Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

Mapenzi ya dhati yakoje?

Sijawahi kukutana nayo. Laiti yangekuwa yanauzwa dukani!

Hahahaha mapenzi ya dhati yapo babu DC shida nikuyapata. Huyo mleta mada anataka mapenzi ya dhati ndio maana kasita kumzalia dogo watoto. Hivi anafikiri huyo dogo anapita kwa watu kuomba ushauri? Mimi namshauri afuate ushairi wa The Boss maana akishafika 50yrs atakuwa nungayembe
 
Last edited by a moderator:
Piga picha mkionaa, baada ya miaka 10 yeye atakuwa early 40's umri uleeee... halafu wewe ndio uko kwenye mid 50's utakuja hapa hapa kulia tena kwamba mwanaume hatulii.

Sometimes wanaume tuna fantasy za ajabu ajabu, uwe makini kutofautisha fantasy na love
 
dada mpaka sa8 usiku mnaongea tuu live bila chenga wala umeme kukatikakatika??
ushauri....wewe kama mnapendana bebaneni tu muoane tena kwa shangwe zote! wambie unamiaka28! kwani wakwe watadai cheti cha kuzaliwa???

rubii bhana...napenda sana unavyowaza nje ya box! Ndugu wa kijana walileta pye pyeeee waambie hutaoana nao utaoana na kijana wao!
 
Last edited by a moderator:
Nan ana hiyo imani sasa ivi?

Yuko kaka mmoja mtaani kwetu,ni msomi wa kiwango wa Masters plus vyeti vingi vingi tu nyemelezi...ni mtumishi mkufunzi wa chuo mwenye hela nzuri tu....sio kasisi...anakimbilia 50 hakuwahi kupata 'kashfa yoyote' ya kukutwa kasimama na binti na bado anataraji kuoa, kupata watoto na kuwalea...Mimi huwa namwombea aishi miaka walau 150 ili walau aweze kushuhudia mwanae akiwa na mtoto!
 
Yuko kaka mmoja mtaani kwetu,ni msomi wa kiwango wa Masters plus vyeti vingi vingi tu nyemelezi...ni mtumishi mkufunzi wa chuo mwenye hela nzuri tu....sio kasisi...anakimbilia 50 hakuwahi kupata 'kashfa yoyote' ya kukutwa kasimama na binti na bado anataraji kuoa, kupata watoto na kuwalea...Mimi huwa namwombea aishi miaka walau 150 ili walau aweze kushuhudia mwanae akiwa na mtoto!

Kabisaa mkuu wapo wengi wa ivo yaani wengi sana....wanaogopaga
 
Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika taasisi ya serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja. Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulishabadishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula. Semina iliisha Ijumaa na tuligwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi ninamiaka mingapi? Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alistuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka. Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je ninamtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye anamiaka 31, anakazi nzuri sana.


Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwasababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake. Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza anamiaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu!! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao. Ushauri jamani.

miaka 44 bado unapuyanga? kweli dunia ina mambo!!
 

Mweeee najuta kupoteza muda wangu kutoa ushauri!
Lkn sio mby
 
In a way tulikuwa tunaongea akaniambia ukikutana na mama yangu wakati unadamu yake mikononi hatakuwa na jinsi, aliongea kama utani lakini ilikuwa sentensi nzito

nzito kwa sasa dia!

baadae opposite yake inaweza pia ikawa nzito hivyohivyo

wengi sana wanakuja na hizo stori eti mama kasema tatizo ni dini, umri, kabila, ukoo...... unamuuliza kwani wewe hukujua mwanzoni kuwa ndugu zako hawapendi? anakuambia mimi sikujua kama watangangania hivi, mara wananitenga, bibi anaumwa ananiachia laana.......... hautakuwa wa kwanza wala wa mwisho ishue kama hizi za msingi kabisa kama zipotiliwa msisitizo mwanzoni huvunja ndoa

ila kama wanavyosema hapo wengine, kama wewe ni wale wa kuzaa watoto na kulea na mzazi mmoja kwa hiari endelea, ila ujue mwanao hatapata ndugu wa damu kabisa watakuwa nusunusu, kama unaweza kukaa kuendelea kusubiri au kulea mtoto mdogo wa mtu mwenye shida, ni muda wa kufanya maamuzi, sasa
 
Kaizer babu Asprin yukwapi aje kuongeza mke hapa!??
Sky Eclat either utuambie unamuombea shosti ako ushauri au ni ipi kati ya thread zako ni ya ukweli...!


 
Last edited by a moderator:
dada mpaka sa8 usiku mnaongea tuu live bila chenga wala umeme kukatikakatika??
ushauri....wewe kama mnapendana bebaneni tu muoane tena kwa shangwe zote! wambie unamiaka28! kwani wakwe watadai cheti cha kuzaliwa???

Hahahaahhaaah alafu tanesco uwaga wana makusudii😁😁😁
 
Huyo kijana baadae atakuacha. Yeye bado mbichi na wewe huna muda mrefu unaweza kuwa huna hamu ya tendo la ndoa.
 
Pole sana my dada, kama mnapendana uamuzi ni wenu ila kama ndoa haiwezekani basi hata upate mtoto tu...pole
 
We Eli79 unaoa kila mwaka? Washafika wangapi sasa?


Hahahahaaaaa... Unamfahamu mfalme mswati? atoto ujue nyie watu ni watamu balaa, nashindwa kuvumilia niliona kitamu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom