Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

ukiwa kwenye harakati Za kujifungua mtoto taahira, utakufa..na huu ndio mwisho wa hadithi yakoo nzuuuri
 
kwa kweli kila mtu anahesab zake kichwani. mimi bajet zangu n kwamba ningekosa wa kuishi nae basi nindetafuta wa kuzaa nae. anyway uulize moyo wako
 
Yaani at 44 unajiuliza uzae au usizae. Dadangu siku zako za kuzaa ziko ukingoni. Kama jamaa yuko tayari wewe zaa tu kama unaweza hata asipokuoa utalea mwenyewe.

Halafu naona na yeye anataka ku-make sure kama bado una uwezo wa kuzaa Ili ndoa isije ikakataa kuitika...
 
Kumbuka Sarah alizaa uzeeni. Sikupenda iwe hivi, nilipanga niolewe watoto niwazae kwenye ndoa.
Biblia ni tabu lilijaa urongo mwingi, siku nyingine usiinukuu kwenye mambo ya msingi. Pole kwa hiyo changamoto... Ushauri wangu ni kuwa usiendeshwe sana na umuhimu wa kuzaa, mnaweza kuasii mtoto kisheria na maisha yakasonga.

Wapo waliozaa watoto wao wenyewe na wanawaendesha puta hadi uzeeni, mateja na machangudoa. Furahia maisha mama, kabla wakati haujataradadi.

Karibu mama!
 
kijana atakua mpuuzi kama atawaambia umri wako wakati anajua italeta shida.
kikubwa awe ''mwanaume'' tu na asimamie anachokiamini.kama wewe ndio mwanamke anaemtaka then he has to stand for you kuhakikisha linakua.
ila tu angalizo dada angu;kama na wewe unampenda kweli na hufanyi lolote kwa shinikizo labda la umri au jamii yako na yeye anakupenda kweli tu, ndio muendelee.vinginevyo mtaumizana ajabu
 
Mimi pia dada angu nakushauri uzae nae. Huna sababu ya kuomba hata ushauri kwani wengi tutakukwaza sana kusema wewe mkubwa na wakati mwingine haifai kusema hivyo. Mungu ana kila sababu juu ya maisha yako.

Hakuna kinachofaa machoni mwa watu isipokuwa angalia moyo wako unakutuma wapi zaidi. Ninachoweza kukuambia ni kuwa: unavyojisikia amani fanya hivyo otherwise utakuja kupoteza bahati yako. Wahenga husema: bahati haiji mara mbili.

FIKIRIA THEN CHUKUA HATUA.
 
Huyo kijana mla mbu.nye tu, hakuna muoaji. Ila kama uko tayari kuzaa na kulea mwenyewe, chukua mbegu fasta. Huu ndio msimu wa upandaji.
 
unasubiri nn? we zaa nae akuoe asikuoe safi tu.hebu ona unazaa una miaka 45, ukistaafu miaka 60 mtoto ana 15yrs form 1. unakulakula penshen miaka 63 anamaliza f4. f6 na chuo hapo lazima uombe msaada wa kumsomesha maana pensheni ishaisha, lakini ndie atakae kulea uzeeni we zaa nae tu.
 
Kama anakupenda kwa dhati mwambie utazalia ukiwa kwenye ndoa maana usikute shida yake ni mtoto kutoka kwako. Halafu jambo jingine imekuwaje unafikia 44 bila kuwa na mume?

hee wee vipi, kwani imeandikwa wapi ukiwa umri mkubwa kias gani lazima uwe na Mme or mke? Mungu ndiyo ajua, so that question isnt proper at ol, "bold red italised, undelined sentence", tena apologise kwa mleta mada
 
unasubiri nn? we zaa nae akuoe asikuoe safi tu.hebu ona unazaa una miaka 45, ukistaafu miaka 60 mtoto ana 15yrs form 1. unakulakula penshen miaka 63 anamaliza f4. f6 na chuo hapo lazima uombe msaada wa kumsomesha maana pensheni ishaisha, lakini ndie atakae kulea uzeeni we zaa nae tu.

daah watu mnajua calculations hiziiiii.....kama masecretary wa Mungu.
 
Mimi pia dada angu nakushauri uzae nae. Huna sababu ya kuomba hata ushauri kwani wengi tutakukwaza sana kusema wewe mkubwa na wakati mwingine haifai kusema hivyo. Mungu ana kila sababu juu ya maisha yako.

Hakuna kinachofaa machoni mwa watu isipokuwa angalia moyo wako unakutuma wapi zaidi. Ninachoweza kukuambia ni kuwa: unavyojisikia amani fanya hivyo otherwise utakuja kupoteza bahati yako. Wahenga husema: bahati haiji mara mbili.

FIKIRIA THEN CHUKUA HATUA.

safi sana Nice words..... asisikilize argumentation za watu hapa sana sana watamkandia tuu.. fata moyo wako dada.
 
Back
Top Bottom