguous ndani ya katiba mahakamani ungeombwa upeleke ushahidi wa hansards za michango ya bunge kuonyesha kweli lengo la ibara ya 5 lilikuwa kutoa haki kwa wagombea huru.

Uwezi kutoa tu kichwani kwako kwa sababu umesoma sheria na kudhani hiyo ndio sheria.

Haya ndio mambo Magufuli hakutaka ya kuchekeana na upinzani wao mradi wapinge tu, na kupotezeana muda na hela kwenye kujenga nchi. Hata ukisikiliza hizo za CDM, ACT na wengineo for the most part ni nonsense tupu, ambazo Magufuli hakuwa na muda wa ku-entertain.

Ukiwasikiliza wanasheria wa Tanzania hakuna kesi ya kushinda ulaya, labda yule jamaa au sijui taasisi iliyokuwa na website ya ‘Jaba-Shadrack’ waliobaki hamna kitu.
 
Is it fair to call Mbowe ‘naive’?

Iweje mbeba maboksi kama mimi ambaye sina elimu yoyote ile niyaone yote haya tangu awali kabisa walipotangaza hayo mazungumzo ya maridhiano halafu yeye Mbowe asiyaone? Yeye ni career politician. Mimi ni mbeba maboksi tu.

I think I have better discernment than he does.

MaCCM wameitawala nchi hii kwa zaidi ya miaka 60! Nadhani kwa mtu yeyote mwenye common sense nzuri, hatopata shida kuwajua hao jamaa jinsi walivyo.
 
Heading yako tu imekaa kipuuzi. Uko upande wa Serikali kupinga maandamano ya amani. No wonder huoni tatizo wanajeshi kutumiwa kwenye siasa za ndani ya Nchi. Ningekuheshimu kama usingekuwa mnafiki.
 
Mhe. Freeman, rudisha moyo, applies zile 4R za Rais Samia tulisongeshe mbele kwa mbele.
Utasongaje mbele wakati Samia 4R hazitekelezi ila ni gheresha tu? Think deep, you shuld no think while anticipating to please samia for a nomination!...... unatafuta uteuzi tu. Mtu anakudanganya na wewe unakuwa zuzu eti kuna R4 ambazo ni cosmetic tu na mwenye kuzipendekeza hazitekelezi. Unaona kabisa kuwa huyu anataka kuwatoa kwenye reli..
SWALI: SAMIA ANAONA UGUMU GANI KULETA KATIBA MPYA? KUANDIKA MISWADA KAMA WADAU WALIVYOSHAURI? ANAOGOPA NINI? KUNA MADHARA GANI? Mpelekee maswali hayo akupe majibu utuletee hapa Pascal Mayalla
 
Ninyi watanzania wenyewe kwa ujinga wenu, njaa au unafiki ndio kikwazo cha maendeleo yenu!
 
Mimi mnanishanagaza watu wa Tanzania hii. Sifa nzuri nzuri anayepongezwa ni rais. Mfano utasikia, TRA imevuka lengo la makusanyo. Rais Samia apewe sifa. Mara sijui umeme wa uhakika, rais apewe sifa.
Ila zikika sifa mbaya za serikali mnataka kumtenganisha na sifa hizo. Kwangu ukisema yeye si mwanasheria anaweza kuwa hajui ubatili wa katiba si utetezi maana rais hatutegemei ajue kila kitu ila kazungukwa na wataa ambao inapaswa awatumie.
Mbowe kavuna alichopanda taingia mwanzo yale maridhiano yalikuwa ni janja janja tu.
Maridhiano ilikuwa ni marekebisho ya katiba si kuitwa ikulu upewe fadhila.
Mtu akikupa fadhila kesho anaweza zichukua kama ambavyo wana ccm mnadai kuruhusu mikutano ya kisiasa ni huruma ya rais Samia kwa wapinzani
 
Is it fair to call Mbowe ‘naive’?
No question about it!
Ilikuwa ni ' naivety' wala haikuhitaji 'political savvy'

Mbowe hatumia 'turufu' ku-force CCM badala yake akawa Submissive.

CCM haijawahi kuwa na nia njema, kuna historia ya kutosha nchini ikiwemo ya 'maridhiano' Zanzibar.
Mbowe alishaingia maridhiano 'Mwanza kwa Magufuli' kilichofuata historia.

Kufungwa ilikuwa siasa kwasababu ya nguvu iliyokuwa nyuma ya Mbowe kudai Katiba mpya.

Kikosi kazi kiliundwa ili kupoteza Rasimu ya Warioba na kupoteza habari za CDM.

SSH akajua ili kufanikisha lengo la Kikosi kazi lazima lazima amwachie Mbowe, akamwachia.
Hii ilikuwa turufu ya kwanza kwamba Mbowe na Chadema walikuwa na 'upper hand'

Kitendo cha kumtoa Magereza na kumwita Ikulu ilikuwa kumnyamazisha na kumfanya 'sehemu' ya mchakato.

Mbowe bila kujiuliza akaenda akiwa na kila sababu za kukutana na watu wake kwanza ili kumarisha nguvu.
Mbowe alipaswa kuonyesha ni 'force to reckon with'' hakutumia fursa hiyo, akaamua kuwa submissive

Hakuna mtu aliyekubali kitendo kile, Mbowe akamwaga 'cold water' katika harakati na siasa za nchi.

Haikuhitaji elimu , ujuzi au uzoefu , ilikuwa ni busara tu kuona CCM ni laghai, historia ipo wazi maktaba

Mbowe alipaswa kuweka 'bargaining chip' mezani, hakuweka akaamini 'mama ana nia njema.

Kwanza, ' COVID-19' waondolewe. Pili, mazungumzo kwa 'vipindi vya miezi 3' na utakalezaji wa kila hatua ukamilike kabla ya hatua nyingine.

Mwenyekiti wa CDM hakufanya akaamini nia njema, leo nikimsikia anasema 'hana imani na SSH na CCM' namshangaa, wao wamefanya walichokusudia na kufanikiwa, hawahitaji Imani ya Mbowe.

Cry wolf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…