Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

Huwa mnalinga sana, dharau ma nyodo. Mkizeeka hata watoto wadogo mtataka wawaoe.

Khaa we bana weeee!! umenifanya niandike kitu wakati nilipanga kuwa msomaji tu!!
 
Pole sana my dada, kama mnapendana uamuzi ni wenu ila kama ndoa haiwezekani basi hata upate mtoto tu...pole

Huyo mtoto alelewe na nani?
Watu wakifikisha 44 watoto washamaliza Chuo na wa mwisho Form 1.
Hapo usizae tu maana hata ovaries zitakuwa zishaexpire.
Mtasababisha watoto waishi maisha ya shida maana kufa mtawahi kufa
 
atakaetoa kibali cha yeye kupata ujauzito na kujifungua salama ndie huyo huyo atakaemlea mtoto, umri huo atapata mtoto japo possibility ya operation ni kubwa
Hongera kwa shombo zako naona ulitoa rushwa kwa mungu akakujaalia hongera
 
Hivi miaka 44 wanazaa bila shida?

nafikiri ana wasiwasi akikuoa atapata watoto?
ndo maana anataka mzae kwanza

na wewe ukuendelea kusubiri utazaa na mika 50?

nafikiri huna choice...zaa nae hata asipokuoa angalau utakua na mtoto

tena zaa nae watoto wawili kwa haraka haraka halafu muache mwenyewe aamue kukuoa au kutokuoa.....

The Boss hapa umemaliza mchezo wote na kama ni mjadala umeufunga.......wazo lako ndio suluhisho kwa huyo dada, dogo ana wasiwasi asijekuuvaa mkenge.
 
Ndio maana Namkumbukaga Tyta zilikua kazi zake hizi huku Jf BTW ahsante mkuu
 
Last edited by a moderator:
Hamna future ktk mapenzi. Mna pass time tu na mapenzi ya kimujini mujini.

Vv
 
atakaetoa kibali cha yeye kupata ujauzito na kujifungua salama ndie huyo huyo atakaemlea mtoto, umri huo atapata mtoto japo possibility ya operation ni kubwa
Hongera kwa shombo zako naona ulitoa rushwa kwa mungu akakujaalia hongera

Inaonesha we nae uko kwenye hilo kundi.
Maana umekuja juu sana

mkuu yashakukuta nn?

Hapana mkuu ila ndo huwa wanaringa mwisho wanakuwa kama daladala kila mtu analipanda afu yakiwafika shingoni ndo wanakumbuka kuna kuzaa wakati hata kizazi hakimo, bora wajitangaze kama Wema kuwa hawawezi pata watoto.
 
Hiyo tofauti ya umri ni kubwa sana miaka 12 hapana. Ila kama huna mtoto na unapenda kuwa na mtoto au unapenda kuzaa naye sawa fanya hivyo. Kisha endelea na maisha yako huku mwanao akiwa na baba maadam kasema mwenyewe.

Ila kiungwana kuolewa naye hapana jamani. Mwache kijana wa watu apate mtu atakayeendana naye. Ingekuwa umemzidi miaka 2 au hata 4 angalau lakini mwanamke mkubwa kwa mwanaume kwa miaka 12 hapana. Chukulia huyo ni mwanao alafu anakuletea mkwe wako wa tofauti ya miaka hiyo utaichukuliaje?
 
Hahahahaaaaa... Unamfahamu mfalme mswati? atoto ujue nyie watu ni watamu balaa, nashindwa kuvumilia niliona kitamu!

Mweeeeeh!!! Huo utamu uliuonja lini?
 
Last edited by a moderator:
Kila la heri na huyo kijana na hongera sana kwa kujitunza na kuonekana una umri wa miaka 28 wakati umri wako halisi ni miaka 44. Umesema umempenda sana huyo kijana na yeye inaelekea anakupenda sana maana hata baada ya kujua umri wako wa kweli hakuingia mitini. Kama nawe unataka hata mtoto mmoja bila kujali kama mtafunga pingu za maisha au la basi kila la heri katika kujaribu ujauzito ila kama hauko tayari kuwa na mtoto kama hujui hatima ya penzi lenu basi mwambie ukweli. Mapenzi yanaweza kustawi popote pale bila kujali umri wa wahusika, na kwa maoni yangu tofauti ya umri kwa miaka 12 si kubwa kihivyo. Kila la heri katika penzi lenu.

Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika taasisi ya serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja. Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulishabadishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula. Semina iliisha Ijumaa na tuligwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi ninamiaka mingapi? Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alistuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka. Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je ninamtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye anamiaka 31, anakazi nzuri sana.

Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwasababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake. Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza anamiaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu!! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao. Ushauri jamani.
 
Last edited by a moderator:
Hivi miaka 44 wanazaa bila shida?

nafikiri ana wasiwasi akikuoa atapata watoto?
ndo maana anataka mzae kwanza

na wewe ukuendelea kusubiri utazaa na mika 50?

nafikiri huna choice...zaa nae hata asipokuoa angalau utakua na mtoto

tena zaa nae watoto wawili kwa haraka haraka halafu muache mwenyewe aamue kukuoa au kutokuoa.....

Mkuu..mm mwenyewe nilikuwa najiuliza kama 44yrs kwa mwanamke anaweza kuzaa bila matatizo..ulaya sawa but huku Africa.!.kuwa makini..na nadhani ungeenda kwa daktari akakucheki akupe na advise kabisaa..I hope sasa huna jinsi umefikia the point of no return..doctor akisema upo ok wewe zaa..sidhani kama utashindwa kumlea mtt hata kama ataingia mitini!
 
Ni kweli alinidump kwa mara ya pili that is a true story and this one is true story. Ninaleta hapa yale yanayoniumbua rohoni ambayo siwezi hadithia watu wanaoweza kunijudge.
 
Mkuu wengi wanapata ujauzito na wanajifungua bila matatizo hasa kama afya haina mgogoro wowote. Ila pia kuna wale ambao hata kupata ujauzito inakuwa ngumu na hata wanapobahatika kuupata mara nyingi madaktari ili kuhakikisha afya ya mama na ya mtoto hutoa recommendation ya C-Section.

Mkuu..mm mwenyewe nilikuwa najiuliza kama 44yrs kwa mwanamke anaweza kuzaa bila matatizo..ulaya sawa but huku Africa.!.kuwa makini..na nadhani ungeenda kwa daktari akakucheki akupe na advise kabisaa..I hope sasa huna jinsi umefikia the point of no return..doctor akisema upo ok wewe zaa..sidhani kama utashindwa kumlea mtt hata kama ataingia mitini!
 
Miaka 44 kwani bado wanazaa?? Mmh..watu wengine nyie, miaka 44 yote hiyo bado tu unatutaka sisi wa 31??? Hebu muache jamaa akakung'ute vzuri saiz yake...

Skumuita amekuja mwenyewe.
 
Back
Top Bottom