Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika taasisi ya serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja. Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulishabadishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula. Semina iliisha Ijumaa na tuligwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.
Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi ninamiaka mingapi? Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alistuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka. Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je ninamtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye anamiaka 31, anakazi nzuri sana.
Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwasababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake. Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza anamiaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu!! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao. Ushauri jamani.