Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika Taasisi ya Serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja.

Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulibadilishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula.

Semina iliisha Ijumaa na tuliagwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi nina miaka mingapi?

Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alishtuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka.

Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je nina mtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye ana miaka 31, anakazi nzuri sana.

Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwa sababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake.

Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza ana miaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao.

Ushauri jamani

if u think anakupenda olewa na zaa, kila kitu kina uzuri na ubaya wake, wapo wakaka wengine hupenda women walio wazid umri coz wana busara sana they cant match na women of the same age.
 
Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika Taasisi ya Serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja.

Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulibadilishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula.

Semina iliisha Ijumaa na tuliagwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi nina miaka mingapi?

Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alishtuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka.

Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je nina mtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye ana miaka 31, anakazi nzuri sana.

Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwa sababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake.

Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza ana miaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao.

Ushauri jamani

Pole. Kidini hiyo offer siyo,Kidunia ni offer ya kukimbilia. Kazi kwako.
 
u

huyo kaka anasema kwao wataleta zengwe,kwahiyo ataenda kuwatangazia ndugu zake kuwa umemzidi?..
If so,hayupo tayari kukudefend huko kwao!?

Dada yangu muombe mungu,ukipata amani moyoni jua ndie ,na km ndie hakutakuwa na chochote kitakachozuia,means kila mmoja wenu atakua tayari kudefen penzi lenu!!

Nb:naona anataka kujua km unaweza kuzaa.
Mtazamo wangu tu!!!

hili swali linashangaza sana. Hivi unataka awadanganye wazazi na ndugu zake kuhusu umri? Wewe ni wa ajabu kabisa.
Kuhusu kujua kuzaa, mwanamme yeyote wa kiafrika aliye kamili asiyechanganya ndoa na siasa interest yake ya kuoa ni watoto, hivyo kama ana uhakika mwanamke hatazaa hawezi kuoa hapo.
 
Na yeye anapenda kupotezewa muda.

kama ankupenda kweli akuowe. mtoto mtapata maana ni mpango wa Mungu na pia MAPENZI ni suala la watu wawili na ni makubaliano yao si ya jamii dada yako hana maamuzi juu ya mahusiano yako zaidi ya kukushauri kama sisi maamuzi unayo wewe kama muhusika mkuu.
 
hili swali linashangaza sana. Hivi unataka awadanganye wazazi na ndugu zake kuhusu umri? Wewe ni wa ajabu kabisa.
Kuhusu kujua kuzaa, mwanamme yeyote wa kiafrika aliye kamili asiyechanganya ndoa na siasa interest yake ya kuoa ni watoto, hivyo kama ana uhakika mwanamke hatazaa hawezi kuoa hapo.

Hebu soma vzr comment Yangu!hakuna mahali nimesema awadanganye wazazi wake!!

Soma tena!
 
Hivi miaka 44 wanazaa bila shida?

nafikiri ana wasiwasi akikuoa atapata watoto?
ndo maana anataka mzae kwanza

na wewe ukuendelea kusubiri utazaa na mika 50?

nafikiri huna choice...zaa nae hata asipokuoa angalau utakua na mtoto

tena zaa nae watoto wawili kwa haraka haraka halafu muache mwenyewe aamue kukuoa au kutokuoa.....

Reproductive age 15 - 49 years..

Missing you mingimingi
 
Inashangaza,watu wana muda wa kupoteza kiasi hiki.
 
Na yeye anapenda kupotezewa muda.

My dear follow your heart.. Deep down your heart you know what is right for you... Hakuna ajuae nafsi ya mtu inawaza nn... What if ndio ubavu wako? What if not? Moyo wa mtu ni kiza kinene sana
 
You nailed it!!! Yeye ni mrefu, ni mtu wa mazoezi lakini akiacha anakuwa na nyama uzembe. Mimi ni 5.6ft tall. Ninatembea one hour morning and another hour evening. Kwakweli magauni yananipendeza sijisifu. Kingine ninampa heshima sana kama mwanaume, ninamsikiliza. e.g. Last week nilikuwa kwenyemkutano Ijumaa wadada niliokuwa nao walitaka tuunganishe weekend huku kwasababu ni kando ya bahari na upepo ni mzuri. Aliniambia nirudi kwangu kama mkutano umekwisha, nilipanda ndege Ijumaa na sasa niko kwangu.

Woow!!! Mimi penda sana hii.... Na mwanaume anapenda mwanamke msikivu
 
Back
Top Bottom